Tindo
Platinum Member
- Sep 28, 2011
- 72,020
- 129,293
Inaonekana ulikuwa hujazaliwa, wakati wa hicho chama kimoja ndio tulivaa viraka, kupiga mswaki kwa chumvi, kufulia na majani ya mpapai. Kunywa chai ya sukari ilikuwa ni anasa. Leo hii watanzania tumekuwa makondoo ambayo kipropaganda inaitwa amani, hii ni kutokana na huo mfumo wa chama kimoja.Hatuoni umuhimu wa mfumo wa vyama vingi hapa Tanzania. Ni matapeli wa kisiasa tu ambao wapo kwa ajili ya kupiga madili na kujaza vitambi.
Watanzania ipo siku tutaandamana na kudai demokrasia ya chama kimoja ambayo huko nyuma ilitunufaisha...
Sasa rais amelazimisha nchi hii kurudi kwenye mfumo wa chama kimoja, ngoja uone tutakavyoingia kwenye aibu. Tumeanza na mgao wa umeme kwa kasi ya ajabu. Subiri usikie kama miradi itakamilika kama matamanio yalivyo.