Hizo batteries chache ziliwahi fanya nini mbona Israel inapita anga la Syria kama uchochoro. Ina maana batteries chache hazilindi hata mji mkuu, Damascus?
Kama haziwezi linda airbase muhimu iliyopo mji mkuu zinalinda kitu gani au ziwa mojawapo uko vijijini.
Uturuki iligomewa na Marekani kuuziwa Patriot ndipo wakaamua kwenda kununua S-400. Hiyo ni second option, ni fungu la kukosa.
Bisha nikuletee kauli za Erdogan na Waziri wake wa Ulinzi
View attachment 2907703Ni kama ambavyo Turkey walifikiria option nyingine baada ya kunyimwa F-35. Na ambavyo walikuwa wafikirie options nyingine kama Marekani isingekubali kuwauzia F-16 mwaka jana.
Then kelele za kusema Iran ina mifumo sawa na S-400 au S-300 zikome. Ni dharau kulinganisha mifumo ya Iran dhidi ya ya Urusi.
India ilinunua S-400 kutoka Urusi muda uleule inasaini na Israel kununua Barak AD. Ni mifumo tofauti kidogo hivyo sio ajabu kununuliwa kwa pamoja.
Kwa China ni case tofauti, China ilinunua S-300 ikafanya reverse engineering ikatoa HQ-9 series zinafanana mno. Ikaagiza S-400 sababu haina long range, sasa kwa case ya Iran mnasema Iran ina mifumo bora kuzidi ya Urusi sijui inalingana, hapohapo Iran inanunua mifumo ya category ileile Urusi?
Na bora kwa China kuna some cases copycats zake zinazidi uwezo original za Urusi. Kama HQ-17 inaizidi Tor-1 sababu ni two decades apart, ila ni copy.
Kwahiyo Iran ana mifumo ya anga inazidi ya Urusi, kwamba Urusi kuna siku ataenda Iran anunue hii mifumo mipya inayozidi ya kwake? Maana huu ndio ubishi wangu.
Marekani ana pact na Europeans, tena kama hao Israel huwa anatoa funds yeye na wataalamu wake baadhi kuunda hiyo mifumo. Then baadae anaweza nunua sababu amefanya investment. Tofauti na Iran na Urusi.
Mleba❌ Muleba✅
tsh❌ Tsh/TSH.✅
wakwambie huiunganishe❌
kuponda ,hivi❌ (mkato huwekwa baada ya neno, sio kabla ya neno)
waafirika❌ Waafrika✅
Lugha unayoshinda nayo kila siku huijui, sembuse mambo ya teknolojia.
Kwahiyo Iran ina AD systems nzuri kuliko Russia? Jibu