Iringa: Kanisa Katoliki lawazuia waumini walioshiriki kongamano la Mwamposa kutopokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu mpaka watakapoungama

Hao maparoko hawajui kitu

Yesu mwenyewe aliagiza

Mathayo 10:8​

Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.

Wanashangaa Mwamposya kuponya wajishangae wao kwa nini hawaponyi wagonjwa
 
Katoliki hawaendeshwi na mihemko, ile ni Taasisi inaendeshwa kwa mifumo thabiti.

Hao wanaotaka 'miujiza' ya papo kwa papo na kutaka utajiri pasipo kufanya kazi na kujiwekea malengo ni 'malaya' wa kiimani.

Kabisa kabisa
 
Wanawaburuza watu wasiolielewa neno na wasiosoma biblia,,

Hilo neno sioni aliposema padre, mchungaji, mtume, nabii n.k,

Neno linajitosheleza sana, " amwaminiye Bwana Yesu atafanya yote aliyofanya Bwana Yesu, na tena makubwa kuliko aliyofanya yeye"
 
Ni sahihi kabisa hata Mungu hapendi michanganyo kama wameona Kwa mwamposa ndio kuliko sahihi si wahamie huko huko Kuna mtu atawakataza? Ila sio kuwa ndumila kuwili huku unataka na huku unataka
 
Waache wafuate wanapotaka na kuona kuwa sahihi, waende huko huko sio wanataka mafuta ya upako na sakrament wanataka huo ni uzinzi kiroho, wakiamua kwenda Kwa Mwamposa na waende ila habari ya kwenda na kurudi haikuzi Imani na sio uhuru unaotakiwa
 
RC wapo sahihi Kabisa

Waumini wa RC wanaotaka kuhamia kwa Mwamposa au Imani nyingine wapo Huru kufanya hivyo muda wowote ila hawataruhusiwa kurudi RC na kuendelea kuwa Waamini hadi watubu dhambi zao

Wanachotakiwa kufanya Waamini hao ni kuamua kuondoka RC au kubaki RC na siyo kuchanganya madesa
 
Ukienda kwa mwamposa unarudi na alama usoni? Je, kwa mikwara hiyo watawatambuaje hao waumini hata wawazuie kupokea hiyo wasemayo >ekaristi<?
Ndugu Hilo Zuio Usilitazame Kimwili. Ni zuio la Kiroho.

Katika Hali ya kawaida,
Waumini wa Kanisa La Kristo Pote Ulimwenguni wanafahamu kuwa wakivunja Amri za Mungu na Za Kanisa wanajitenga wenyewe na Sakramenti Ya Ekaristi Takatifu (Mwili na Damu Ya Yesu).

Hivyo waumini walioasi mafundisho ya Kanisa wanakumbushwa kutokula hukumu.

Tumsifu Yesu Kristo.
 
Watu wengi wanaotoa maoni yao humu hawana uelewa na sheria na taratibu za Kanisa Katoliki.Kwanza kabisa itambulike kwamba Misa Takatifu ni sehemu muhimu sana ya maisha ya mkatoliki.

Unapobatizwa, Unapopata komunyio pamoja na Kipaimara unafanywa kuwa askari hodari wa Yesu.Mfano unapokuwa mwanajeshi wa JWTZ maana yake umekula kiapo na daima kuwa mtii kwa jeshi,Na Viongozi wakuu wa jeshi mpaka kufa kwako.Inapotokea mwanajeshi amehamia jeshi lingine moja kwa moja huyo ameasi.

Vivyo hivyo unapoenda kinyume na taratibu na mafundisho ya kanisa unakuwa umeasi.

Kanuni ya Imani

Nasadiki kwa Mungu, Baba Mwenyezi, mwumba mbingu na dunia.
Na kwa Yesu Kristu, Mwanaye wa pekee, Bwana wetu; aliyetungwa kwa Roho Mtakatifu,
akazaliwa na Bikira Maria,
akateswa kwa mamlaka ya Ponsyo Pilato,
akasulubiwa, akafa, akazikwa, akashukia kuzimu;
siku ya tatu akafufuka katika wafu;
akapaa mbinguni; amekaa kuume kwa Mungu Baba Mwenyezi;
toka huko atakuja kuwahukumu walio hai na wafu.
Nasadiki kwa Roho Mtakatifu,
Kanisa takatifu katoliki,
ushirika wa Watakatifu,
maondoleo ya dhambi,
ufufuko wa miili, uzima wa milele.
Amina.

Sakramenti zote ni TAKATIFU sana kwa mujibu wa mafundisho ya mama kanisa.Kwenda katika mafundisho yanayokinzana na mafundisho ya kanisa tena kwa kuamini ni kujitenga na kuukana UTAKATIFU wa Sakramenti ulizonazo. Hivyo ili kurudi katika mstari ni lazima wote wapate Sakramenti za kitubio na kukiri tena imani zao ili wawe wakristu tena.
 
Bado Kakobe
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…