Iran ni nchi ya maajabu sana

Tatizo wao ndio wanaojishtukia, lkn swala hili halihusiani na dini ya mtu.

Bali tunazungumzia uhalisia wa kweli dhidi ya propaganda za uongo walizoaminishwa watu huko zaman kabla ya kuja kuuona kweli.
Yeap wataleta hoja za udini
 
Vipi kuhusu UGANDA, EQUATORIAL GUINEA, NA CENTRAL AFRICAN STATE vipi Hizi nchi zimeendelea Sana kuliko Tanzania?...
 
Umeizungumzia Israel kwa mwonekano bila kugusia misingi ya nchi ya Israel kuanzishwa kwake na uimara wake,sijafahamu Imani ya dini yako,lakini kama ni Mkristo basi soma Biblia kitabu cha Mwanzo na kutoka utafahamu mengi na hata haya uliyoyaandika,kufanywa utumwa,kutawanyika kwao Dunian,kukusanyika kwao na kuundwa kwa hili Taifa utayapata...kifupi Israel ndio wenye nguvu kuliko hayo mataifa ya Ulaya na Marekani uliyosema,Iran alisha tamka kulifuta hilo Taifa lakini hatakaa aweze.
Jiulize Israel anazungukwa na maadui kote lkn bado anatoboa unafikiri ni rahisi?hilo ni Taifa teule japo wengi hawapendi kusikia likiitwa teule,lakini ndio ukweli mchungu.

Hili Taifa limepitia misukosuko mingi sana,hiyo uliyaandika hapo ni michache mno,rudi kwenye Biblia kalisome hili Taifa ndipo utalifahamu vizuri,huwezi pigana na Israel ukashinda maana mkono wa Mungu uko na hilo Taifa,kwa wale Wakristo wanasoma Biblia wanafahamu ninachozungumzia,lkn kama hausomi Biblia huwezi elewa haya.
 
Ukimpiga chura teke unampa mwendo zaidi,angalia Russian,North Korea,Irani,Hata akina China but matokeo ya kutumia akili zao wakijua maandui zao kamwe hawayataki maendeleo yao🏃🏃
 
Tatizo lako mkuu unajihisi uko smart na unajua vitu kuliko wengine,hilo ni tatizo kubwa mno....ukitaka kufahamu vitu vingi,soma na ukubali kujifunza kwa wengine,tambua wapo waliokutangulia wenye ufahamu wa mambo kukuzidi...bandiko lako unataka kutuaminisha ilani ina nguvu kuliko mataifa mengine,wanaweza kua na nguvu kwa sehemu flani,lkn hanawa huo uwezo kuzidi tunayoyaita Mataifa makubwa kama Marekani,China na Russia...kutengeneza hizo drones ambazo rada za mataifa mengine zinapata shida kuzisoma haina maana kwamba wao wako top...na kifupi soon watazigundua,huyo Muiran,Muisrael tu hapo hamuwezi ukatae ukubali huo ndio ukweli.
 
Nyuzi kama hizi huwa zinachekesha sana.....ukitazama unaweza kuzani wa Iran na Waisrael wanabishana kumbe ni wamatumbi wenzetu walioamua kuwa watumwa wa fikra za watu wengine.............

Na wote sources zao ni google na articles za mitandaoni...........hapa watu watatukanana na kudhalilishana Kwa mambo haya ya kipuuzi......lakini huwezi kukuta nchi zingine watu wanabishana na kutukanana kuhusu mambo ya nchi zingine.....
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Tatizo la wayahudi wa buza kila jambo linalohusu Iran au Palestina wao wanalichukulia kiimani ya dini, hata kama hakuna uhusian wowote kati ya dini na jambo husika.
Waambie mwamposa anawaita
Instead ya kuleta ujuha humu
 
Mwenye akili na mfuatiliaji kuhusu Iran anajua kwanini anachungwa sana na kuzuiwa kufanya mengi na hata vikwazo vingi kuwekewa

Iran ana wataalamu wengi sana na ni akili kubwa
Amejiwekeza kwenye maendeleo na kutengeneza silaha mwenyewe kama wazungu wanavyofanya kwa nchi zao

Woga wa wazungu uliwafanya watafute nchi itakayopigana na Iran kwa kuwa tu wanaogopa ipo siku ataishika Saudia
Na Saudia ni kibaraka wa wazungu huku akiwauzia mafuta na wao wakijenga nchi za GCC kwa kupata ukandarasi wote

Hapo wakamshawishi Iraq aingie vita ya bila kichwa wala miguu kwenye mto wa Shat Al Arab ambapo kwa bahati nilikuwa huko na kushuhudia vita zote mbili, hiyo ya 1980 na uvamizi tena wa Iraq huko Kuwait 1990

Iran wana wataalamu wengi sana wa masuala ya utengenezaji wa silaha na mengine mengi ila wanaogopwa sana eti kwa usalama wa ME lakini ukweli ni kuwa wanaemlinda ni Israel


Bora na sisi tuanze kununua silaha za Iran kama Rifles zao za Fajr
Wako vizuri kwa nyanja nyingi na wanatengeneza silaha nyingi sana za maangamizi ambapo kuna wengi humu watashangaa na hata kupinga kuwa jamaa yuko vizuri sana

List ya silaha anayotengeneza Iran ni ndefu sana yaani kama ningekuwa na uwezo wa kupata hata tenda ya kuanza na military uniforms tu halafu taratibu nikaanza kuuwauzia silaha hata bunduki 1000 tu kwa kuanzia

Kuna fursa duniani ila tumekazana za [emoji631] na [emoji636] tu huu ni utumwa na hautaisha
Tuna safari ndefu sana
 
Tukiuweka uislamu pembeni wairan ni waajemi na kama umesoma Biblia kwenye kitabu Cha Danieli Hawa Jamaa Tangu zamani ni watu Wenye akili nyingi (mf Mfalme Nebukadreza)ni Watu ambao maswala ya Sayansi na Teknolojia ilishakwepo kwao kabla hata ya kuja Kwa Yesu

Hivyo sizani hivo vikwazo uchwara vya watu magharibi kama vinaweza kukwamisha Maendeleo ya hao watu
 

Wewe ndie msomi unayeandika "ilani"... "hawana"...hehehehe makubwa haya

Lakini nakusahisha bwana Msomi mtoa mada hajasema 'ilani' iko top zaidi ya hizo nchi ulizotaja bali ameshangazwa na kugangamala kwake licha ya kuwekewa vikwazo kwa zaidi ya miaka 50 lakini hajatetereka ukilinganisha na Nchi zingine akatoa mfano wa Venezuela,

Kusoma ni kuelewa sio ukariri tu.
 
Jamaa wako vizuri sana na wanatengeneza silaha za kila aina tena hatari sana
Wataalamu wao wanalindwa haswa
Hizi baadhi tu ya silaha wanazotengeneza
 
Wewe nae unajitia mjuaji kumbe huna lolote,muwe mnasoma thd na kuzielewa kwanza kuliko kukurupuka tu kama chafya,ni wapi mleta mada amesema Iran ina nguvu kuliko mataifa mengine kama Marekani,China na Russia? mleta mada anasema licha ya Iran kuwekewa vikwazo kwa miaka kibao ila wapo vizuri kwenye kutengeneza silaha zao wao wenyewe,

Halafu na wewe eti unajiita ni msomi na kujiona ni bora zaidi kuliko mleta mada!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…