Iran ni nchi ya maajabu sana

Iran ni nchi ya maajabu sana

Mwenye akili kubwa anajitegemea siyo kumtegemea mtu. Israel inasavaivu kwa msaada wa Marekani na washirika wao. Kwanini hawajitegemei?
Asante kwa swali zuri ulilomuuliza jamaa. Sina uhakika kama atajibu kama inavyotakiwa.
 
Jibu ni moja Wana akili za uvumbuzi kama tuu Koreans zote..

Hiki ni kipawa kama vipawa vingine..

Na bado wanatoa misaada na kukopesha Nchi zingine ikiwemo Tanzania [emoji116]

Duh! Kwa hiyo maafisa wetu walikwenda Hispania wakapewa mkopo wa milioni 44 tu! Hii pesa si hata wasanii wa bongo fleva wakijichanga chini ya Steve Nyerere wanaipa nchi.

Samahani wakuu, niko nje ya mada.
 
Waende wakajaribu, wasiishie kuongea maneno ya kwenye kanga, unajua historia ya vita ya mwaka 1967 Isreal alivyowakalisha waarabu wakati huo Ariel Sharon akiwa general aliyeongoza vita.......fuatilia historia, Isreal wakishindwa vita ni kwa kuwa Mungu kawapa adhabu na si vinginevyo.​
Kitu unacho kosea mpaka leo ni kimoja tu
Taifa la Israel lilikuwa ni taifa teule kipindi hicho cha Mussa lakini sio sasa.

Walicho bakia nacho au barikiwa ni akili tu.

Taifa gani teule linauwa watu, lina ubaguzi alafu istoshe haliabudu mnacho kiabudu.
 
Kama siyo taifa teule, tupe maandiko ambayo yanaonyesha Mungu kujitwalia taifa tofauti liwe taifa teule badala ya Israel. Usichokijua ni kwamba hatma ya taifa la Israel imeandikwa hadi kiama, hata hukumu yao ni tofauti na watu wa mataifa. Wao hadi idadi yao watakaoingia mbinguni kutoka kila kabila imetajwa..........na hata mji wa Yerusalemu mpya utakuwa na malango kumi na mbili kwa ajili ya makabila kumi na mbili ya Israel. Kwa hiyo watu wa mataifa mengine kutaka kujilinganisha na Israel kisa wamekuwa wakiadhibiwa na Mungu ni sawa na mtu kuingilia ugomvi usiomhusu.​
 
😂😂😂😂 unachekesha sana mkuu.

Yani waisarel waende wakafanye mambo hayo huko ulaya na marekani, huku nchi yao wenyewe ikiwa inahitaji msaada wa kiuchumi na kijeshi kutoka katika hizo nchi ulizotaja?
Hakika unachekesha na kushangaza sana aisee.
Wanatumia akili yao kuendesha mambo duniani na kuamua hatma ya dunia, hicho ndo walichojaliwa ndo maana ni taifa teule. Innovations zote zinazohitaji akili kubwa zinazofanyika marekani, ulaya na hata russia ni wao. Usichokijua ni kwamba watu wenye asili ya kiyahudi wametapakaa kote marekani, ulaya na nchi zote za iliyokuwa shirikisho la Urusi.
 
Tatizo lenu nyinyi mmeng'ang'ania kuamini mambo yalioandikwa kwenye vitabu na sio yale mnayoyaona au kuyatafakari wenyewe.

1) Wa Israel wangekuwa na akili unayosema wasingefanywa watumwa huko Misri (Afrika)

2) Wa Israel wangekuwa na akili wasingeruhusu warumi waingie katika nchi yao na kufanya waliyoyafanya. Kumbuka warumi asili yao ni ulaya. Sasa kama unaamini nchi za ulaya zinaitegemea Israel ilikuje anaetegemewa (Israel) atawaliwe na anaemtegemea (mzungu) hii inaingia akilini kweli?

Wa israel wangekuwa na akili unayosema wasingeangamizwa na Hitler Mzungu tena ni miaka 50 au 70 tu iliyopita, wakati wazungu wameanza kuitawala dunia au sehem kubwa ya dunia miaka zaidi ya elfu iliyopita.

SWALI LA MWISHO:

Kama Israel inategemewa na wazungu inakuaje nchi za wazungu ndio zenye nguvu za kijeshi, uchumi mkubwa na maendeleo ya kiteknolojia zaidi ya Israel yenyewe?

Yan nchi yenye wataalam bado inategemea msaada wa kifedha na kijeshi kutoka kwa wale inaowasaidia, hii inaingia akilini kweli?

Sawa vitabu vya dini tusome lkn na akili zetu pia tuzitumie kufanya tasmini ili kujua ukweli wa mambo.

Israel ingekuwa na sifa hizo unazozisema hapa. Basi leo ndio ingekuwa nchi ya kwanza kiuchumi, kijeshi na kiteknolojia, ila kwa vile hawana sifa hizo mlizomezeshwa ndo maana leo iko nyuma hata ya China.

Acheni kuweka mambo ya dini kwenye mambo muhimu.
Mara zote Isreal akichukuliwa mateka au kupelekwa utumwani huwa ni adhabu toka kwa Mungu mwenyewe, mataifa mengine ambayo yalikuwa yakifanya uovu Mungu alitumia taifa la Israel kuyafuta kabisa, maana alilichagua taifa la Israel ili ajitukuze miongoni mwa mataifa.
 
Haya ni mambo uliyoyasoma tu kwenye vitabu na wew ukakariri, sio yalio kwenye uhalisia.
Nchi inayotegemewa duniani haiko hata kwenye nchi 10 zenye uchumi mkubwa duniani.
Nchi inayotegemewa duniani haiko hata kwenye 5 bora ya nchi zenye nguvu kijeshi.
So what kind of joke are you try to joke here bro?
Nyanja zote za technolojia zinazohitaji akili kubwa ni wao, either wako marekani, ulaya au urusi. Usichokijua waisrael wametapakaa kote marekani, ulaya hadi urusi.
 
Kama siyo taifa teule, tupe maandiko ambayo yanaonyesha Mungu kujitwalia taifa tofauti liwe taifa teule badala ya Israel. Usichokijua ni kwamba hatma ya taifa la Israel imeandikwa hadi kiama, hata hukumu yao ni tofauti na watu wa mataifa. Wao hadi idadi yao watakaoingia mbinguni kutoka kila kabila imetajwa..........na hata mji wa Yerusalemu mpya utakuwa na malango kumi na mbili kwa ajili ya makabila kumi na mbili ya Israel. Kwa hiyo watu wa mataifa mengine kutaka kujilinganisha na Israel kisa wamekuwa wakiadhibiwa na Mungu ni sawa na mtu kuingilia ugomvi usiomhusu.​
Ila sio sasa japo historia inasema kwenye maandiko ya Dini.
 
Kitu watu wengi wana changanya ni kuwa hizi nchi zimezungukana na zipo karibu karibu. Asili yao ni moja.
Ukifuatilia hata mitume wamezaliwa katika hayo mataifa japo wengi ni wayahudi.

Vita ya Palestinian na Israel inaendelea hadi leo ni sababu hizi hizi tunazo bishana
 
Wakuu vipi, kwema.

Wakuu Iran ni mmoja kati ya nchi ambazo ziliwekewa vikwazo vikali na nchi za magharibi toka mnamo mwa miaka ya 70s huko hadi leo hii na siku zijazo.

Vikwazo hivyo ni vya kiuchumi, kijeshi nk, tena vimekuwa vikiongezwa siku hadi siku.

Tofauti na ilivyo kwa nchi nyingine kama vile Cuba, Venezuela nk zilizowekewa vikwazo pengine na marekan tu, au baadhi ya nchi za magharibi. vikwazo vya Iran vimewekwa na nchi za magharibi kama zote wakishirikiana na makampuni ya nchi hizo.

Lakini cha kushangaza Iran imeweza kuwa na uwezo hasa wa kijeshi sawa au pengine zaidi ya ule wa nchi ambazo hazijawahi kuwekewa vikwazo na nchi hizo.

Iran ni miongoni mwa nchi zenye eneo kubwa na watu wengi barani Asia, so pamoja na vikwazo vya kiuchumi walivyowekewa takriban miaka 50 na zaidi, lkn wameweza kuwa na mifumo mizuri ya kudhibiti hali ya umasikini nchini mwao, tofauti na nchi kama Venezuela ambazo vikwazo vya miaka miwili au mitatu vimesababisha mamilioni ya raia waishi maisha ya shida na ya umasikini kupita maelezo.

Pamoja na vikwazo vikali vya magharibi hasa kwa upande wa mambo ya ulinzi, lkn bado nchi hiyo imeweza kuonesha kuwa haipo chini au nyuma kijeshi hata siku moja. Wengi tuliona jinsi wa Iran walivyoziangamiza ndege zisizo na ruban zilizokuwa zinatumiwa na Marekan kupima upepo katika eneo lao, wengi tuliona jinsi Iran ilivyozilipua meli ambazo zilikuwa zinabeba wapelelezi mbali mbali wa magharibi karibu na eneo lake, wengi tuliona jinsi Iran ilivyoshambulia kambi kadhaa za Marekani kule Iraq na kusababisha maafa na uharibifu mkubwa katika kambi hizo baada ya Mmarekani kumuuwa mmoja wa maofisa wakubwa wa Iran kule Iraq, tena kabla ya kufanya mashambulizi hayo wa Iran walitoa taarifa mapema kuwa watalipiza kisasi kupitia kambi za wamarekan kule Iraq, so marekan ikajiandaa kuzuia shambulizi lkn mwisho wa siku shambulizi likashindikana kuzuilika na kuleta maafa kwa jeshi la nchi hiyo kubwa duniani.

Wengi tulishuhudia jinsi Iran ilivyotoa msaada wa silaha kwa kundi la hezbullah ambalo liliichachafya Israel inayopata msaada mkubwa wa fedha kutoka Marekani kwa ajili ya ulinzi wao. Hiyo ilikuwa mwaka 2006 hadi jumuiya ya kimataifa ikaingilia kati na kuomba ipatekane suluhu ya kudumu baina ya Israeli na hezbullah.

Wengi tulishuhudia jinsi Iran ilivyosimama na kumlinda Asad wa Syria katika vita vyake, hadi kupelekea mipango ya Marekani na nchi za magharibi kumng'oa imeshindikana.

Wengi tunashuhudia sasa jinsi silaha kidogo tu za ndege zisikuwa na rubani za Iran zinavyofanya uharibifu mkubwa, na kusababisha maafa makubwa na zaidi ya yale yaliokuwa yanafanywa na Russia kupitia silaha zake mwenyewe (Russia) huko Ukraine.
Mpaka Marekani na nchi zingine za magharibi zinapiga kelele, maana silaha zinazotumika sio zile za Russia ambazo zilikuwa zinampa jeuri raisi wa Ukraine kuona kwamba sasa vita vimekwisha.

Hata zile himars za Marekani sasa hivi zinaonekana hazifanyi kazi mbele ya maangamizi ya ndege hizi za Iran.

Sasa tujiulize, kama nchi iliyowekewa vikwazo na mataifa makubwa duniani kwa zaidi ya miaka 50 bado ina uwezo iliyo nao leo, sasa je kama isingewekewa vikwazo kwa miaka yote hiyo 50 leo ni nchi gani ambayo ingeitisha pale Asia na hata duniani kwa ujumla.

Hizo nilizosema hapa ni zile silaha ilizotoa kuwawezesha hao niliwataja washinde mapambano yao, hapo hatujazungumzia silaha zake mwenyewe alizoweka kwa lengo la kujilinda ambazo kwa sheria za kijeshi duniani huwa zinafanywa siri kubwa ili adui asizione.

Mpaka sasa Marekani na nchi za magharibi zinashindwa kujua ni njia gani nyingine ya kumdhibiti huyu mtemi, maana wamarekani waliwahi kumtumia msaudi mwaka jana, hapo hapo Iran hakuchelewesha akaangamiza mitungi yake mikubwa ya kuwekea mafuta mpaka saudia na dunia ikapiga kelele.

Hili taifa ni la maajabu sana, japo lina maadui wengi lililotengenezewa na nchi za magharibi na halipati msaada wa kifedha kutoka kwa nchi yoyote lkn bado linajiamini kupita maelezo.

Mti wenye matunda ndio hurushiwa mawe, namaanisha ukiona nchi za magharibi na vibaraka wao wanapambana kwa hali na mali dhidi ya uchumi na ulinzi wa kijeshi wa nchi moja, basi jua kwamba wamagharibi hao wameshagundua kwamba nchi hiyo ni hatari maradufu kwa mustakabali wa uchumi wao pamoja na ulinzi wao.
He country.
 
Wanatumia akili yao kuendesha mambo duniani na kuamua hatma ya dunia, hicho ndo walichojaliwa ndo maana ni taifa teule. Innovations zote zinazohitaji akili kubwa zinazofanyika marekani, ulaya na hata russia ni wao. Usichokijua ni kwamba watu wenye asili ya kiyahudi wametapakaa kote marekani, ulaya na nchi zote za iliyokuwa shirikisho la Urusi.
Nchi yenye kuendesha mambo na kuamua hatma ya dunia, inashindwaje kuendesha mambo yake yenyewe kiuchumi na kijeshi mpaka itegemee mataifa mengine?

Laiti kama hayo unayosema yangekuwa ya kweli basi nchi zote ambazo ziko mbele kiuchumi na kijeshi zaidi ya Israel leo hii ndio zingekuwa zinaenda kuomba msaada wa kifedha na kiulinzi, lkn tunachokiona sasa ni tofauti na kile kilichoandikwa kwenye vitabu. Taifa teule ndio linategemea huruma ya kifedha kwa ajili ya uchumi na ulinzi wake kutoka katika mataifa ambayo sio teule.
a) Israel yenye waisrael watupu leo hii haipo hata katika nchi 10 zenye jeshi lenye nguvu na vifaa bora duniani.
b) Israel yenye waisrael watupu leo hii haipo hata katika nchi 10 zenye uchumi bora duniani.

Afu uniambie watu ambao wameshindwa kuifanya nchi yao wenyewe kuwa yenye nguvu na uchumi mkubwa duniani zaidi ya Marekani, China, Ujerumani, Uingereza nk ndio wanategemewa kusimamia hatma ya dunia.

Na cha kushangaza taifa teule linaogopa jiran yake asiwe na uhuru wa kutengeneza silaha zake na kuimarisha uchumi wake 😂😂😂, sasa hapo huo uwezo na uteule wake uko wapi?

Yani hapo ni sawasawa na kusema kuwa mimi nina nguvu za kupiga mtaa mzima (israel), lkn hapo hapo naenda kuwaita watu wa mtaa mungine waje wakuzuie wewe usiwe na uwezo wa kutoka nje kutafuta chakula au kufanya mazoezi ya kujilinda (Iran)

Sasa hapo kwa wenye akili wataona mimi nina nguvu kweli? Maana watajiuliza kama nina nguvu na kujiamini ni kwanini niogope wewe usiwe unatoka nje kufanya mazoezi ya kujilinda? Ni nini kiko nyuma ya pazia?

Sometimes waafrika tukiamini kila kilichoandikwa katika vitabu vya dini tunakuwa tunajilemaza sisi wenyew kiakili, maana hata jambo ambalo halina uhalisia kama hili la Israel tutaendelea kuliamini huku tunaowaamini wenyewe wakiwa hawana uwezo huo tunaowaamini nao.
Ndio maana wenzetu wachina wamejiepusha na kuamini kila kilichoandikwa kwenye vitabu vya dini na leo hii wameweza kuwa mbali ki teknolojia, uchumi, jeshi nk.

Sisi waafrika tumeshindwa kujisimamia kama China tukiamini kuwa uwezo huo kapewa mu Israel peke yake kupitia vitabu 😂😂😂😂

Huyu raisi wa China aliongea kweli, japo siku zote ukweli ni mchungu kwa yule ambae hakutaka kuusikia ukweli huo. Ebu msome afu upime na kile unachong'ang'ania kukisema kupitia vitabu vya dini.
 
Attachments

  • Screenshot_20221024-214325.jpg
    Screenshot_20221024-214325.jpg
    68.1 KB · Views: 6

Hizo innovations za kijeshi ni akili zao wenyewe, kwa hiyo kimsingi wanatumia akili zao kujilinda.....ndo maana aliwakalisha waarabu mwaka 1967 na kuteka maeneo yao kadhaa ambayo hadi leo hawana ubavu wa kuyarudisha.​
 
Mara zote Isreal akichukuliwa mateka au kupelekwa utumwani huwa ni adhabu toka kwa Mungu mwenyewe, mataifa mengine ambayo yalikuwa yakifanya uovu Mungu alitumia taifa la Israel kuyafuta kabisa, maana alilichagua taifa la Israel ili ajitukuze miongoni mwa mataifa.
Wafrika bado tuna safari ndefu ya kujikomboa 😂😂😂😂😂😂😂

Kama alivyosema raisi wa nchi kwamba inafika kipindi sisi waafrika ndio tunajifanya tunazijua dini kuliko wale waliotuletea dini hizo.

Ukute hayo unayosema wewe myahudi wa buza kuhusu kitabu unachoamini wew, wayahudi wenyew waliopo ndani ya Israel yenyew wala hawakiamini. Haya banah
 
Attachments

  • Screenshot_20221024-214325.jpg
    Screenshot_20221024-214325.jpg
    68.1 KB · Views: 5
Wafrika bado tuna safari ndefu ya kujikomboa 😂😂😂😂😂😂😂

Kama alivyosema raisi wa nchi kwamba inafika kipindi sisi waafrika ndio tunajifanya tunazijua dini kuliko wale waliotuletea dini hizo.

Ukute hayo unayosema wewe myahudi wa buza kuhusu kitabu unachoamini wew, wayahudi wenyew waliopo ndani ya Israel yenyew wala hawakiamini. Haya banah
Ni kama wewe unavyoamini kile kitabu cha mnyaazi, hahaah...
 
Hizo innovations za kijeshi ni akili zao wenyewe, kwa hiyo kimsingi wanatumia akili zao kujilinda.....ndo maana aliwakalisha waarabu mwaka 1967 na kuteka maeneo yao kadhaa ambayo hadi leo hawana ubavu wa kuyarudisha.​
Ushasema aliwakalisha waarabu. Hapa hoja ni Iran ambao ni waajemi na sio waarabu.
Bila shaka wew haujui unachoandika.

Waarabu na wa Iran ni race mbili tofauti, lkn pia unachotakiwa kufahamu kwamba hizo nchi ambazo zilipigana na Israel ni maadui wakubwa wa Iran miaka na miaka. Katika thread yangu nimekwambia kwamba mwaka jana Iran iliwahi kupiga rocket katika mitungi inayohifadhi mafuta kule Saudia Arabia, sasa hiyo tu ya kuunguza mitungi ya mafuta na mengineyo ikuoneshe kwamba wa iran hawana urafiki wala uhusiano na nchi za kinafiki za kiarabu, kizungu, kichina nk.

Hebu kasome historia ya waajemi katika biblia afu urudi hapa tuendelee, maana siwezi kubishana na mtu asiejua historia ya biblia kuhusu waajemi, siwezi kubishana na mtu ambae anashindwa kutofautisha waajemi na waarabu nk.
 
Ni kama wewe unavyoamini kile kitabu cha mnyaazi, hahaah...
Mimi siamini kila kinachoandikwa, lkn pia simfagilia mtu kwa sababu ya dini, ndio maana katika mada nimekuwekea kipengele kinachoonesha kuwa Iran iliiwahi kuipiga Saudia Arabia bila kujali kuwa Saudia Arabia iliyopigwa ni nchi ya kiislam au nini. Ila wewe unatetea kwa vile unaona imetajwa Israel ndio tatizo. Yani huko kwenye Saudia nilipotaja hukupaona wew umekimbilia kuona kwenye Israeli hapo ndo ulipokosea.
 
Umeandika pumba tupu, kichwa chako ni cha hovyo akina akili.
ni nchi ambayo iliweka misingi imala ya UONGOZI
Asikwambie mtu DEMOCRASIA inadumaza

ukitaka nchi yako ifanikiwe na ipige HATUA achana na DEMOCRASIA
DEMOCRASIA ni mtego mbaya wa WESTERN
ili kuendelea kukutawala na kukididimiza
CHINA ingekuwa imefuata huo upuuzi isingefika pele ilipo same na IRAN pia

hata ULAYA na AMERICA iliichukua mamia ya miaka mpk kuja kuwa na SERA ya DEMOCRASIA baada kuwa imejengeka na wamekuwa IMARA

Ndio maana hatahapa NCHINI kwetu tunahitaji RAISI mwenye kariba ya HAYATI MAGUFURI Ili kusonga mbele
DEMOCRASIA kwangu mimi ni ADUI mkubwa kwa MATAIFA yanayoendelea kama hapa NCHIN kwetu
 
Kama siyo taifa teule, tupe maandiko ambayo yanaonyesha Mungu kujitwalia taifa tofauti liwe taifa teule badala ya Israel. Usichokijua ni kwamba hatma ya taifa la Israel imeandikwa hadi kiama, hata hukumu yao ni tofauti na watu wa mataifa. Wao hadi idadi yao watakaoingia mbinguni kutoka kila kabila imetajwa..........na hata mji wa Yerusalemu mpya utakuwa na malango kumi na mbili kwa ajili ya makabila kumi na mbili ya Israel. Kwa hiyo watu wa mataifa mengine kutaka kujilinganisha na Israel kisa wamekuwa wakiadhibiwa na Mungu ni sawa na mtu kuingilia ugomvi usiomhusu.​
Kama mungu analeta ubaguzi wa kuchagua nchi moja na makabila 12 tu, na kuacha mamia ya nchi na maefu ya makabila basi huyo mungu hana sifa za kuwa mungu.

Ni kwanini aumbe dunia nzima afu achague nchi 1 na mataifa 12.

Kama aliona kuwa hiyo nchi na makabila yake 12 ndio vinahitaji baraka zake, sasa kulikuwa na haja gani ya kuumba nchi zingine na maelfu ya makabila?

Si angeumba hilo hilo taifa 1 na makabila 12 basi inatosha, kuliko kubagua makabila na nchi zingine ambazo sio za Israel afu na wao wakimbagua huyo mungu kama alivyowanagua eti siku ya mwisho mungu huyo huyo awachome!!!

Huyu raisi wa China anajitambua sana, ameukwepa mtego wa kuamini kwamba dunia nzima tutegemee mstakabali wa nchi moja yenye makabila 12 tu.
 
Back
Top Bottom