Iran: Milipuko ilisikika mjini Tehran huku Israel ikithibitisha mashambulizi

🤣🤣

Hivi si ulisema Israel imefyata na haitojibu mapigo?

Imekuwaje tena sasa?
 
Nina wasi wasi na afya ya ubongo wako huenda uliangushwa ukiwa utoton
 
Raia watafikiwa tu, maana wataambiwa wahame makazi ili kuepusha kugeuzwa kuwa ngao. Wakikaidi watapigwa.
 
Kumbe ni Marekani inamlipia kisasi Israel halafu sisi tunaisifia Israel kuwa ni mwamba
 
🤣🤣

Hivi si ulisema Israel imefyata na hata nini mapigo?
Si unaona wamesubiri hadi US kapeleka ndege vita za kutosha, kuna F22, F16, F15E na A 10...
Ngoja tusubiri madhara watakayosababisha, hata hapo wameshambulia kwa uoga mkubwa ni ile basi tu wasionekane wanyonge.

Ni ile unapigwa ngumi nzito hadi jino linatoka halafu unarudisha kibao kama unaua mbu kwa sababu ya uoga.

Tutaona hapa baadae hayo mashambulizi wametumia ndege vita, misiiles za masafa ama drones? na wameshabulia sehemu ngapi? tuendelee kusubiri..
 
25 October 2024

Shalom Shalom

Mashambulizi ya Angani ya IDF Yalenga Maeneo Nyeti Iran, Yamegonga pia Makao Makuu ya Jeshi la Iran IRGC, Milipuko Mingi ya Yatetemesha jiji la Tehran

Jeshi la Ulinzi la Israel (IDF) limethibitisha kufanya mashambulizi ya anga ya kulipiza kisasi katika maeneo yaliyolengwa nchini Iran.

Huku milipuko mikubwa ikiripotiwa mjini Tehran na karibu na Karaj usiku huu wa giza, Jumamosi. Vyombo vya habari vyenye uhusiano na serikali ya Iran, vikiwemo Fars News, viliripoti milipuko karibu na maeneo muhimu, ukiwemo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Imam Khomeini.

Vyombo rasmi vya serikali ya Iran vimethibitisha Milipuko kadhaa kusikika mjini Tehran, kwa mujibu wa shirika la habari la Fars la Iran. Nalo Shirika rasmi la habari la Tasnim liliripoti kuwa milipuko kadhaa ilisikika magharibi mwa mji mkuu wa Iran. Milipuko hiyo inakuja wakati eneo hilo likijiandaa kukabiliana na malipizi ya Israel kufuatia shambulio la Iran mapema mwezi huu.
 
Hoja haikuwa US kupeleka ndege. Hoja ilikuwa ni Israel kujibu.

Wamejibu.
 
Raia watafikiwa tu, maana wataambiwa wahame makazi ili kuepusha kugeuzwa kuwa ngao. Wakikaidi watapigwa.
Unafikri Gaza hio, dunia ya sasa sio ya mwaka ule 2003 US na propaganda zake anawachota akili mataiifa zaidi ya 40 kwenda kumshambulia Sadam Hussein.

Nchi nyingi hivi sasa wamepata uelewa mkubwa wa kile kinachoendelea duniani, ndio maana unaona hivi sasa mataifa makubwa yenye nguvu yanataka kujiunga BRICS, usitegemee Iran itavamiwa kama Iraq, thubutuuu na haitotokea...

USA yenyewe imekuwa wa kwanza kuishauri Israel isishambulie sehemu za nuclear na mafuta eti kwa kigezo cha kusababisha inflation ya bei za mafuta, wakati wenyewe ndio wamewawekea vikwazo hao Iran toka 1970s...

Ukweli ni kwamba US kawaambia Israel indirect mkipiga seheu za mafuta za Iran na vinu vya nuclear mtakuwa kwenye hali ngumu...
 
 
Dunia hii ilivyo na mambo mengi chini ya kapeti, ukute hapo walishafikia makubaliano pande mbili na kuihusisha Russia kuwa Iran iwape baadhi ya target zao za kijeshi wazipige ili kulimaliza hili suala na ionekane KISASI KIMELIPWA. Haiingii akilini taifa kama Israel lipigwe halafu eti iwachukuwe karibia mwezi kujipanga kulipa kisasi. Israel tunayoijua hujibu papo kwa papo.

Hii ya kusubiria muda wote huo ninaamini kulikuwa na majadiliano ya pande mbili yalikuwa yakiendelea.
 
Wakati mashambulizi yanafanyika nimesikia Netanyahu yupo kwenye bunker kajificha katika kambi moja inaitwa Kirya na Yoav Gallant.
Hawezi kutoka hadi wiki iishe.
Hiyo picha ni ya kikao teule ni ya leo mkuu wakati precise strike na target zilipokuwa zinaendelea maamae.

Courtesy

Jerusalem Post
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…