Pre GE2025 Ipo siku waliotaka "kukiuka katiba" baada ya kile kifo watapewa tuzo

Pre GE2025 Ipo siku waliotaka "kukiuka katiba" baada ya kile kifo watapewa tuzo

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla, wakati na baada)
Bora umewaelewesha mkuu. Kuna watu Wana maono ya muda mfupi wakipata changamoto midogo wanafikiria njia rahisi ya kutatua ambayo mara nyingi ina athari kubwa kuliko faida.
Shida kubwa nayoona Mimi ni nchi Haina mfumo Bali inategemea individuals...Hii ni hatari mno mno...Katika nchi yenye mfumo hakuna anayeweza kufanya jambo lake Kwa maslahi binafsi akabaki salama...Hapa kwetu inaonekana Kuna watu wakiamua basi hakuna anayeweza fanya lolote na majeshi yana walinda badala ya kulinda Katiba na nchi

Inakuaje chama Cha siasa kina amua jambo ambalo halikubaliki kidemokrasia Halafu kina impact Kwa nchi na hakuna anayeweza ku object?

Inawezekanaje watu kura zinaibwa waziwazi na wezi wakabaki salama? Inawezekanaje rasilimali za nchi including pesa zinaibwa na hakuna anayejali?

Hii ndiyo inayoogopesha haswa kwamba public Haina say wala hakuna jinsi Wanaweza fanya dhidi ya kundi la watu wachache!
 
Watu siku hizi hawawazi kumtoa raisi kwenye sanduku la kura. Wanawaza mapinduzi "daah! Aisee!
 
Sasa kama Magufuli alikua na maana hiyo...

Bashiru na Kabudi wana ubaya gani...

Mheshimiwa Samia ni raisi wa tatu tangu tuanze kupata maraisi wanaocheka cheka...

Nchi ilipiga hatua gani kulinganisha na hawa wakali wawili(Nyerere na JPM)?
Samia amekusanya mapato kuliko JPM, yaani ubabe wote ule ila mama anayecheka cheka ameweza kudhibiti ukwepaji kodi!!

Baada ya JPM kufeli negotiations za bandari ya Bagamoyo, Samia ameweza na inajengwa kwa pesa za ndani sio ubia wala kukodisha.

Pia amefanikisha negotiations za mradi wa gesi kitu ambacho JPM alifeli for all 7 years kisa hakutaka kutembelea mafanikio ya JK aliyejenga bomba la gesi.

Na mengine mfano Bwawa la Nyerere, mpaka JPM anafariki halikua limefika hata 30% ila ndani ya miaka 3 pekee limemalizika!! Same to SGR ya Dar to Dodoma ilisuasua kipindi cha JPM ila Samia kamaliza in no time.

Samia katoa ajira nyingi ndani ya miaka 3 kuliko miaka yote 6 ya JPM!! cha ajabu JPM alisema haajiri sababu anajenga miradi. Mbona Mama anakamilisha miradi ya matrilioni huku bado anaajiri?

Ndio Rais aliyetoa bajeti kubwa ya Dawa na Kilimo tokea uhuru, huyo JPM na Tanzania ya viwanda alifanikiwa kipi? Ila mwenzake kajikita kwenye kilimo kwa kutoa bajeti mara 7 kuliko JPM ili Kilimo kiwe backbone ya uchumi and so far progress ni nzuri.
 
Hapa jukwaani wewe na Lumumba Malcom...

Ndio wasomi pekee mnaopingaga aina ya uongozi wa JPM na Nyerere bila hoja za msingi ...
Mimi mara zote nimempinga sera za JPM kwa facts na ndio maana huwa hazijibiwi kama wewe unaweza jibu pitia hii thread twende hoja kwa hoja kama unajiamini.

1. Nilihoji vita yake fake ya ufisadi kwamba kwanini ripoti ya ukaguzi wa mali za CCM hakuna aliyekamatwa hadi leo? Ripoti ya TAKUKURU dhidhi ya watoa rushwa kwenye chaguzi ndogo nani alikamatwa? Utoroshwaji makinikia waliotajwa wote walikua CCM nani alikamatwa hadi leo? No one ila tunaambiwa alikua mpinga ufisadi?

2. Mengine ilikua sera ya uchumi ya contractionary, kukandamiza private sector, kuua ajira, kuchukua mikopo yenye riba za kibiashara kujenga miundombinu,

Pia niliongelea mambo ya ukaguzi mfano CAG alipotaka kukagua TGFA na manunuzi ya ndege alifukuzwa!! Sasa kama ni msafi why aogope ukaguzi? Cha ajabu suala la CAG huwa mnajifanya halikutokea ila angefanya samia kama naona mngemuita fisadi wa karne!!

Nikahoji na suala la NIDA licha ya ubabe wake mpaka anafariki NIDA ilikua bado haijawahi toa vitambulisho watu wame apply tokea 2015 huko!! So JPM anapewa tu sifa na laymen wasio na facts ila ukiwa makini utaona he was a mediocre president aliyetegemea propaganda kuficha udhaifu wake.
 
Mimi nimesoma kichwa cha mada, sijasoma maelezo huko ndani na kuona nijibu hicho kichwa cha mada.
Hawa, kama kweli wanao uchungu na nchi hii, na ndiyo sababu wakataka kufanya kama inavyosemekana walipanga; basi wakati wao mzuri ni huu sasa hivi kutoka mbele na kusimamia waliyotaka yawe wakati tukielekea kwenye chaguzi.

Wakiendelea kukaa kimya, itafahamika walichotaka kufanya, kumnyima Samia u-Rais wa kuokota, zilikuwa ni njama tu za kujinufaisha wao wenyewe.
Nategemea kumsikia Ndugai, Bashiru, Kalamaganda Kabuti, Lukuvi na wengi wengine wakijitokeza wakati huu watueleze. Hata kama wanamuunga mkono huyo Samia sasa hivi, watoke tu waseme kwa nini wanamuunga mkono.
Lakini najuwa ilivyo ngumu kwa yeyote ndani ya CCM kuwa na ujasiri wa aina hiyo. Waziri mkuu wa Mkapa, ni kama ni marehemu sasa hivi. Marehemu Lowassa alikwenda kutubu, sijui kutubu kitu gani, kwa sababu sikuwahi kusikia akikinanga chama chake kwa vyovyote alipokuwa CHADEMA.

Kwa hiyo, hawa watu watueleze sasa wanaposimamia.
 
Hujitambui wewe, kuna kitu kinaitwa precedence ndio ingekua order of the day. So kama Samia angepinduliwa ingekua ndio mchezo kila Rais anayefuata angeondolewa kwa mapinduzi.

Same to fomu moja CCM, tulipiga kelele sana 2020 na 2010 humu JF kwamba ni precedence mbaya. Cha ajabu wana CCM wakamtetea JPM kuwa anakubalika sana so hakuna haja ya kugawa fomu nyingine. Leo Mama Samia naye anapewa fomu peke yake ya kugombea watu wamekua wakali ila kiini ni precedence.

Kwahiyo tamaa ya siku moja isikupande kichwani hadi ikabadili mfumo wa uongozi milele. Hao waliotaka kupindisha ilifaa wanyongwe kabisa!!

Kingine hao waliotaka kupindisha katiba sio kwamba walijua mama hawezi Urais ila wao nao walitaka kuweka Rais watakaomcontrol ili waibe zaidi. Sitaki kuamini kwa jinsi mafisadi yalivyojaa CCM kwamba yalitaka Rais "mkali", maana wangeiba wapi sasa? So wote tu walikuwa wanataka kuiba kuliko wenzao.
💯
 
Mimi mara zote nimempinga sera za JPM kwa facts na ndio maana huwa hazijibiwi kama wewe unaweza jibu pitia hii thread twende hoja kwa hoja kama unajiamini.

1. Nilihoji vita yake fake ya ufisadi kwamba kwanini ripoti ya ukaguzi wa mali za CCM hakuna aliyekamatwa hadi leo? Ripoti ya TAKUKURU dhidhi ya watoa rushwa kwenye chaguzi ndogo nani alikamatwa? Utoroshwaji makinikia waliotajwa wote walikua CCM nani alikamatwa hadi leo? No one ila tunaambiwa alikua mpinga ufisadi?

2. Mengine ilikua sera ya uchumi ya contractionary, kukandamiza private sector, kuua ajira, kuchukua mikopo yenye riba za kibiashara kujenga miundombinu,

Pia niliongelea mambo ya ukaguzi mfano CAG alipotaka kukagua TGFA na manunuzi ya ndege alifukuzwa!! Sasa kama ni msafi why aogope ukaguzi? Cha ajabu suala la CAG huwa mnajifanya halikutokea ila angefanya samia kama naona mngemuita fisadi wa karne!!

Nikahoji na suala la NIDA licha ya ubabe wake mpaka anafariki NIDA ilikua bado haijawahi toa vitambulisho watu wame apply tokea 2015 huko!! So JPM anapewa tu sifa na laymen wasio na facts ila ukiwa makini utaona he was a mediocre president aliyetegemea propaganda kuficha udhaifu wake.
Yule mzee alikuwa mzugaji sana.
 
Kwa namna mambo yalivyo na namna mambo yanavyoendelea, nashawishika kusema waliotaka kukiuka katiba baada ya kile kifo walikuwa sahihi sana.

Watu hawa wana macho makali yanayoona mbali kama ndege aina ya tai. Kiukweli pasipo inda, chuki wala choyo watu hawa wanastahili tuzo.

Mambo hivi sasa hayaendi kabisa. Nchi ni kama imesimama.
Hebu tuambie mambo gani hayo ambayo hayaendi sio unatoa lawama ambazo huzitaji pengine sababu sio rais wa nchi pengine wewe ndiyo kikwazo
 
Kwa namna mambo yalivyo na namna mambo yanavyoendelea, nashawishika kusema waliotaka kukiuka katiba baada ya kile kifo walikuwa sahihi sana.

Watu hawa wana macho makali yanayoona mbali kama ndege aina ya tai. Kiukweli pasipo inda, chuki wala choyo watu hawa wanastahili tuzo.

Mambo hivi sasa hayaendi kabisa. Nchi ni kama imesimama.
Jiwe alikua shetani mkubwa,na hao unaowasema pia ni mazuzu fulani hawana maajabu wala connection na mfumo mkuu wa nchi,
 
Tungekuw tunaongozwa na lile dubwana sasa hivi ningekuwa napembea najisemea mwenyewe kama chizi. Shukrani Samia sasa hivi maisha yangu mazuri nimepata ajira serikalini na mke wangu alienikimbia kwa ukata karudi.
Yule jamaa yeye alukuw nawaza barabara tu
Yule mbwa alikua shetani mkubwa
 
Watu walimuona Ndugai kichaa ila yule jamaa ana akili sana.
 
  • Thanks
Reactions: G4N
Kelele za chura hizo.
We baki kulalama huku watu tunafurahia maisha pengine kuliko kipindi chochote tokea nchi hii ipate uhuru. Labda kipindi cha Mwinyi tu
Wajinga hao, chini ya rais Samia maisha yamekua matamu na ya amani, tofauti na enzi za jini makata
 
Back
Top Bottom