Iran Yajiandaa na Operation True Promise 3 kutekelezwa kabla ya Tarehe 5 November. Vyombo vya habari Nchini Israel vimeripoti

Vyombo mbalimbali vya habari Nchini Israel na Iran vimeripoti hii Leo kuwa Iran inajiandaa kuishambulia Israel kwa

makombora ya ballistic. Imeelezwa kuwa hii Leo Iran imehamisha makombora yake kuelekea magharibi mwa Iran kwaajili ya maandalizi ya kujibu mashambulio dhidi ya Israeli.

Itakumbukwa tangu majibizano baina ya Israel na Iran kuanza baada ya kifo cha Ismail Haniye Iran imekuwa ikitekeleza Operation True Promise 1, ikaja Operation True Promise 2 na sasa unakuja Operation True Promise 3 ambayo inatajwa kuwa itakua kubwa kuliko zote zilizopita na itatekelezwa kabla ya Tarehe 5.

Binafsi nadhani kuanzia kesho usiku mpaka jumamosi tutaona moto ukiwaka TelAviv na maeneo mengine.
View attachment 3140014View attachment 3140015
Israel wanachobugi kwa Iran ni kumheshimu Ayatollah.

Wangelimuweka kwenye orodha kama walivyomfanya Nasrallah ili ahamishiwe shimoni akafichwe humo na baadaye wamuue.

Bila ya kumuua Ayatollah, malipizi ya show off yataendelea.
 
Uko sahihi. Taifa huingizwa vitani na mtu mmoja tu; usually "kichwa". Kikikatwa na vita inakuwa imeisha.

Tatizo kwa sasa kichwa kinalindwa kuzidi malkia wa nyuki; kumfikia malkia ni lazima nyuki wa kutosha wateketee! It's doable but ni kashfa.
 
Kama watafanya hili itapendeza sana wazayuni wanatakiwa wafe wote au warudi kwao Poland na kwengine huko Europe
Tatizo la stori za kuokoteza vijiweni hizi.

Poland ama nchi za ulaya unazifungamanishaje na uhalisia wa raia wa Israel.

Nakubaliana kuwa walilazimishwa kwenda uhamishoni na kuziishi hizo nchi, lakini wayahudi wanatunza dini, tamaduni na koo zao.

Ndiyo maana pote walipoenda bila kujali miaka waliyoishi huko, utambulisho wao uliendelea kuwepo hadi walipotangaziwa kurudi nchini kwao.
 
Uko sahihi. Taifa huingizwa vitani na mtu mmoja tu; usually "kichwa". Kikikatwa na vita inakuwa imeisha.

Tatizo kwa sasa kichwa kinalindwa kuzidi malkia wa nyuki; kumfikia malkia ni lazima nyuki wa kutosha wateketee! It's doable but ni kashfa.
Mkuu kwani Nasralallah wadhani ulinzi wake ulikuwa wa kitoto?

Wakimtaka hawaendi kimakamenguvu, wanachinja kwa teknolojia kama ambavyo walimuua Rais wao Raisi.

Na uzuri hata Iran mwenyewe alishakiri kuwa kuna utitiri wa informers na mamluki wa kutosha nchini mwake na ndani ya jeshi wanaomfanyia kazi Israel, hivyo kumuua Ayatollah hawashindwi hata wakitaka leo, ila ni mipango tu hawajapanga.
 
Juzi tuu Myahudi alikuwa anaingia anapiga na kutoka kama anavyotaka ndani ya Iran, nitaamini kama Ayatollah ataingiza hata ndege moja na kupiga ndani ya Tel aviv na kutoka salama, kama ni kweli hatutaki kuja kusikia mnalalamika Myahudi anapiga watoto na kina mama au sijui hospitali
 
Hakuna ndege ya israel iliyoingia anga ya Iran, acheni kujipa moyo
 
Hizi Promises ziko ngapi kwani, mkuu? Maana nijuacho mie promise siyo surprise. Sisi watetezi wa taifa teule na taifa tweule tungependa sana kujua ili tujue la kufanya.
Hizi promises ni continuation ya majibu kwa Kila pigo atakalopigwa Israel. Kwahiyo itategemea yeye Israel anataka ziwe ngapi atachagua yeye ila Kila atakaporudisha mapigo itapigwa nyingine.
 
Israel wanachobugi kwa Iran ni kumheshimu Ayatollah.

Wangelimuweka kwenye orodha kama walivyomfanya Nasrallah ili ahamishiwe shimoni akafichwe humo na baadaye wamuue.

Bila ya kumuua Ayatollah, malipizi ya show off yataendelea.
Wanatamani sana ila sasa uwezo ndio hamna. Halafu Iran Huwa hafanyi showoff nadhani ulijionea mwenyewe moto ule wa Oktoba 1
 
Uko sahihi. Taifa huingizwa vitani na mtu mmoja tu; usually "kichwa". Kikikatwa na vita inakuwa imeisha.

Tatizo kwa sasa kichwa kinalindwa kuzidi malkia wa nyuki; kumfikia malkia ni lazima nyuki wa kutosha wateketee! It's doable but ni kashfa.
Nadhani kichwa cha Netanyahu ndio muhimu zaidi kwa amani ya mashariki ya kati
 
Mkuu kwani Nasralallah wadhani ulinzi wake ulikuwa wa kitoto?

Wakimtaka hawaendi kimakamenguvu, wanachinja kwa teknolojia kama ambavyo walimuua Rais wao Raisi.

Na uzuri hata Iran mwenyewe alishakiri kuwa kuna utitiri wa informers na mamluki wa kutosha nchini mwake na ndani ya jeshi wanaomfanyia kazi Israel, hivyo kumuua Ayatollah hawashindwi hata wakitaka leo, ila ni mipango tu hawajapanga.
Tangu mwezi wa Oktoba uanze ndani ya Israel wamekamatwa zaidi ya raia 10 wa Israel ambao wameripotiwa kutumika na Iran kwaajili ya kichwa cha Netanyahu. Nadhani ili amani ipatikane mashariki ya kati ni muhimu Netanyahu akaliwa kichwa.
 
Juzi tuu Myahudi alikuwa anaingia anapiga na kutoka kama anavyotaka ndani ya Iran, nitaamini kama Ayatollah ataingiza hata ndege moja na kupiga ndani ya Tel aviv na kutoka salama, kama ni kweli hatutaki kuja kusikia mnalalamika Myahudi anapiga watoto na kina mama au sijui hospitali
Haya matango pori Huwa mnalishwa mkiwa wapi sijui. Hakuna ndege ya Israel Wala marekani iliyoingia katika anga ya Iran
 
Mbona nasikia wanataka kurushia makombora katika ardhi ya Iraq ili wasionekane ni wao.. maana Nyumba yao ni ya Kioo kisije kikapasuka
 
Hapa ndipo mtaona ubora wa defense systems alizoleta Marekani. Inawezekana vikombora vyote vya Iran vikayeyukia angani
 
Wanapanga keshokutwa huku wenzao baada ya alah akbaru kesho jioni moto unamwagwa.
Tupo hapa.
 
Ziliingia zaidi ya 100 zikapiga na kutoka, vile viantena vyenu sojuzie mnaita 300 vilichomwa vyote , sasa mko uchi lianzisheni tena muone
Tuwekee angalau picha ya ndege moja angani Tehran basi tujiridhishe, maana waongowaongo siku hizi wamekithiri sana. Ndege mia, halafu isionekane hata moja?

Kama teknolojia ya Israeli imefikia kiwango cha juu hivyo, basi wasingekwatuliwa kwa aibu hivyo na wanamgambo wa Hamas, Hezbollah na, juzi kati hapa, Irani yenyewe.

Haiwezekani kuwa na teknolojia ya kuingia chumbani mwa adui bila kutambulika, halafu mkakosa ya kulindia vyumba vyenu wenyewe.

Unachosema bila shaka ni uongo wa kutisha au ujinga usiovumilika.
 
Back
Top Bottom