Mnap
Mnapoandika, kwanza muwe mnajiuliza kama mna uelewa wa kutosha kuhusiana na jambo mnaloenda kuliandika.
Hivi hayo mataifa yote, hasa hayo ya Kiarabu, kama Iran akiipiga Israel, yanaumizwa na nini?
Hayo mataifa yote yanayoitaka Iran isijaribu kuishambulia Israel, yana watu wenye hekima, wanaojua madhara makubwa yatakayowapata wananchi, zaidi kwa upande wa Iran, na kiasi kwa Waisrael, na kwa kiasi kudogo sana kwa wananchi wa mataifa yao, kuanzia usalama, na zaidi kwenye uchumi. Ufahamu kuwa Israel haipakani na Iran, ili Iran ipigane na Israel, ni lazima viwe vita vya anga, na kwenye vita vya anga, Iran ni dhaifu sana ukilinganisha na Israel. Karibuni tu hapo Iran iliporusha msululu wa maroketi na drones kwa Israel, hayakuwa na madhara yoyote makubwa. Israel ilishambulia mara moja tu Iran, na ikawa kwenye target, ikateketeza mtambo uliotumika kurusha makombora, na Iran ikawa kimya.
Iran ikianza kurusha makombora dhidi ya Israel, mengi yatadunguliwa na kuangukia ndani ya mataifa mengine, na mabaki hayo yanaweza kuleta madhara kwa mataifa hayo. Na pia tafiti za kitaalam kwenye mambo ya kivita, zinasema kuwa Iran ina silaha nyingi lakini ni outdated, za tekinolojia duni, zisizo na precisjon. Mfano mmojawapo umeona hata chopa iliyomwua Rais wao. Kutokana na kasoro hizo, inaweza kutokea ikalenga makombira yakatue Israel, halafu mengine yakaishia kudondokea katika mataifa mengine kwa kukosa precision. Ndiyo maana mataifa hayo, hayataki hilo litokee.
Lakini pia, Iran inachukiwa na mataifa karibia yote ya Mashariki ya kati kwa sababu ni nchi inayoanzisha na kuyafadhili makundi ya kigaidi dhidi ya Serikali zote zisizo za kishia. Ndiyo maana usishangae, siku Iran ikirusha makombora kwenda Israel, mengi yatadunguliwa na mataifa ya kiarabu kabla hayajaingia kwenye anga la Israel, kama ilivyotokea safari iliyopita.
Mataifa karibia yote ya kiarabu yana mahusiano mazuri na Israel, japo siyo kwa uwazi sana, kwa sababu Israel ndiye mbabe wa kukabiliana na Taifa la kigaidi la Iran. Mataifa ya kiarabu wala hayana huruma na magaidi ya Hamas, Hezbollah n.k., yanaumizwa na mauaji ya wapalestina wasio na hatia, kama ambavyo imekuwa kwa nchi nyingi za Ulaya.
Sasa ukiwa na akili ndogo na uelewa mdogo, utachukulia mambo kama ulivyoyachukulia.