Kumuita mtu muonga bila kurejea uongo wake hizo ni dalili za kukata tamaa na kuchanganyikiwa, zaidi inaonyesha kuwa hiyo sifa ya uongo ni sifa yenu pendwa.
Mnarudia yaleyale, kukemea ujinga kila wakati sababu mnafanya ujinga kila wakati, ninyi ndiyo mnaita uropokokaji? Mbona Magufuli alikuwa ni mropokaji wa viwango vya juu na alipewa urais na mkamshangilia? Kuna mropokaji mwingine, Paul Makonda, mpaka leo mnamkumbutia na kumshangilia, siyo kwa uwezo bali kwa ajili ya uropokaji wake hata mkaupa jina zuri eti ni uthubutu.
Ninyi mlishaamua kuwa mapunguani na sasa mnatafuta wafuasi kuongeza namba katika huo upunguani wenu.
Watu kwenda nje ya nchi inawaumeni sana. Viongozi wangapi wa serikali wanaenda nje na wengine familia zao zipo nje?
Mpaka leo kuna mijitu mnawaza kuwa mtu kwenda nje ni uhaini? Watu wamesoma nje, wameanzia maisha nje, wameoa na kuolewa nje, wana biashara wana ndugu na marafiki wengi zaidi huko.
Nyie endeleeni na mentality zenu za kuishi kimasikini nchini kuwa ndiyo uzalendo, wakati kurudi hata kwenda kusalimia tu vijijini kwenu mnaogopa kuwa mtarogwa.