Iramba: Serikali kupitia TARURA yatoa TZS 7bl kufungua barabara

View attachment 2052042

SERIKALI ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imetenga shilingi bilioni 7.3 kwa ajili ya kufungua barabara za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida ikiwa ni utekelezaji wa kauli mbiu yake ijulikanayo kama ‘Tunakufungulia barabara kufika kusikofikika’.

Aidha kwa niaba ya Rais Samia akiwa katika ziara ya kikazi wilayani humo,Waziri wa Nchi Ofisi ya Raia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema azma ya Serikali ni kufungua barabara za vijijini ili wananchi waweza kufanya kazi zao bila kikwazo cha usafiri.

Akikagua barabara ya Shelui - Tintigulu inayojengwa kwa urefu wa kilomita saba, Waziri ameelekeza barabara hiyo ijengwe kwa ubora unaotakiwa ili iweze kudumu na kuwasaidia wananchi wa Shelui katika shughuli zao za kila siku.

"Lengo la Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuwafungulia wananchi wa vijijini barabara ili isiwe kikwazo tena katika shughuli zao na hapa nimeona baada ya barabara hii kukamilika inakwenda kufungua na kurahisisha mawasiliano ya kata tatu na vijiji sita,"amesema.

Pia Waziri Ummy alimuelekeza Meneja wa TARURA Wilaya ya Shelui, Mhandisi Evance Kibona kuhakikisha kuwa wanafanya usanifu wa Daraja la Nshoka linalounganisha kata za Shelui - Tintigulu ili barabara hiyo inayojengwa iweze kuleta manufaa zaidi kwa wananchi wa maeneo hayo.

"Nimekagua ujenzi wa barabara, umeanza lakini nimeona kuna mto Nshoka ambao unatakiwa kujengewa daraja ili barabara hii inayojengwa iweze kuleta manufaa, vinginevyo bado watakuwa wanapata usumbufu wakati wa mvua nataka tumalize kabisa changamoto hii.

"Mto huu ni mkubwa na hakuna daraja sasa wakati wa mvua wananchi hawawezi kupita hapa hivyo ni vyema hapa pakajengwa daraja ili barabara hii iwe na tija stahiki, hivyo wahandisi anzeni kufanya usanifu na muingize kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 tuweke ujenzi wa daraja hili kwenye bajeti yetu.

Akizungumza wakati wa ukaguzo wa barabara hiyo ya Shelui-Tintigulu Meneja wa TARURA Wilaya ya Iramba, Mhandisi Evance Kibona amesema, ujenzi wa barabara hiyo umeanza Desemba 11 na utakamilika Juni,2022.
Binafsi naamini its better kusema serikai imetoa pesa kuliko kusema rwis ametoa pesa

Hizi sentiments kuna siku zitatucost (na zimeshawahi kutucost pale ambapo mtu alifikia hatua ya kufanya pesa zote kuwa zake)

Turudi kwenye ustaarabu wetu wa jadi
 
Mkuu hebu soma aya ya kwanza ya habari hii,
 
View attachment 2052042

SERIKALI ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imetenga shilingi bilioni 7.3 kwa ajili ya kufungua barabara za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida ikiwa ni utekelezaji wa kauli mbiu yake ijulikanayo kama ‘Tunakufungulia barabara kufika kusikofikika’.

Aidha kwa niaba ya Rais Samia akiwa katika ziara ya kikazi wilayani humo,Waziri wa Nchi Ofisi ya Raia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema azma ya Serikali ni kufungua barabara za vijijini ili wananchi waweza kufanya kazi zao bila kikwazo cha usafiri.

Akikagua barabara ya Shelui - Tintigulu inayojengwa kwa urefu wa kilomita saba, Waziri ameelekeza barabara hiyo ijengwe kwa ubora unaotakiwa ili iweze kudumu na kuwasaidia wananchi wa Shelui katika shughuli zao za kila siku.

"Lengo la Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuwafungulia wananchi wa vijijini barabara ili isiwe kikwazo tena katika shughuli zao na hapa nimeona baada ya barabara hii kukamilika inakwenda kufungua na kurahisisha mawasiliano ya kata tatu na vijiji sita,"amesema.

Pia Waziri Ummy alimuelekeza Meneja wa TARURA Wilaya ya Shelui, Mhandisi Evance Kibona kuhakikisha kuwa wanafanya usanifu wa Daraja la Nshoka linalounganisha kata za Shelui - Tintigulu ili barabara hiyo inayojengwa iweze kuleta manufaa zaidi kwa wananchi wa maeneo hayo.

"Nimekagua ujenzi wa barabara, umeanza lakini nimeona kuna mto Nshoka ambao unatakiwa kujengewa daraja ili barabara hii inayojengwa iweze kuleta manufaa, vinginevyo bado watakuwa wanapata usumbufu wakati wa mvua nataka tumalize kabisa changamoto hii.

"Mto huu ni mkubwa na hakuna daraja sasa wakati wa mvua wananchi hawawezi kupita hapa hivyo ni vyema hapa pakajengwa daraja ili barabara hii iwe na tija stahiki, hivyo wahandisi anzeni kufanya usanifu na muingize kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2022/23 tuweke ujenzi wa daraja hili kwenye bajeti yetu.

Akizungumza wakati wa ukaguzo wa barabara hiyo ya Shelui-Tintigulu Meneja wa TARURA Wilaya ya Iramba, Mhandisi Evance Kibona amesema, ujenzi wa barabara hiyo umeanza Desemba 11 na utakamilika Juni,2022.
Ikumbukwe kuwa hizo pesa zinatolewa na wananchi hususani maskini wanaokamuliwa kila siku kupitia tozo mbalimbali za miamala na malipo.

Ikumbukwe vilevile kuwa bidhaa zinapanda bei kila siku inayoitwa leo ili hali vipato havijaongezeka. Kwa busara ilikuwa ni vema kuwapongeza wananchi wanaovumilia tozo ambazo ndizo zinajenga hiyo miundombinu badala ya kumpongeza Rais anayepanga matumizi.

Krismasi Njema!
 
Rais anafanya kazi kwa niaba yetu mkuu, Asante X-mass njema na kwako pia,
 
Mkuu hebu soma aya ya kwanza ya habari hii,
Na wewe soma title ya habari… hakuna waandishi wa habari wa hovyo kama wa kwetu… samia stoa pesa kumfungulia mwigulu barabara… what about the government? What about the people?

Wameacha principles za uandishi kabisa

Rais Samia atoa TZS 7.3BL kumfungulia barabara Dkt Mwigulu Nchemba Iramba,​

Rais ni taasisi mjomba, Rais ndio mshauri mkuu wa Gvnt budget
 
Hata kama macho hayaoni ata majirani huwasikii wakisemasema huko mtaani kwenu kazi za mama?
 
Rais ni taasisi mjomba, Rais ndio mshauri mkuu wa Gvnt budget
Rais ni taasisi… very true

Lakini serikali ila muundo wake na mfumo wake wa ufanyaji kazi…. Don’t deresponsibilitize people ili badae mdilute roles za key people in the system who offer quality technical services

This was not our culture before president Magufuli

Msilete perepete zenu
 
Unachukia vile Rais Samia anapiga kazi?
 
hii namna ya reporting kama samia ndio mwenye hizi hela binafsi yake ni aina fulani ya kipindi cha ujima na upumbavu

Sema state imetoa pesa kiasi hiki na hiki kwa ajili ya shughuli hii na hii

I wonder miaka 50 from now vitukuu vikija kusoma huu upumbavu wetu humu itakua ni kesi
CHADEMA inawauma sana hii performance ya Rais wetu aise
 
State ndio nini, Hata wewe mbona hujui zaidi yake?
duuh

nimezungumzia kitu very professional aisee wewe umegeuza namuonea wivu mtu asiejua lolote kama samia?

Samia kwenye account personal ana hata shilingi mia to her name?

Nothing

Truth ni kwamba ,ni state imetoa not these matarishi ndugu!
 
Aise kila kona ya nchi kuna mradi mpya wa Rais Samia unaendelea,

Huyu mama atawala mpaka achoke aise
Hii sio miradi ya samia, ni miradi ya serikali, serikali ndio inatoa hela kupitia kodi yako pamoja na misaada na mikopo kutoka ndani/nje. samia hatoi chochote na hata kodi halipi.
 
Hahahaa

Hujui maana ya State mkuu?

Shule ulisomeshwa na wazazi wako kwa hasara

Si ajabu maana hata jina lako hujui jinsi la kuliandika sawasawa,umeandika Bitcoine badala ya Bitcoin,kuna ujinga mwingi unao ndio maana!
Hahaha,

Sasa maswala ya jina langu unataka unifundishe tena namna ya kuliandika?

Wewe hujui ata nini maana ya "State "

Elewa Rais ni taasisi mjomba
 
Back
Top Bottom