Israel haina uwezo kupiga vinu vya nuclear vya Iran...
Iran imejifunza kwa vinu vya nuclear vilivyoshambuliwa na Israel nchini Iraq na Syria...
Operation opera Israel ilipiga vinu vya nuclear Iraq mwaka 1981, Israel ikashambulia kinu cha nuclear Syria katika operation waliita outside the box mwaka 2007... Hivyo vinu vya nuclear vyote vilijengwa kama majengo ya kawaida ambapo hata CIA waliweza kufuatilia kila kitu kinachoendelea, walijitahidi kuficha vinu hivyo jangwani lakini haikusaidia... Kwa satellite kila kitu kilikuwa wazi...
Kwa kutumia ndege vita Israel wakashambulia...
Iran haikutaka kufanya makosa, vinu vyao vipo deep underground, sio deep underground tu , vimewekwa chini kabisa ya milima.. Halafu vipo locations tofauti tofauti..
Kwa jiografia Iran ni nchi yenye milima mikubwa na ipo mingi, wameweka vinu vyao chini ya milima na kuweka concrete juu ngumu sana...
Mbali na hapo vinu vyao vinalindwa na air defenses na AAA(anti aircraft artillery) , kwa kutumia bomber kama F16 lazima ndege iruke usawa wa target na kuachia bunker buster... Kitu ambacho air defenses zitashambulia ndege..
Hata bunker buster ya tons 16 ambayo US wanayo haiwezi haribu hivyo vinu...
Israel bomber anazotumia ni F15 na F16 labda kwa sasa na F35..
Kingine F15 na F16 hazina uwezo ku handle uzito wa bunker buster kwenda kupiga Iran kwa huo umbali, fuel haiwezi kutosha kuifikisha ndege kama F15 au F16 kupiga nuclear facility Iran... Bunker buster ni nzito mno kumbuka...
Operation opera na outside the box pale Syria ndege vita zilibeba tanks za ziada na baada ya mashambulizi walitupa tanks hizo kupunguza mzigo ili ku manage fuel consumption, walitumia pia mbinu ya kuruka kwenye high altitude wakati wa kurudi baada ya shambulizi...
Ndege vita kama F15 au F16 zinaporuka altitude ndogo huwa zinakula mafuta zaidi kuipa ndege thrust kwenda mbele tofauti na ikiwa anga za juu zaidi... Lakini wanapita chini kukwepa radars...
Hapo umeona kuna ugumu kiasi gani kushambulia vinu vya nuclear Iran...
Ndio maana Israel imekuwa ikitumia njia kama kuua wanasayansi wa atomic wa Iran ili kuzuia zoezi hilo ambapo imeshindikana pia...
Vinu vya nuclear Iran vingekuwa vimejengwa kama uwanja wa Mkapa, tayari Israel ingeshalipua muda mrefu sana..