Hammaz
JF-Expert Member
- May 16, 2018
- 6,607
- 14,076
Ukimgusa Israel ujue unapambana na Amerika. Kama kuogopwa anaogopwa Marekani si Israel.Hawezi kabisa. Lakini huwa hapendi kuonekana mnyonge, atajaribu kwa namna yeyote kulipiza kisasi.
Marekani kwenye hii vita anamsaidia kumpelekea wataalamu wa ki vita, msaada wa silaha na mabomu kwa sababu Israel alikuwa ameshaishiwa.
Marekani anamsaidia kuwadhibiti Houth kwa kulinda anga la Israel kupitia baharini.
Marekani anamsaidia kuwadhibiti Hizbullah ambao hata kwenye channel zao Israel wanadiriki kusema kwa nafasi Hizbullah waliyofikia sasa hivi ni lazima na wao watapata madhara makubwa ya moja kwa moja.
Marekani anamsaidia msaada wa kifedha ili Israel iweze kuendesha gharama za vita kwani uchumi wa Israel umeshuka sana.
Marekani imemsaidia pia kumkingia kifua dhidi ya maazimio mengi juu yake Israel kwenye vikao vya usalama vya umoja wa mataifa (UN).