Iran imetangaza kulipiza tena Kisasi kwa Israel baada ya shambulizi huko Syria

Iran imetangaza kulipiza tena Kisasi kwa Israel baada ya shambulizi huko Syria

Amiri Jeshi Mkuu wa Jeshi la Walinzi wa Mapinduzi ya Kiislamu nchini Iran Hossein Salami ametangaza Israel isubiri jibu baada ya mauaji ya mshauri wao wa kijeshi nchini Syria Saeed Abyar.

Shambulizi hilo la anga ambalo limetokea Aleppo juzi June 3 limeua watu 17 ambao inaelezwa ni wapiganaji wanaoiunga mkono Iran ambapo afisa wa jeshi ambae ni mshauri wa kijeshi nchini Syria Saeed Abyar ni miongoni mwa waliofariki kwenye shambulio hilo.

PIA SOMA:
- Israel yaua Jenerali mwingine wa Iran nchini Syria
Iran nao wanabwabwaja sana kuliko vitendo
 
Netanyahu alisema kifo cha rais wa Iran ni sawa na kisasi kidogo saana. Jibu limo humo ndani ya fumbo, kuna ndio na hapana
Netanyahu alitanguliza kusema ISRAEL HAIHUSIKI NA KIFO CHA EBRAHIM RAISI.
Na Israel haiwezi lipiza kisasi kidogo hivyo.
Tunajielewa humu sio watoto.
 
Iran nao wanabwabwaja sana kuliko vitendo
Iran ina vita ya kiuchumi kabla ya hizo vita za silaha.
Mshukuruni sana rais mpya aliyesema Iran inatakiwa ijihusishe na uchumi sio kuendekeza mapigano.
Laa sivyo Israel wangeipata fresh.
 
Back
Top Bottom