Iran ni nchi ya maajabu sana

Iran ni nchi ya maajabu sana

Tatizo wao ndio wanaojishtukia, lkn swala hili halihusiani na dini ya mtu.

Bali tunazungumzia uhalisia wa kweli dhidi ya propaganda za uongo walizoaminishwa watu huko zaman kabla ya kuja kuuona kweli.
Yeap wataleta hoja za udini
 
ni nchi ambayo iliweka misingi imala ya UONGOZI
Asikwambie mtu DEMOCRASIA inadumaza

ukitaka nchi yako ifanikiwe na ipige HATUA achana na DEMOCRASIA
DEMOCRASIA ni mtego mbaya wa WESTERN
ili kuendelea kukutawala na kukididimiza
CHINA ingekuwa imefuata huo upuuzi isingefika pele ilipo same na IRAN pia


hata ULAYA na AMERICA iliichukua mamia ya miaka mpk kuja kuwa na SERA ya DEMOCRASIA baada kuwa imejengeka na wamekuwa IMARA

Ndio maana hatahapa NCHINI kwetu tunahitaji RAISI mwenye kariba ya HAYATI MAGUFURI Ili kusonga mbele
DEMOCRASIA kwangu mimi ni ADUI mkubwa kwa MATAIFA yanayoendelea kama hapa NCHIN kwetu
Vipi kuhusu UGANDA, EQUATORIAL GUINEA, NA CENTRAL AFRICAN STATE vipi Hizi nchi zimeendelea Sana kuliko Tanzania?...
 
Unazungumzia Israel gani mkuu? Hii ambayo raia wake walifanywa watumwa na firauni kule Misri? Hii ambayo raia wake walitawaliwa na kuteswa na warumi? Hii ambayo raia wake walishindwa kujisimamia na kuamua kukimbilia ulaya hadi pale Hitler alipoamua kuwasambaratisha na kuwaangamiza? Unazungumzia Israel ambayo ni waingereza ndio waliwasaidia kuwatoa huko katika makambi ya ulaya na kuja kuwapachika hapo mashariki ya kati ambapo leo ndio wanapopigania na wapalestina? Au unazungumzia Israel hii inayopewa misaada ya fedha na ya kijeshi na Marekani?

Unafikiri Israel ikinyimwa tu misaada ya kifedha kwa muda wa miaka 5 tu na Marekan achilia mbali kuwekewa vikwazo itaweza ku savaivu?

Israel, Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na vibaraka wao Saudia wamejaribu kuidhibiti Iran kwa kila njia lkn imeshindikana. Jiulize kwanini nchi za magharibi hawakuziwekea vikwazo Saudia na washirika wake kama jinsi wameiwekea Iran? Jibu ni kwa sababu wamegundua wa Iran ndio taifa ambalo kama haukuliwekea vikwazo vya kiuchumi na silaha linaweza kutengeneza silaha mbaya na zenye nguvu zaidi kuliko nchi zote zilizopo mashariki ya kati ikiwemo hiyo Israel yako.

Waswahili wanakwambia mti wenye matunda mazuri ndio hupigwa mawe, nikimaanisha ukiona nchi karibuni zote za magharibi na washirika wake wakiwemo saudia na israel wameiwekea vikwazo vikubwa Iran jua nchi hiyo wanaiona ni hatari na tishio kwa mustakabali wa ulinzi wao na uchumi wao.
Umeizungumzia Israel kwa mwonekano bila kugusia misingi ya nchi ya Israel kuanzishwa kwake na uimara wake,sijafahamu Imani ya dini yako,lakini kama ni Mkristo basi soma Biblia kitabu cha Mwanzo na kutoka utafahamu mengi na hata haya uliyoyaandika,kufanywa utumwa,kutawanyika kwao Dunian,kukusanyika kwao na kuundwa kwa hili Taifa utayapata...kifupi Israel ndio wenye nguvu kuliko hayo mataifa ya Ulaya na Marekani uliyosema,Iran alisha tamka kulifuta hilo Taifa lakini hatakaa aweze.
Jiulize Israel anazungukwa na maadui kote lkn bado anatoboa unafikiri ni rahisi?hilo ni Taifa teule japo wengi hawapendi kusikia likiitwa teule,lakini ndio ukweli mchungu.

Hili Taifa limepitia misukosuko mingi sana,hiyo uliyaandika hapo ni michache mno,rudi kwenye Biblia kalisome hili Taifa ndipo utalifahamu vizuri,huwezi pigana na Israel ukashinda maana mkono wa Mungu uko na hilo Taifa,kwa wale Wakristo wanasoma Biblia wanafahamu ninachozungumzia,lkn kama hausomi Biblia huwezi elewa haya.
 
Wakuu vipi, kwema.

Wakuu Iran ni mmoja kati ya nchi ambazo ziliwekewa vikwazo vikali na nchi za magharibi toka mnamo mwa miaka ya 70s huko hadi leo hii na siku zijazo.

Vikwazo hivyo ni vya kiuchumi, kijeshi nk, tena vimekuwa vikiongezwa siku hadi siku.

Tofauti na ilivyo kwa nchi nyingine kama vile Cuba, Venezuela nk zilizowekewa vikwazo pengine na marekan tu, au baadhi ya nchi za magharibi. vikwazo vya Iran vimewekwa na nchi za magharibi kama zote wakishirikiana na makampuni ya nchi hizo.

Lakini cha kushangaza Iran imeweza kuwa na uwezo hasa wa kijeshi sawa au pengine zaidi ya ule wa nchi ambazo hazijawahi kuwekewa vikwazo na nchi hizo.

Iran ni miongoni mwa nchi zenye eneo kubwa na watu wengi barani Asia, so pamoja na vikwazo vya kiuchumi walivyowekewa takriban miaka 50 na zaidi, lkn wameweza kuwa na mifumo mizuri ya kudhibiti hali ya umasikini nchini mwao, tofauti na nchi kama Venezuela ambazo vikwazo vya miaka miwili au mitatu vimesababisha mamilioni ya raia waishi maisha ya shida na ya umasikini kupita maelezo.

Pamoja na vikwazo vikali vya magharibi hasa kwa upande wa mambo ya ulinzi, lkn bado nchi hiyo imeweza kuonesha kuwa haipo chini au nyuma kijeshi hata siku moja. Wengi tuliona jinsi wa Iran walivyoziangamiza ndege zisizo na ruban zilizokuwa zinatumiwa na Marekan kupima upepo katika eneo lao, wengi tuliona jinsi Iran ilivyozilipua meli ambazo zilikuwa zinabeba wapelelezi mbali mbali wa magharibi karibu na eneo lake, wengi tuliona jinsi Iran ilivyoshambulia kambi kadhaa za Marekani kule Iraq na kusababisha maafa na uharibifu mkubwa katika kambi hizo baada ya Mmarekani kumuuwa mmoja wa maofisa wakubwa wa Iran kule Iraq, tena kabla ya kufanya mashambulizi hayo wa Iran walitoa taarifa mapema kuwa watalipiza kisasi kupitia kambi za wamarekan kule Iraq, so marekan ikajiandaa kuzuia shambulizi lkn mwisho wa siku shambulizi likashindikana kuzuilika na kuleta maafa kwa jeshi la nchi hiyo kubwa duniani.

Wengi tulishuhudia jinsi Iran ilivyotoa msaada wa silaha kwa kundi la hezbullah ambalo liliichachafya Israel inayopata msaada mkubwa wa fedha kutoka Marekani kwa ajili ya ulinzi wao. Hiyo ilikuwa mwaka 2006 hadi jumuiya ya kimataifa ikaingilia kati na kuomba ipatekane suluhu ya kudumu baina ya Israeli na hezbullah.

Wengi tulishuhudia jinsi Iran ilivyosimama na kumlinda Asad wa Syria katika vita vyake, hadi kupelekea mipango ya Marekani na nchi za magharibi kumng'oa imeshindikana.

Wengi tunashuhudia sasa jinsi silaha kidogo tu za ndege zisikuwa na rubani za Iran zinavyofanya uharibifu mkubwa, na kusababisha maafa makubwa na zaidi ya yale yaliokuwa yanafanywa na Russia kupitia silaha zake mwenyewe (Russia) huko Ukraine.
Mpaka Marekani na nchi zingine za magharibi zinapiga kelele, maana silaha zinazotumika sio zile za Russia ambazo zilikuwa zinampa jeuri raisi wa Ukraine kuona kwamba sasa vita vimekwisha.

Hata zile himars za Marekani sasa hivi zinaonekana hazifanyi kazi mbele ya maangamizi ya ndege hizi za Iran.

Sasa tujiulize, kama nchi iliyowekewa vikwazo na mataifa makubwa duniani kwa zaidi ya miaka 50 bado ina uwezo iliyo nao leo, sasa je kama isingewekewa vikwazo kwa miaka yote hiyo 50 leo ni nchi gani ambayo ingeitisha pale Asia na hata duniani kwa ujumla.

Hizo nilizosema hapa ni zile silaha ilizotoa kuwawezesha hao niliwataja washinde mapambano yao, hapo hatujazungumzia silaha zake mwenyewe alizoweka kwa lengo la kujilinda ambazo kwa sheria za kijeshi duniani huwa zinafanywa siri kubwa ili adui asizione.

Mpaka sasa Marekani na nchi za magharibi zinashindwa kujua ni njia gani nyingine ya kumdhibiti huyu mtemi, maana wamarekani waliwahi kumtumia msaudi mwaka jana, hapo hapo Iran hakuchelewesha akaangamiza mitungi yake mikubwa ya kuwekea mafuta mpaka saudia na dunia ikapiga kelele.

Hili taifa ni la maajabu sana, japo lina maadui wengi lililotengenezewa na nchi za magharibi na halipati msaada wa kifedha kutoka kwa nchi yoyote lkn bado linajiamini kupita maelezo.

Mti wenye matunda ndio hurushiwa mawe, namaanisha ukiona nchi za magharibi na vibaraka wao wanapambana kwa hali na mali dhidi ya uchumi na ulinzi wa kijeshi wa nchi moja, basi jua kwamba wamagharibi hao wameshagundua kwamba nchi hiyo ni hatari maradufu kwa mustakabali wa uchumi wao pamoja na ulinzi wao.
Ukimpiga chura teke unampa mwendo zaidi,angalia Russian,North Korea,Irani,Hata akina China but matokeo ya kutumia akili zao wakijua maandui zao kamwe hawayataki maendeleo yao🏃🏃
 
Dunia hii na karne hii ya 21 bado unashikiwa akili na kudanganywa utafikiri bado upo katika karne ya 10 huko.
Wengi mnamezeshwa uongo na nyinyi bila kujitambua au kutafakari mnameza tu.
Ukweli ni kwamba Israel inafadhiliwa kijeshi na kifedha na serikali ya Marekani ikishirikiana na nchi zingine za magharibi. Obvious ni kweli kuna matajiri wa Israel na hata wasiokuwa Israel wanaifadhili Israel lkn, lkn serikali za nchi hizo nilizotaja hapo juu ndio wafadhili wakubwa wa Israel ndio maana utasikia serikali ya Marekani inaipa au imeipa Israel bilioni fulan kwa ajili ya kuimarisha shughuli zake za ulinzi na kiuchumi, vigumu kusikia taarifa ya habari ikisema matajiri kadhaa wa Marekani wameipa Israel bilion fulan kwa ajili ya shughuli fulan nk.

Sasa jiulize taifa teule kwanini litegemee misaada ya kifedha na kijeshi kutoka nje?
Kwanini ling'ang'anie kusema Iran iendelee kuwekewa vikwazo? Yenyewe si ina nguvu inaogopa nini sasa hadi ing'ang'anie mwenzake aendelee kuwekewa vikwazo?

Israel ni sawa sawa na bondia 'A' ambae anataka kupigana na bondia 'B' ambae ni Iran, afu Israel bondia
A anasema kwamba kabla ya pambano bondia 'B' afungwe kwanza mikono (awekewe vikwazo) afu ndo aingie mapambanoni.

Pamoja na kuachiwa atengeneze silaha, na msaada wa kijeshi juu kwa zaidi ya miaka 50 lkn bado anahofia Iran ikiwa huru inaweza kutengeneza silaha ambazo zitaleta maangamizi makubwa katika ardhi yake.

Israel pia ni kama CCM, yenyewe iko huru kufanya mikutano na kampeni mbali mbali ikisaidiwa na serikali (USA, UK, France nk) huku ikizuia wapinzani (Iran) wasifanye mikutano wala kampeni (vikwazo) afu kwenye uchaguzi wanategemea kusema eti wameshinda uchaguzi huo kwa njia ya haki kweli?

Kwanini wasiwaachie (waondoe vikwazo) na wapinzani (Iran) kufanya mikutano na kampeni zao kama ilivyo kwa CCM (Israel)
Afu sasa ndio waende kwenye mpambano wa uchaguzi (vita) kuona nani ni mshindi wa kweli?

Jinsi CCM inavyoogopa upinzani na kuuzuia usifanye mikutano yake, ndo jinsi Israel, Marekani, Saudia na nchi za magharibi zinavyoihofia Iran isiwe huru kutengeneza silaha zake na kuboresha uchumi wake.
Tatizo lako mkuu unajihisi uko smart na unajua vitu kuliko wengine,hilo ni tatizo kubwa mno....ukitaka kufahamu vitu vingi,soma na ukubali kujifunza kwa wengine,tambua wapo waliokutangulia wenye ufahamu wa mambo kukuzidi...bandiko lako unataka kutuaminisha ilani ina nguvu kuliko mataifa mengine,wanaweza kua na nguvu kwa sehemu flani,lkn hanawa huo uwezo kuzidi tunayoyaita Mataifa makubwa kama Marekani,China na Russia...kutengeneza hizo drones ambazo rada za mataifa mengine zinapata shida kuzisoma haina maana kwamba wao wako top...na kifupi soon watazigundua,huyo Muiran,Muisrael tu hapo hamuwezi ukatae ukubali huo ndio ukweli.
 
Nyuzi kama hizi huwa zinachekesha sana.....ukitazama unaweza kuzani wa Iran na Waisrael wanabishana kumbe ni wamatumbi wenzetu walioamua kuwa watumwa wa fikra za watu wengine.............

Na wote sources zao ni google na articles za mitandaoni...........hapa watu watatukanana na kudhalilishana Kwa mambo haya ya kipuuzi......lakini huwezi kukuta nchi zingine watu wanabishana na kutukanana kuhusu mambo ya nchi zingine.....
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23] Tatizo la wayahudi wa buza kila jambo linalohusu Iran au Palestina wao wanalichukulia kiimani ya dini, hata kama hakuna uhusian wowote kati ya dini na jambo husika.
Waambie mwamposa anawaita
Instead ya kuleta ujuha humu
 
Mwenye akili na mfuatiliaji kuhusu Iran anajua kwanini anachungwa sana na kuzuiwa kufanya mengi na hata vikwazo vingi kuwekewa

Iran ana wataalamu wengi sana na ni akili kubwa
Amejiwekeza kwenye maendeleo na kutengeneza silaha mwenyewe kama wazungu wanavyofanya kwa nchi zao

Woga wa wazungu uliwafanya watafute nchi itakayopigana na Iran kwa kuwa tu wanaogopa ipo siku ataishika Saudia
Na Saudia ni kibaraka wa wazungu huku akiwauzia mafuta na wao wakijenga nchi za GCC kwa kupata ukandarasi wote

Hapo wakamshawishi Iraq aingie vita ya bila kichwa wala miguu kwenye mto wa Shat Al Arab ambapo kwa bahati nilikuwa huko na kushuhudia vita zote mbili, hiyo ya 1980 na uvamizi tena wa Iraq huko Kuwait 1990

Iran wana wataalamu wengi sana wa masuala ya utengenezaji wa silaha na mengine mengi ila wanaogopwa sana eti kwa usalama wa ME lakini ukweli ni kuwa wanaemlinda ni Israel


Bora na sisi tuanze kununua silaha za Iran kama Rifles zao za Fajr
Wako vizuri kwa nyanja nyingi na wanatengeneza silaha nyingi sana za maangamizi ambapo kuna wengi humu watashangaa na hata kupinga kuwa jamaa yuko vizuri sana

List ya silaha anayotengeneza Iran ni ndefu sana yaani kama ningekuwa na uwezo wa kupata hata tenda ya kuanza na military uniforms tu halafu taratibu nikaanza kuuwauzia silaha hata bunduki 1000 tu kwa kuanzia

Kuna fursa duniani ila tumekazana za [emoji631] na [emoji636] tu huu ni utumwa na hautaisha
Tuna safari ndefu sana
 
Tukiuweka uislamu pembeni wairan ni waajemi na kama umesoma Biblia kwenye kitabu Cha Danieli Hawa Jamaa Tangu zamani ni watu Wenye akili nyingi (mf Mfalme Nebukadreza)ni Watu ambao maswala ya Sayansi na Teknolojia ilishakwepo kwao kabla hata ya kuja Kwa Yesu

Hivyo sizani hivo vikwazo uchwara vya watu magharibi kama vinaweza kukwamisha Maendeleo ya hao watu
 
Tatizo lako mkuu unajihisi uko smart na unajua vitu kuliko wengine,hilo ni tatizo kubwa mno....ukitaka kufahamu vitu vingi,soma na ukubali kujifunza kwa wengine,tambua wapo waliokutangulia wenye ufahamu wa mambo kukuzidi...bandiko lako unataka kutuaminisha ilani ina nguvu kuliko mataifa mengine,wanaweza kua na nguvu kwa sehemu flani,lkn hanawa huo uwezo kuzidi tunayoyaita Mataifa makubwa kama Marekani,China na Russia...kutengeneza hizo drones ambazo rada za mataifa mengine zinapata shida kuzisoma haina maana kwamba wao wako top...na kifupi soon watazigundua,huyo Muiran,Muisrael tu hapo hamuwezi ukatae ukubali huo ndio ukweli.

Wewe ndie msomi unayeandika "ilani"... "hawana"...hehehehe makubwa haya

Lakini nakusahisha bwana Msomi mtoa mada hajasema 'ilani' iko top zaidi ya hizo nchi ulizotaja bali ameshangazwa na kugangamala kwake licha ya kuwekewa vikwazo kwa zaidi ya miaka 50 lakini hajatetereka ukilinganisha na Nchi zingine akatoa mfano wa Venezuela,

Kusoma ni kuelewa sio ukariri tu.
 
Tukiuweka uislamu pembeni wairan ni waajemi na kama umesoma Biblia kwenye kitabu Cha Danieli Hawa Jamaa Tangu zamani ni watu Wenye akili nyingi (mf Mfalme Nebukadreza)ni Watu ambao maswala ya Sayansi na Teknolojia ilishakwepo kwao kabla hata ya kuja Kwa Yesu

Hivyo sizani hivo vikwazo uchwara vya watu magharibi kama vinaweza kukwamisha Maendeleo ya hao watu
Jamaa wako vizuri sana na wanatengeneza silaha za kila aina tena hatari sana
Wataalamu wao wanalindwa haswa
Hizi baadhi tu ya silaha wanazotengeneza
Screenshot_20221023-111713_Google.jpg
 
Tatizo lako mkuu unajihisi uko smart na unajua vitu kuliko wengine,hilo ni tatizo kubwa mno....ukitaka kufahamu vitu vingi,soma na ukubali kujifunza kwa wengine,tambua wapo waliokutangulia wenye ufahamu wa mambo kukuzidi...bandiko lako unataka kutuaminisha ilani ina nguvu kuliko mataifa mengine,wanaweza kua na nguvu kwa sehemu flani,lkn hanawa huo uwezo kuzidi tunayoyaita Mataifa makubwa kama Marekani,China na Russia...kutengeneza hizo drones ambazo rada za mataifa mengine zinapata shida kuzisoma haina maana kwamba wao wako top...na kifupi soon watazigundua,huyo Muiran,Muisrael tu hapo hamuwezi ukatae ukubali huo ndio ukweli.
Wewe nae unajitia mjuaji kumbe huna lolote,muwe mnasoma thd na kuzielewa kwanza kuliko kukurupuka tu kama chafya,ni wapi mleta mada amesema Iran ina nguvu kuliko mataifa mengine kama Marekani,China na Russia? mleta mada anasema licha ya Iran kuwekewa vikwazo kwa miaka kibao ila wapo vizuri kwenye kutengeneza silaha zao wao wenyewe,

Halafu na wewe eti unajiita ni msomi na kujiona ni bora zaidi kuliko mleta mada!
 
Back
Top Bottom