Yule kiongozi wa Hamas baada ya kuuawa kulikuwa na maoni tofauti ya viongozi wa Iran kuhusu kuishambulia Israel, lakini walitangaza watajibu... Kwa mujibu wa vyanzo vya Iran... Inasemekana rais wa sasa wa Iran hapendelei vita...
Ila baada ya Israel kummaliza Nasrallah na wale viongozi wa jeshi la Iran ndipo naona wakaamua kujibu leo...
Jana nilikuwa nimeingia WikiLeaks kusoma documents mbali mbali... Aisee US wanatengeneza spyware softwares ambazo Israel ni overrated, hao NSA wana projects zao za hatari mno..
Tuje kwenye Cyber warfare units ambapo watu wanaiona Israel ni mjuzi sana, tuache jeshi ambapo wanapata msaada kila mwaka kutoka US, Cyber warfare unit Israel kuna Unit 8200 kwa USA kuna NSA, UK wana GCHQ, Russia unit 29155 GRU, lakini hao unit 8200 bado kwa NSA... Hata Russia hawajafika..
Sijajua hizi story watu huwa wanazitoa wapi mkuu...
Kwenye jeshi ndio kabisa bila US sijui Israel maisha yangekuwa vipi...