Iraq: Iran yashambulia kwa makombora kambi mbili za Jeshi za Marekani, Ain al-Asad na Erbil

Iraq: Iran yashambulia kwa makombora kambi mbili za Jeshi za Marekani, Ain al-Asad na Erbil

Iran Fires 15 Ballistic Missiles at US Bases in Iraq, 11 Hit Targets - Reports
Iran launched a total of 15 ballistic missiles at US bases in Iraq, 11 of them hit the targets, ABC News reported on Wednesday citing a defence official.
===
(11/15)× 100=73%. Accuracy siyo mbaya. Kwa hiyo, Patrotic ina accuracy ya kulinda ngome kwa 27%. Jeshi la marekani liko hatarini. Maana tunaambiwa Makamanda wa US wako tayari 24/7.
===
There are "no US casualties" from Iran's missile strike, Fox News reported, citing a military official in Baghdad.
- - -
Fox news bwana !
 
Cha kusikitisha zaidi mataifa yote mawili hayapigani kwenye ardhi za nchi zao, bali wanapigania Iraq ambapo tayari Iran inaamini kwamba ni Marekani ndogo baada ya Marekani kuihodhi Iraq kwa kisingizio cha kuijenga upya na kulinda amani.
Mwisho wa siku wa Iraq ndio hasa watakao athirika na hii vita ya mafahari wawili.
By the way, mbona Marekani iliwaondoa wanachi na majeshi yake yote huko Iraq..??
Sasa Iran anapo shambulia vituo vya Marekani ilhali tayari Marekani iliwaondosha watu wake, Je hapo Marekani ana athirika vipi..??

Sent using Jamii Forums mobile app
Kuna barua ilitoka kwamba usa anatoa jeshi jana waziri wa ulinzi ameitengua. Which means jeshi la usa bado liko Iraq.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hakuna madhara , Iran wamewah Sana kustrike back mda ambao kambi zote za marekan zpo under high alert , Bora hata wamtafute mtu mmoja mhimu wa Marekan wamuue kuliko kufanya ujinga wanaofanya ....
Nadhani wamelenga ku'clipple' vifaa vinavyoweza kuwadhuru...maana wanajua wanajeshi wa miguu wa US lazima wawaze mara mbili kutia mguu Iran.
 
Hakuna madhara , Iran wamewah Sana kustrike back mda ambao kambi zote za marekan zpo under high alert , Bora hata wamtafute mtu mmoja mhimu wa Marekan wamuue kuliko kufanya ujinga wanaofanya ....
Siku zote marekani hajawahi kuwa mkweli kwa hiyo tusitegemee kupata taalifa zakweli kuhusu madhara yaliyo tokea.
 
Kama jinsi dola ya Uajemi na Waamedi chini ya mfalme Cyrus ilivyoipiga na kuizima Babylon ya kale, huenda Dola la Uajemi la sasa likaiangusha Babylon ya sasa (Marekani).
Marekani ni Taifa lenye nguvu lakini limekuwa Taifa litendalo ouvu mwingi sana duniani kama vile vita za kuua mamilioni mfano Vietnam, Iraki n. k. Limekuwa Taifa la matendo ya ushoga n. k
Sasa ni kinyume chake

Sent using Jamii Forums mobile app
 
1578456943098.png

Karibu kambi mbili za wanajeshi wa Marekani nchini Iraq zimeshambuliwa kwa makombora kadhaa, kwa mujibu wa idara ya ulinzi ya Marekani.

Runinga ya kitaifa ya Iran imetangaza kuwa shambulio hilo ni la kulipiza kisasi mauaji ya kamanda mkuu Qasem Soleimani aliyeuawa katika shambulio la ndege isiyokuwa na rubani mjini Baghdad, kufuatia agizo la rais wa Marekani Donald Trump.

Pentagon inasema kuwa karibu kambi mbili zilishambuliwa, mjini Irbil na Al Asad.

Bado haijafahamika kama kuna majeruhi wowote kutokana na shambulio hilo.

"Tunafahamu ripoti ya mashambulizi dhidi ya kambi ya kijeshi ya Marekani nchini Iraq. Rais amefahamishwa kuhusu tukio hilo na anafuatilia kwa karibu hali ikoje katika eneo hilo ili kushauriana na kamati ya kitaifa ya usalama," Taarifa ya msemaji wa ikulu ya White House, Stephanie Grisham.

Jeshi la ulinzi la Iran Revolutionary Guard limesema kuwa shambulio hilo ni la kulipiza kisasi kifo cha Soleimani cha Ijumaa iliyopita .

"Tunaonya washirika wote wa Marekani,ambao wameruhusu vikosi vya Marekani kuwa katika ardhi yao, kwamba wakijaribu uchokozi wa aina yoyote dhidi ya Iran yatalengwa," ilisema kupitia taarifa yake iliyotolewa shirika la habari la Iran, IRNA news agency.

Mashambulio hiyo yalifanyika saa kadha baada ya mazishi ya Soleimani.

Shambulio la pili lilifanyika katika mji wa Irbil muda mfupi baada ya roketi ya kwanza kugonga Al-Asad, kituo cha televisheni cha Al Mayadeen kiliripoti.
 
Back
Top Bottom