Iran ni nchi ya maajabu sana

Iran ni nchi ya maajabu sana

Dunia hii na karne hii ya 21 bado unashikiwa akili na kudanganywa utafikiri bado upo katika karne ya 10 huko.
Wengi mnamezeshwa uongo na nyinyi bila kujitambua au kutafakari mnameza tu.
Ukweli ni kwamba Israel inafadhiliwa kijeshi na kifedha na serikali ya Marekani ikishirikiana na nchi zingine za magharibi. Obvious ni kweli kuna matajiri wa Israel na hata wasiokuwa Israel wanaifadhili Israel lkn, lkn serikali za nchi hizo nilizotaja hapo juu ndio wafadhili wakubwa wa Israel ndio maana utasikia serikali ya Marekani inaipa au imeipa Israel bilioni fulan kwa ajili ya kuimarisha shughuli zake za ulinzi na kiuchumi, vigumu kusikia taarifa ya habari ikisema matajiri kadhaa wa Marekani wameipa Israel bilion fulan kwa ajili ya shughuli fulan nk.

Sasa jiulize taifa teule kwanini litegemee misaada ya kifedha na kijeshi kutoka nje?
Kwanini ling'ang'anie kusema Iran iendelee kuwekewa vikwazo? Yenyewe si ina nguvu inaogopa nini sasa hadi ing'ang'anie mwenzake aendelee kuwekewa vikwazo?

Israel ni sawa sawa na bondia 'A' ambae anataka kupigana na bondia 'B' ambae ni Iran, afu Israel bondia
A anasema kwamba kabla ya pambano bondia 'B' afungwe kwanza mikono (awekewe vikwazo) afu ndo aingie mapambanoni.

Pamoja na kuachiwa atengeneze silaha, na msaada wa kijeshi juu kwa zaidi ya miaka 50 lkn bado anahofia Iran ikiwa huru inaweza kutengeneza silaha ambazo zitaleta maangamizi makubwa katika ardhi yake.

Israel pia ni kama CCM, yenyewe iko huru kufanya mikutano na kampeni mbali mbali ikisaidiwa na serikali (USA, UK, France nk) huku ikizuia wapinzani (Iran) wasifanye mikutano wala kampeni (vikwazo) afu kwenye uchaguzi wanategemea kusema eti wameshinda uchaguzi huo kwa njia ya haki kweli?

Kwanini wasiwaachie (waondoe vikwazo) na wapinzani (Iran) kufanya mikutano na kampeni zao kama ilivyo kwa CCM (Israel)
Afu sasa ndio waende kwenye mpambano wa uchaguzi (vita) kuona nani ni mshindi wa kweli?

Jinsi CCM inavyoogopa upinzani na kuuzuia usifanye mikutano yake, ndo jinsi Israel, Marekani, Saudia na nchi za magharibi zinavyoihofia Iran isiwe huru kutengeneza silaha zake na kuboresha uchumi wake.
Unahangaika bure kumjibu. Mtu mwenyewe kuandika hajui.
 
ni nchi ambayo iliweka misingi imala ya UONGOZI
Asikwambie mtu DEMOCRASIA inadumaza

ukitaka nchi yako ifanikiwe na ipige HATUA achana na DEMOCRASIA
DEMOCRASIA ni mtego mbaya wa WESTERN
ili kuendelea kukutawala na kukididimiza
CHINA ingekuwa imefuata huo upuuzi isingefika pele ilipo same na IRAN pia


hata ULAYA na AMERICA iliichukua mamia ya miaka mpk kuja kuwa na SERA ya DEMOCRASIA baada kuwa imejengeka na wamekuwa IMARA

Ndio maana hatahapa NCHINI kwetu tunahitaji RAISI mwenye kariba ya HAYATI MAGUFURI Ili kusonga mbele
DEMOCRASIA kwangu mimi ni ADUI mkubwa kwa MATAIFA yanayoendelea kama hapa NCHIN kwetu
Umenena vema mkuu hata ikikitooea rais bora mwenye maono watataoa atawale miaka mitano ampishe mwingine asiye na uelekeo thats why waliumwa na vichwa waliposikia tetesi Magufuli anataka abaki madarakani....

Ni ukweli mchungu pia hata huu unaoitwa upinzani ni mbinu ya mabeberu kuleta mbambamba kwenye mataifa yetu thats why upinzani kwa afrika umefeuka kua fujo na mapambano dhidi ya serikali zinazotawala

Kikubwa ni kwamba wameya design haya iwa makusudi kabisa na wanajua kabisa kwamba mazingira yao s kama yakwetu wao nchi kwanza mambo mengine yatafuata

Sent from my M100 using JamiiForums mobile app
 
Kumbe Israel wanapewa fedha za kujilinda na America?😎 Kweli wachovu
Hilo liko wazi mkuu hata wayahudi wa buza wanalifahamu.

Bila huruma ya magharibi na msaada wa Marekani kamwe hawawezi kuwa na visalaha walivyonavyo.

Iran ni jeshi la mtu mmoja. Haihitaji msaada wa mtu yeyote kujijenga na kujisimamia, sana sana yenyewe ndio unatoa msaada wa kijeshi kwa nchi kama vile Rassia, Syria, hezbullah, wale waasi wa kule Yemen nk. Tena hapo ikiwa chini ya vikwazo vikali vya kiuchumi na kijeshi kwa zaidi ya miaka 50.
Je isingewekewa vikwazo hivyo vya kiuchumi na kijeshi miaka hiyo 50 iliyopita leo hii ingekuwa wapi?
 
Unafahamu kuwa Uamedi na uajemi walishawai kutawala dunia..??? kama unajua hilo jua ndo Iran ya sasa....
Shukran mkuu kwa kuweka ukumbusho huu, maana najua kuna wengi ambao hawalijui hilo na wachache wenye kujua huenda wangine wamesahau.
 
Wakuu vipi, kwema.

Wakuu Iran ni mmoja kati ya nchi ambazo ziliwekewa vikwazo vikali na nchi za magharibi toka mnamo mwa miaka ya 70s huko hadi leo hii na siku zijazo.

Vikwazo hivyo ni vya kiuchumi, kijeshi nk, tena vimekuwa vikiongezwa siku hadi siku.

Tofauti na ilivyo kwa nchi nyingine kama vile Cuba, Venezuela nk zilizowekewa vikwazo pengine na marekan tu, au baadhi ya nchi za magharibi. vikwazo vya Iran vimewekwa na nchi za magharibi kama zote wakishirikiana na makampuni ya nchi hizo.

Lakini cha kushangaza Iran imeweza kuwa na uwezo hasa wa kijeshi sawa au pengine zaidi ya ule wa nchi ambazo hazijawahi kuwekewa vikwazo na nchi hizo.

Iran ni miongoni mwa nchi zenye eneo kubwa na watu wengi barani Asia, so pamoja na vikwazo vya kiuchumi walivyowekewa takriban miaka 50 na zaidi, lkn wameweza kuwa na mifumo mizuri ya kudhibiti hali ya umasikini nchini mwao, tofauti na nchi kama Venezuela ambazo vikwazo vya miaka miwili au mitatu vimesababisha mamilioni ya raia waishi maisha ya shida na ya umasikini kupita maelezo.

Pamoja na vikwazo vikali vya magharibi hasa kwa upande wa mambo ya ulinzi, lkn bado nchi hiyo imeweza kuonesha kuwa haipo chini au nyuma kijeshi hata siku moja. Wengi tuliona jinsi wa Iran walivyoziangamiza ndege zisizo na ruban zilizokuwa zinatumiwa na Marekan kupima upepo katika eneo lao, wengi tuliona jinsi Iran ilivyozilipua meli ambazo zilikuwa zinabeba wapelelezi mbali mbali wa magharibi karibu na eneo lake, wengi tuliona jinsi Iran ilivyoshambulia kambi kadhaa za Marekani kule Iraq na kusababisha maafa na uharibifu mkubwa katika kambi hizo baada ya Mmarekani kumuuwa mmoja wa maofisa wakubwa wa Iran kule Iraq, tena kabla ya kufanya mashambulizi hayo wa Iran walitoa taarifa mapema kuwa watalipiza kisasi kupitia kambi za wamarekan kule Iraq, so marekan ikajiandaa kuzuia shambulizi lkn mwisho wa siku shambulizi likashindikana kuzuilika na kuleta maafa kwa jeshi la nchi hiyo kubwa duniani.

Wengi tulishuhudia jinsi Iran ilivyotoa msaada wa silaha kwa kundi la hezbullah ambalo liliichachafya Israel inayopata msaada mkubwa wa fedha kutoka Marekani kwa ajili ya ulinzi wao. Hiyo ilikuwa mwaka 2006 hadi jumuiya ya kimataifa ikaingilia kati na kuomba ipatekane suluhu ya kudumu baina ya Israeli na hezbullah.

Wengi tulishuhudia jinsi Iran ilivyosimama na kumlinda Asad wa Syria katika vita vyake, hadi kupelekea mipango ya Marekani na nchi za magharibi kumng'oa imeshindikana.

Wengi tunashuhudia sasa jinsi silaha kidogo tu za ndege zisikuwa na rubani za Iran zinavyofanya uharibifu mkubwa, na kusababisha maafa makubwa na zaidi ya yale yaliokuwa yanafanywa na Russia kupitia silaha zake mwenyewe (Russia) huko Ukraine.
Mpaka Marekani na nchi zingine za magharibi zinapiga kelele, maana silaha zinazotumika sio zile za Russia ambazo zilikuwa zinampa jeuri raisi wa Ukraine kuona kwamba sasa vita vimekwisha.

Hata zile himars za Marekani sasa hivi zinaonekana hazifanyi kazi mbele ya maangamizi ya ndege hizi za Iran.

Sasa tujiulize, kama nchi iliyowekewa vikwazo na mataifa makubwa duniani kwa zaidi ya miaka 50 bado ina uwezo iliyo nao leo, sasa je kama isingewekewa vikwazo kwa miaka yote hiyo 50 leo ni nchi gani ambayo ingeitisha pale Asia na hata duniani kwa ujumla.

Hizo nilizosema hapa ni zile silaha ilizotoa kuwawezesha hao niliwataja washinde mapambano yao, hapo hatujazungumzia silaha zake mwenyewe alizoweka kwa lengo la kujilinda ambazo kwa sheria za kijeshi duniani huwa zinafanywa siri kubwa ili adui asizione.

Mpaka sasa Marekani na nchi za magharibi zinashindwa kujua ni njia gani nyingine ya kumdhibiti huyu mtemi, maana wamarekani waliwahi kumtumia msaudi mwaka jana, hapo hapo Iran hakuchelewesha akaangamiza mitungi yake mikubwa ya kuwekea mafuta mpaka saudia na dunia ikapiga kelele.

Hili taifa ni la maajabu sana, japo lina maadui wengi lililotengenezewa na nchi za magharibi na halipati msaada wa kifedha kutoka kwa nchi yoyote lkn bado linajiamini kupita maelezo.

Mti wenye matunda ndio hurushiwa mawe, namaanisha ukiona nchi za magharibi na vibaraka wao wanapambana kwa hali na mali dhidi ya uchumi na ulinzi wa kijeshi wa nchi moja, basi jua kwamba wamagharibi hao wameshagundua kwamba nchi hiyo ni hatari maradufu kwa mustakabali wa uchumi wao pamoja na ulinzi wao.
Ebu niwe muungwana kidogo leo! Kongole kwa uchambuzi wako! ingawa uzi wako umejaa ushabiki na chumvi nyingi tofauti na uhalisia!! ingawa kwa upande mmoja umeeleza ukweli!!
Nianze na kuunga mkono!
-Ni kweli iran imeweza kustahimili vikwazo ingawa wananchi wake wanateseka na imepelekea kuwepo kwa biashara za magendo mipakani ambazo n dawa,vifaa,simu nk
-Iran ni taifa lenye watu wenye akili zaidi middle east kwa asili ni waajemi na si waarabu kama saudia,yemen ,oman au UAE

-Iran inauwezo mkubwa wa kijeshi licha ya vikwazo!! Lakini ni nchi ambayo hamna nchi ya kiarabu inaweza kushindana kijeshi hasa ukizingatia ni inatengeneza silaha zake yenyewe


UKOSOAJI!!
-Iran alikua mshirika mkubwa wa marekani zaidi hata ya saudia enzi za Iran monarch hivo ilikua inauziwa silaha nyingi kutoka marekani!!Nadhani ndo mwanzo wa kuwa imara kijeshi! kama unavoona sasa Saudia inauwezo mkubwa kijeshi kwa sababu ya ushirika wa kimkataba wa ulinzi wa US.Ni pale serikali ya kiislam ya irani ilipopindua serikali ya kifalme ya iran ndpo uhusiano na marekani ulipozorota na kuanza kwa vikwazo

-Drone za Iran si kwamba ndiyo ziko advanced zaidi ya drone zote hapana. wala si kwamba ni bora kuliko za Rusia hapana
Sababu pekee ambayo inafanya ziwe muhimu ni kutokana na
-Russia kushindwa kutengeneza drone nyingi kwa haraka ukilinganisha na mahitaji ya vita! ikumbukwe Russia imepoteza drone nyingi sana UKRAINE!
-Drone za Iran ni bei ndogo na zipo nyingi sana kiasi kwamba zinaendana na mahitaj ya vita

•Si kweli kwamba vikwazo vya marekani na washirika kwamba haviiumizi IRAN. Kuna kipindi vilitaka hata kuua Program ya nuclea!
wananchi wanaojarobu kuandamana wamekua waakikutana na mkono wa chuma
 
Ni hawa hawa Iran wenye uwezo wa kuifuta Isreal kwenye uso wa dunia kwa maneno ya mdomoni, usifanye mchezo na taifa la kiyahudi, level yao ni juu mara mia zaidi ya binadamu mwingine yoyote anayeishi duniani....Israel is blessed.
Umekaririshwa ndugu yangu
Inabidi ufanye utafiti kabla huja ongea huu upotoshaji. Sikatai kusema israel was blessed but not this Israel ya sasa. Tuanzia hapo.
Pili, umewafuatilia Iran kwenye historia vizuri? Hawa majamaa wana uwezo wa kuimaliza Israel kwenye sayari ya dunia vizuri tu.

We unajua kwanini marekani inaendelea kuwawekea vikwazo Iran, sababu ni ugomvi wake wa asili na Israel. We imagine Iran hana vikwazo vyovyote alafu aende one on one na Israel unadhani atakufa nani?

Katika historia hawa wa Persian/waajemi sio waarabu ni taifa lililo barikiwa lina kila utajiri unao udhani wewe. Alafu they are blessed kuwa taifa la kwanza dunia kustaarabika(civilized) na wajenzi. Wazungu wamejifunza kupitia hawa majamaa. Kitu usicho jua ni kwamba hata wairan wana akili vile vile kama hao wayahudi unao wasifia.

Kitu kibaya kwao ambacho watu wengi hawakijui ni dini yao ya uislam imefitishwa. Lakini ni taifa lenye nguvu
 
Hawa vijana wamemezeshwa uongo wa kizamani sana, afu cha kushangaza mpaka zaman hizi za sayansi na teknolojia wameshindwa kuutambua uongo huo.

Inashangaza sana.
Uongo wa jua kuzama kwenye tope sio?
 
Hilo liko wazi mkuu hata wayahudi wa buza wanalifahamu.

Bila huruma ya magharibi na msaada wa Marekani kamwe hawawezi kuwa na visalaha walivyonavyo.

Iran ni jeshi la mtu mmoja. Haihitaji msaada wa mtu yeyote kujijenga na kujisimamia, sana sana yenyewe ndio unatoa msaada wa kijeshi kwa nchi kama vile Rassia, Syria, hezbullah, wale waasi wa kule Yemen nk. Tena hapo ikiwa chini ya vikwazo vikali vya kiuchumi na kijeshi kwa zaidi ya miaka 50.
Je isingewekewa vikwazo hivyo vya kiuchumi na kijeshi miaka hiyo 50 iliyopita leo hii ingekuwa wapi?
Hana hiyo jeuri anapewa teknolojia na urusi mbona liko wazi hili.
 
Umekaririshwa ndugu yangu
Inabidi ufanye utafiti kabla huja ongea huu upotoshaji. Sikatai kusema israel was blessed but not this Israel ya sasa. Tuanzia hapo.
Pili, umewafuatilia Iran kwenye historia vizuri? Hawa majamaa wana uwezo wa kuimaliza Israel kwenye sayari ya dunia vizuri tu.

We unajua kwanini marekani inaendelea kuwawekea vikwazo Iran, sababu ni ugomvi wake wa asili na Israel. We imagine Iran hana vikwazo vyovyote alafu aende one on one na Israel unadhani atakufa nani?

Katika historia hawa wa Persian/waajemi sio waarabu ni taifa lililo barikiwa lina kila utajiri unao udhani wewe. Alafu they are blessed kuwa taifa la kwanza dunia kustaarabika(civilized) na wajenzi. Wazungu wamejifunza kupitia hawa majamaa. Kitu usicho jua ni kwamba hata wairan wana akili vile vile kama hao wayahudi unao wasifia.

Kitu kibaya kwao ambacho watu wengi hawakijui ni dini yao ya uislam imefitishwa. Lakini ni taifa lenye nguvu
Waende wakajaribu, wasiishie kuongea maneno ya kwenye kanga, unajua historia ya vita ya mwaka 1967 Isreal alivyowakalisha waarabu wakati huo Ariel Sharon akiwa general aliyeongoza vita.......fuatilia historia, Isreal wakishindwa vita ni kwa kuwa Mungu kawapa adhabu na si vinginevyo.​
 
Unazungumzia Israel gani mkuu? Hii ambayo raia wake walifanywa watumwa na firauni kule Misri? Hii ambayo raia wake walitawaliwa na kuteswa na warumi? Hii ambayo raia wake walishindwa kujisimamia na kuamua kukimbilia ulaya hadi pale Hitler alipoamua kuwasambaratisha na kuwaangamiza? Unazungumzia Israel ambayo ni waingereza ndio waliwasaidia kuwatoa huko katika makambi ya ulaya na kuja kuwapachika hapo mashariki ya kati ambapo leo ndio wanapopigania na wapalestina? Au unazungumzia Israel hii inayopewa misaada ya fedha na ya kijeshi na Marekani?

Unafikiri Israel ikinyimwa tu misaada ya kifedha kwa muda wa miaka 5 tu na Marekan achilia mbali kuwekewa vikwazo itaweza ku savaivu?

Israel, Marekani, Uingereza, Ujerumani, Ufaransa na vibaraka wao Saudia wamejaribu kuidhibiti Iran kwa kila njia lkn imeshindikana. Jiulize kwanini nchi za magharibi hawakuziwekea vikwazo Saudia na washirika wake kama jinsi wameiwekea Iran? Jibu ni kwa sababu wamegundua wa Iran ndio taifa ambalo kama haukuliwekea vikwazo vya kiuchumi na silaha linaweza kutengeneza silaha mbaya na zenye nguvu zaidi kuliko nchi zote zilizopo mashariki ya kati ikiwemo hiyo Israel yako.

Waswahili wanakwambia mti wenye matunda mazuri ndio hupigwa mawe, nikimaanisha ukiona nchi karibuni zote za magharibi na washirika wake wakiwemo saudia na israel wameiwekea vikwazo vikubwa Iran jua nchi hiyo wanaiona ni hatari na tishio kwa mustakabali wa ulinzi wao na uchumi wao.
Unafikiri kwa nini wazungu na hasa marekani wanawakumbatia Isreal, ni kwamba innovations zote zile pasua kichwa kwenye nyanja zote ikiwemo teknolojia za kijeshi zinafanywa na waisrali wanaoishi huko. Hata hiyo iron dome system inayowalinda dhidi ya makombora ya wapalestina ni akili zao wenyewe. Isreal ameweza kuishi jangwani na kuzalisha bidhaa za kilimo bora zaidi ambazo anauza hadi ulaya, jambo ambalo mwarabu hana hiyo akili . Ndugu, yangu elewa hao watu wako privilaged kuliko binadamu wengine upstairs. Fuatilia historia, Israel walikuiwa wanashindwa vita au kupelekwa utumwani kama adhabu kutoka kwa Mungu mwenyewe, kinyume chake huwezi kusimama kupambana nao ukashinda.​
 
Umeizungumzia Israel kwa mwonekano bila kugusia misingi ya nchi ya Israel kuanzishwa kwake na uimara wake,sijafahamu Imani ya dini yako,lakini kama ni Mkristo basi soma Biblia kitabu cha Mwanzo na kutoka utafahamu mengi na hata haya uliyoyaandika,kufanywa utumwa,kutawanyika kwao Dunian,kukusanyika kwao na kuundwa kwa hili Taifa utayapata...kifupi Israel ndio wenye nguvu kuliko hayo mataifa ya Ulaya na Marekani uliyosema,Iran alisha tamka kulifuta hilo Taifa lakini hatakaa aweze.
Jiulize Israel anazungukwa na maadui kote lkn bado anatoboa unafikiri ni rahisi?hilo ni Taifa teule japo wengi hawapendi kusikia likiitwa teule,lakini ndio ukweli mchungu.

Hili Taifa limepitia misukosuko mingi sana,hiyo uliyaandika hapo ni michache mno,rudi kwenye Biblia kalisome hili Taifa ndipo utalifahamu vizuri,huwezi pigana na Israel ukashinda maana mkono wa Mungu uko na hilo Taifa,kwa wale Wakristo wanasoma Biblia wanafahamu ninachozungumzia,lkn kama hausomi Biblia huwezi elewa haya.
Hao ni wale wa upande ule, wanajaribu kubishana na facts.....wanasema Isreal anasaidiwa na wazungu wakati kimsingi wazungu ndo wanamtegemea Isreli kwenye mambo yote yanayohitaji akili kubwa ikiwemo teknolojia za kijeshi, kiufupi Isreali anajilinda mwenyewe kwa kipawa chake cha akili, haijalishi anafanya hivyo kutokea ulaya au marekani.​
 
Tatizo lako mkuu unajihisi uko smart na unajua vitu kuliko wengine,hilo ni tatizo kubwa mno....ukitaka kufahamu vitu vingi,soma na ukubali kujifunza kwa wengine,tambua wapo waliokutangulia wenye ufahamu wa mambo kukuzidi...bandiko lako unataka kutuaminisha ilani ina nguvu kuliko mataifa mengine,wanaweza kua na nguvu kwa sehemu flani,lkn hanawa huo uwezo kuzidi tunayoyaita Mataifa makubwa kama Marekani,China na Russia...kutengeneza hizo drones ambazo rada za mataifa mengine zinapata shida kuzisoma haina maana kwamba wao wako top...na kifupi soon watazigundua,huyo Muiran,Muisrael tu hapo hamuwezi ukatae ukubali huo ndio ukweli.
Nasema hivi hayo mataifa mengine yana nguvu kwa sababu hayajawekewa, wala kujiwekea vikwazo vya kutengeneza silaha, na pia hayana vikwazo vya kiuchumi nk, ndio maana leo hii wewe unawaona wana nguvu kuliko wengine.

Laiti kama Iran isingewekewa vikwazo vya silaha na kiuchumi kwahiyo miaka 50, nakuhakikishia kuwa leo hii usingekuwa unaongea haya unayoongea hapa.

Sababu ya kuiwekea vikwazo ni kwa sababu wameiona hiyo nchi ikiwa huru unaweza kutengeneza silaha zenye hatari kubwa kwao na vibaraka wao kama vile Saudia, Israel nk.

Ndo maana nikakupa mfano kuwa Iran ni sawa sawa na bondia aliefungwa mikono, lkn bado anaonekana tishia kwa yule ambae hakufungwa mikono (Israel) pamoj na kwamb ana support kubwa kutoka kwa waandaji wa pambano (USA, UK, EU nk)

Swali ni kwanini Israel inahofia Iran isiwe huru kutengeneza silaha kama ilivyo kwa yenyewe, Marekani, Ulaya nk.

Mbona hatujasikia Iran ikilalamika kuwa Israel iwekewe vikwazo vya kiuchumi na kijeshi.

Pia kumbuka nlikupa mfano wa CCM na upinzani kufanya mikutano na kampeni mbali mbali. Ukiuelewa vizuri mfano ule basi hautakuwa na shaka juu ya nilichokiandika.
 
ni nchi ambayo iliweka misingi imala ya UONGOZI
Asikwambie mtu DEMOCRASIA inadumaza

ukitaka nchi yako ifanikiwe na ipige HATUA achana na DEMOCRASIA
DEMOCRASIA ni mtego mbaya wa WESTERN
ili kuendelea kukutawala na kukididimiza
CHINA ingekuwa imefuata huo upuuzi isingefika pele ilipo same na IRAN pia


hata ULAYA na AMERICA iliichukua mamia ya miaka mpk kuja kuwa na SERA ya DEMOCRASIA baada kuwa imejengeka na wamekuwa IMARA

Ndio maana hatahapa NCHINI kwetu tunahitaji RAISI mwenye kariba ya HAYATI MAGUFURI Ili kusonga mbele
DEMOCRASIA kwangu mimi ni ADUI mkubwa kwa MATAIFA yanayoendelea kama hapa NCHIN kwetu
wala hivo sio hoja,eti demokrasi inabkwamisha maendeleo,nchi ngapi duniani zina udikteta wa kupitilizaza lakini ni masikini za kutupwa,nenda latini America huko,Huyo Jiwe na udikteta uchwara wake kuna nini cha kujivunia alichokiacha?
iran licha ya vikwazo vikali bado anauza gesi yake kwa iraq na uturuki,na maisha ya wananchi wake ni magumu,sana,sema ndio huo utemi ni ngumu kuyajua.
 
Back
Top Bottom