Iran: Milipuko ilisikika mjini Tehran huku Israel ikithibitisha mashambulizi

Chanzo ni CNN
Inasemekana Israel imeanza mashambulizi yake ya kulipiza kisasi kama ilivyo ahidi kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya Iran nchini Israel mnamo tarehe 1 Oct 2024, nchini Iran milipuko kadhaa imesikika ndani ya
Tehran muda huu.

IDF inasema inalenga maeneo ya kijeshi nchini Iran.

Siku ya ijumaa ndege za kimarekani aina ya F16 ziliingia mashariki ya kati kutokea Germany ambapo ilisemekana zitatumika kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi nchini Iran, ndege zilizopelekwa ni pamoja na F16 F15E, F22 na A-10, pia Pentagon ilipeleka mitambo ya ulinzi wa anga aina ya THAAD, ikumbukwe septemba Pentagon ilisema itaongeza askari zaidi , mifumo ya ulinzi wa anga na askari zaidi mashariki ya kati kwa kile kinachodaiwa uwezekano wa migogoro ya Israel na Iran.

Source
🤣🤣

Hivi si ulisema Israel imefyata na haitojibu mapigo?

Imekuwaje tena sasa?
 
Ayatollah amesema askari wajiandae kurusha makombora 1000, sasa hapo kumenoga.
Kulikuwa hamna ndege yoyote iliyokuwa inapaa anga ya Syria na nothern Iraq 26. Mteule maamae akaamua atawale anga pekee yake.

Screenshot_20241026-033803.jpg
 
Hayawi-hayawi mwisho imekuwa baada ya majeshi ya israel kuanza kuwapiga mbwa usiku huu Majeshi hayo ya Israel yameanza kumpiga Mwenye Mbwa yaani Iran mpaka sasa ninavyoandika hapa hukoanachapika vizuri sana.
Several loud explosions have been heard in Iran's capital Tehran and Israel has confirmed it has launched strikes on military targets.

The Israeli military said it is conducting "precise strikes" on military targets in Iran in response to what it called "the continuous attacks from the regime in Iran against Israel".
Nina wasi wasi na afya ya ubongo wako huenda uliangushwa ukiwa utoton
 
Netanyahu anachofanya ni kujitafutia matatizo, hapo alipo kwake amekimbia kwa kukoswa na drone la hezbollah lililopiga nyumba yake, haijulikani anaishi lodge au hostel halafu bado anachokoza tena tehran.

Lakini IDF waesema wanalenga military targets, hawei kuleta ule usenge wake kwenda kupiga raia, tena hapo USA kawaambia msithubutu kuua raia yeyote wa Iran.

Ninasoma muda huu USA inasema haihusiki na mashambulizi nchini Iran...[emoji1787]
Raia watafikiwa tu, maana wataambiwa wahame makazi ili kuepusha kugeuzwa kuwa ngao. Wakikaidi watapigwa.
 
Chanzo ni CNN
Inasemekana Israel imeanza mashambulizi yake ya kulipiza kisasi kama ilivyo ahidi kulipiza kisasi kwa mashambulizi ya Iran nchini Israel mnamo tarehe 1 Oct 2024, nchini Iran milipuko kadhaa imesikika ndani ya
Tehran muda huu.

IDF inasema inalenga maeneo ya kijeshi nchini Iran.

Siku ya ijumaa ndege za kimarekani aina ya F16 ziliingia mashariki ya kati kutokea Germany ambapo ilisemekana zitatumika kufanya mashambulizi ya kulipiza kisasi nchini Iran, ndege zilizopelekwa ni pamoja na F16 F15E, F22 na A-10, pia Pentagon ilipeleka mitambo ya ulinzi wa anga aina ya THAAD, ikumbukwe septemba Pentagon ilisema itaongeza askari zaidi , mifumo ya ulinzi wa anga na askari zaidi mashariki ya kati kwa kile kinachodaiwa uwezekano wa migogoro ya Israel na Iran.

Source
Kumbe ni Marekani inamlipia kisasi Israel halafu sisi tunaisifia Israel kuwa ni mwamba
 
🤣🤣

Hivi si ulisema Israel imefyata na hata nini mapigo?
Si unaona wamesubiri hadi US kapeleka ndege vita za kutosha, kuna F22, F16, F15E na A 10...
Ngoja tusubiri madhara watakayosababisha, hata hapo wameshambulia kwa uoga mkubwa ni ile basi tu wasionekane wanyonge.

Ni ile unapigwa ngumi nzito hadi jino linatoka halafu unarudisha kibao kama unaua mbu kwa sababu ya uoga.

Tutaona hapa baadae hayo mashambulizi wametumia ndege vita, misiiles za masafa ama drones? na wameshabulia sehemu ngapi? tuendelee kusubiri..
 
25 October 2024

Shalom Shalom

:FIRE: Mashambulizi ya Angani ya IDF Yalenga Maeneo Nyeti Iran, Yamegonga pia Makao Makuu ya Jeshi la Iran IRGC, Milipuko Mingi ya Yatetemesha jiji la Tehran

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limethibitisha kufanya mashambulizi ya anga ya kulipiza kisasi katika maeneo yaliyolengwa nchini Iran.

Huku milipuko mikubwa ikiripotiwa mjini Tehran na karibu na Karaj usiku huu wa giza, Jumamosi. Vyombo vya habari vyenye uhusiano na serikali ya Iran, vikiwemo Fars News, viliripoti milipuko karibu na maeneo muhimu, ukiwemo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeini.

Vyombo rasmi vya serikali ya Iran vimethibitisha Milipuko kadhaa kusikika mjini Tehran, kwa mujibu wa shirika la habari la Fars la Iran. Nalo Shirika rasmi la habari la Tasnim liliripoti kuwa milipuko kadhaa ilisikika magharibi mwa mji mkuu wa Iran. Milipuko hiyo inakuja wakati eneo hilo likijiandaa kukabiliana na malipizi ya Israel kufuatia shambulio la Iran mapema mwezi huu.
 
Si unaona wamesubiri hadi US kapeleka ndege vita za kutosha, kuna F22, F16, F15E na A 10...
Ngoja tusubiri madhara watakayosababisha, hata hapo wameshambulia kwa uoga mkubwa ni ile basi tu wasionekane wanyonge.

Ni ile unapigwa ngumi nzito hadi jino linatoka halafu unarudisha kibao kama unaua mbu kwa sababu ya uoga.

Tutaona hapa baadae hayo mashambulizi wametumia ndege vita, misiiles za masafa ama drones? na wameshabulia sehemu ngapi? tuendelee kusubiri..
Hoja haikuwa US kupeleka ndege. Hoja ilikuwa ni Israel kujibu.

Wamejibu.
 
Raia watafikiwa tu, maana wataambiwa wahame makazi ili kuepusha kugeuzwa kuwa ngao. Wakikaidi watapigwa.
Unafikri Gaza hio, dunia ya sasa sio ya mwaka ule 2003 US na propaganda zake anawachota akili mataiifa zaidi ya 40 kwenda kumshambulia Sadam Hussein.

Nchi nyingi hivi sasa wamepata uelewa mkubwa wa kile kinachoendelea duniani, ndio maana unaona hivi sasa mataifa makubwa yenye nguvu yanataka kujiunga BRICS, usitegemee Iran itavamiwa kama Iraq, thubutuuu na haitotokea...

USA yenyewe imekuwa wa kwanza kuishauri Israel isishambulie sehemu za nuclear na mafuta eti kwa kigezo cha kusababisha inflation ya bei za mafuta, wakati wenyewe ndio wamewawekea vikwazo hao Iran toka 1970s...

Ukweli ni kwamba US kawaambia Israel indirect mkipiga seheu za mafuta za Iran na vinu vya nuclear mtakuwa kwenye hali ngumu...
 
630167.jpeg
 
Si unaona wamesubiri hadi US kapeleka ndege vita za kutosha, kuna F22, F16, F15E na A 10...
Ngoja tusubiri madhara watakayosababisha, hata hapo wameshambulia kwa uoga mkubwa ni ile basi tu wasionekane wanyonge.

Ni ile unapigwa ngumi nzito hadi jino linatoka halafu unarudisha kibao kama unaua mbu kwa sababu ya uoga.

Tutaona hapa baadae hayo mashambulizi wametumia ndege vita, misiiles za masafa ama drones? na wameshabulia sehemu ngapi? tuendelee kusubiri..
Dunia hii ilivyo na mambo mengi chini ya kapeti, ukute hapo walishafikia makubaliano pande mbili na kuihusisha Russia kuwa Iran iwape baadhi ya target zao za kijeshi wazipige ili kulimaliza hili suala na ionekane KISASI KIMELIPWA. Haiingii akilini taifa kama Israel lipigwe halafu eti iwachukuwe karibia mwezi kujipanga kulipa kisasi. Israel tunayoijua hujibu papo kwa papo.

Hii ya kusubiria muda wote huo ninaamini kulikuwa na majadiliano ya pande mbili yalikuwa yakiendelea.
 
Wakati mashambulizi yanafanyika nimesikia Netanyahu yupo kwenye bunker kajificha katika kambi moja inaitwa Kirya na Yoav Gallant.
Hawezi kutoka hadi wiki iishe.
Hiyo picha ni ya kikao teule ni ya leo mkuu wakati precise strike na target zilipokuwa zinaendelea maamae.

Courtesy

Jerusalem Post
 
Back
Top Bottom