Iramba: Serikali kupitia TARURA yatoa TZS 7bl kufungua barabara

Iramba: Serikali kupitia TARURA yatoa TZS 7bl kufungua barabara

Iramba kwa mara ya kwanza katika historia inapokea mzigo wa TZS 7.3BL za barabara,

#IRAMBA TUMUUNGE MKONO RAIS WETU ANAFANYA MAMBO MAKUBWA,
Na mlikua na mbunge tena anapenda mipasho kumbe barabara hakuna jimboni kwake
 
Khaaaa, Kwakweli huyu Mama anajitahidi sana, Iramba haikuwa na Barabara kabisa, Kazi nzuri sana Rais wetu
Nilitegemea mumuwajibishe mbunge wenu inakuaje miaka nenda rudi hamna barabara? Huduma nyeti kama hiyo, wakulima wananufaika vipi na kufikisha mazao yao sokoni
 
View attachment 2052042

SERIKALI ya Rais Samia Suluhu Hassan kupitia Wakala wa Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imetenga TZS 7.3BL kwa ajili ya kufungua barabara za Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mkoani Singida ikiwa ni utekelezaji wa kauli mbiu yake ijulikanayo kama ‘Tunakufungulia barabara kufika kusikofikika’.

Aidha kwa niaba ya Rais Samia akiwa katika ziara ya kikazi wilayani humo,Waziri wa Nchi Ofisi ya Raia Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mheshimiwa Ummy Mwalimu amesema azma ya Serikali ni kufungua barabara za vijijini ili wananchi waweza kufanya kazi zao bila kikwazo cha usafiri.

Akikagua barabara ya Shelui - Tintigulu inayojengwa kwa urefu wa kilomita saba, Waziri ameelekeza barabara hiyo ijengwe kwa ubora unaotakiwa ili iweze kudumu na kuwasaidia wananchi wa Shelui katika shughuli zao za kila siku.

"Lengo la Serikali ya Awamu ya Sita chini ya Rais Samia Suluhu Hassan ni kuwafungulia wananchi wa vijijini barabara ili isiwe kikwazo tena katika shughuli zao na hapa nimeona baada ya barabara hii kukamilika inakwenda kufungua na kurahisisha mawasiliano ya kata tatu na vijiji sita,"amesema.

Pia Waziri Ummy alimuelekeza Meneja wa TARURA Wilaya ya Shelui, Mhandisi Evance Kibona kuhakikisha kuwa wanafanya usanifu wa Daraja la Nshoka linalounganisha kata za Shelui - Tintigulu ili barabara hiyo inayojengwa iweze kuleta manufaa zaidi kwa wananchi wa maeneo hayo.

"Nimekagua ujenzi wa barabara, umeanza lakini nimeona kuna mto Nshoka ambao unatakiwa kujengewa daraja ili barabara hii inayojengwa iweze kuleta manufaa, vinginevyo bado watakuwa wanapata usumbufu wakati wa mvua nataka tumalize kabisa changamoto hii.

"Mto huu ni mkubwa na hakuna daraja sasa wakati wa mvua wananchi hawawezi kupita hapa hivyo ni vyema hapa pakajengwa daraja ili barabara hii iwe na tija stahiki, hivyo wahandisi anzeni kufanya usanifu na muingize kwenye bajeti ya mwaka wa fedha 2022|23 tuweke ujenzi wa daraja hili kwenye bajeti yetu.

Akizungumza wakati wa ukaguzo wa barabara hiyo ya Shelui-Tintigulu Meneja wa TARURA Wilaya ya Iramba, Mhandisi Evance Kibona amesema, ujenzi wa barabara hiyo umeanza Desemba 11 na utakamilika Juni,2022.

Wilaya ya Iramba ilikuwa na majimbo mawili ya Iramba mashariki|Mkalama na Iramba magharibi kabla ya Mkalama kuwa Wilaya, Jimbo la Iramba Magh linaloongozwa na Waziri wa fedha na Mipango Dkt Mwigulu Nchemba,Iramba Kaziiendelee
kazi nzuri sana hii
 
Binafsi naamini its better kusema serikai imetoa pesa kuliko kusema rwis ametoa pesa

Hizi sentiments kuna siku zitatucost (na zimeshawahi kutucost pale ambapo mtu alifikia hatua ya kufanya pesa zote kuwa zake)

Turudi kwenye ustaarabu wetu wa jadi
Fact sana mkuu ,kwa maana hajatoa mfukoni mwake
 
Aise kila kona ya nchi kuna mradi mpya wa Rais Samia unaendelea,

Huyu mama atawala mpaka achoke aise
Huo unaoongea ni unafiki. Samia anaweza kutoka, wakaja wazuri zaidi yake?

Kuna msemo usemao, always the best are not yet born. Nyuma yetu wanakuja wazuri zaidi.
 
Ila umma ndio wenye mamlaka,
Hakuna upuuzi kama huo. Samia atamaliza muda wake wa miaka 5 au 10, ataonfoka. Watakuja wengine, ndiyo itaratibu. Watu wenye hekima na akili hufiata itaratibu.

Diku zote watu wenye akili na hekima hupenda kufuata utaratibu. Rais Samia kama ana akili na hekima, hawezi kukubali ujinga wa eti kuongezewa muda. Maana hayo ni maneno ya wanafiki wajinga.
 
Hakuna upuuzi kama huo. Samia atamaliza muda wake wa miaka 5 au 10, ataonfoka. Watakuja wengine, ndiyo itaratibu. Watu wenye hekima na akili hufiata itaratibu.

Diku zote watu wenye akili na hekima hupenda kufuata utaratibu. Rais Samia kama ana akili na hekima, hawezi kukubali ujinga wa eti kuongezewa muda. Maana hayo ni maneno ya wanafiki wajinga.
Ndio, Kumi inatosha, Katiba lazima iheshimiwe japo tunamuhitaji zaidi ya miaka 20
 
Team JF,


MERRY CHRISTMAS AND HAPPY NEW YEAR 2022.

#TUENDELEE KUMUUNGA MKONO RAIS WETU,
 
Kuna comments za kinafiki humu, huu uzi upewe tuzo haa haahaa haa, daah!

Everyday is Saturday................................😎
 
Back
Top Bottom