Iringa: Kanisa Katoliki lawazuia waumini walioshiriki kongamano la Mwamposa kutopokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu mpaka watakapoungama

Iringa: Kanisa Katoliki lawazuia waumini walioshiriki kongamano la Mwamposa kutopokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu mpaka watakapoungama

Wanawaburuza watu wasiolielewa neno na wasiosoma biblia,,

Hilo neno sioni aliposema padre, mchungaji, mtume, nabii n.k,

Neno linajitosheleza sana, " amwaminiye Bwana Yesu atafanya yote aliyofanya Bwana Yesu, na tena makubwa kuliko aliyofanya yeye"
Unadhani wewe umesoma na unaifahamu Biblia kuliko Padre? Unaifahamu injili ya Barnaba? Haufahamu hata vitabu vya deutekaranoni wala haufahamu historia ya Biblia achilia mbali maandiko yaliyomo kwenye Biblia! Haulifahamu Nemo wewe! Kaa utulie
 
Yote makosa ila hatuna wajibu wa kuhukumu!
Nimeenda kwa mganga, nimechepuka, nimeenda kwa mwamposa, nimeiba kwa kalamu ofisini, nimejiuza hayo tumwachie MUNGU
Fanya yote hayo lakini usiende kuchafua karamu ya Bwana! Ekaristi ni mwili na damu ya Yesu! Hauwezi kuwa mchafu alafu ujongee katika karamu ya Bwana!
 
Hao maparoko hawajui kitu

Yesu mwenyewe aliagiza

Mathayo 10:8​

Pozeni wagonjwa, fufueni wafu, takaseni wenye ukoma, toeni pepo; mmepata bure, toeni bure.

Wakashangaa Mwamposya kuponya wajishangae wao kwa nini hawaponyi wagonjwa
Kanisa linaponya law njia na mafundisho sahihi kama Yesu alivyoagiza! Si kama wafanyavyo wengine ambao wengi wao ni matapeli
 
Nimeshangaa juu ya tamko lao kuhusu uponyaji wa magojwa, nanukuu:

"Tunakemea na kubeza mafundisho potofu ya uwongo (bandia) kama vile ...kuwaponya wagonjwa, ..."

Yesu mwenyewe alisema:

Yohana 14:12​

Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.

Maana ake kama vile Yesu alivyoponya magonjwa, na wafuasi wake wanaponya magonjwa, nk. Sijajua wanatumia maandiko gani kwa hili!!!
Haujaelewa walichomaanisha.Kuponya wagonjwa sio tatizo.Bali kuponya wagonjwa kwa mafundisho ya uongo ndiyo tatizo.
 
Wala Kanisa halijatumia mabavu kama unavyodhani. Siku zote Kanisa Katoliki lina misingi na kanuni zake. Ukikiuka, lazima uwajibishwe ipasavyo. Haijalishi wewe ni muumini wa kawaida, mtawa, Padre, au Askofu!

Hivyo hakuna jipya hapo.
Sista alotiwa na muimba kwaya parokia ya Mt benadeta,akahamishiwa kipalapala,unazungumzia misingi gani!?
 
Ni kweli kanisa katoliki linataratibu zake na hukumu hiyo ni ya haki kulingana na Canon law.Hivyo mtu hatakiwi kuwa vuguvugu nusu mkatoliki nusu mlokole huo ni unafiki,hivyo wanastahili kabisa kuonywa ili warudi kundini.Kufungiwa Sakramenti ni haki yao. Ndio maana mfuasi wa kanisa la kilokole akikutwa amelewa anatengwa lakini kwa mkatoliki hata alale baa hawezi kuandikiwa waraka mkubwa kama huu.Lakini biblia ndio inayotoa msimamo wa maisha ya Mkristo.Hapa namaanisha Mkatoliki ana taratibu zake,mlokole,msabato,Mluteli,Methodists,Mashahidi wa Yehova na wengine wengi wana kanuni zao za imani ila hawa mama yao ni katoliki kama ilivyoandikwa kwenye ufunuo 17.Wakristo wao wanaongozwa na biblia tu.
 
Mtu yeyote mwenye akili akisoma huo waraka atakuwa upande wa kanisa, Yani watu wanaambiwa waombewe ili wawe matajiri kitu ambacho hata Yesu hakufanya, Kama hufanyi kazi huwezi kuwa tajiri
Yesu aliomba,wakanasa samaki wengi,baada ya kukosa kwa majaribio ya kutosha
 
Sista alotiwa na muimba kwaya parokia ya Mt benadeta,akahamishiwa kipalapala,unazungumzia misingi gani!?
Kama hakuna ushahidi wa kujitosheleza, hizo zitaendelea tu kubakia kama tetesi. Ila taratibu za Kanisa ziko wazi kabisa. Wapo maelfu ya Watawa, Mapadre na pia Maaskofu walio ondolewa/ kufukuzwa kwenye hizo nafasi zao baada tu ya kukiuka miiko ya viapo vyao.
 
Ni kweli kanisa katoliki linataratibu zake na hukumu hiyo ni ya haki kulingana na Canon law.Hivyo mtu hatakiwi kuwa vuguvugu nusu mkatoliki nusu mlokole huo ni unafiki,hivyo wanastahili kabisa kuonywa ili warudi kundini.Kufungiwa Sakramenti ni haki yao. Ndio maana mfuasi wa kanisa la kilokole akikutwa amelewa anatengwa lakini kwa mkatoliki hata alale baa hawezi kuandikiwa waraka mkubwa kama huu.Lakini biblia ndio inayotoa msimamo wa maisha ya Mkristo.Hapa namaanisha Mkatoliki ana taratibu zake,mlokole,msabato,Mluteli,Methodists,Mashahidi wa Yehova na wengine wengi wana kanuni zao za imani ila hawa mama yao ni katoliki kama ilivyoandikwa kwenye ufunuo 17.Wakristo wao wanaongozwa na biblia tu.
Katoliki na walokole wote so no wa yesu!?
 
Huu nao ni utumbo, wanamtisha nani, kila mtu ana haki ya kuabudu anachokiamnini, au wanahisi wanasimamia watoto wa chekechea?

Mtu ana uhuru wa kuwa anapotaka na siyo kushikwa masikio kama mbuzi anapelekwa machinjioni

Kama wakienda huko wanapokea uponyaji, watakuwa wanakosea sana,

Kuna story moja ndani ya biblia ipo very interesting, inafanana sana na wanachofanya hao mapadre wakatoliki,

Yohana 9: 16...., nakazia mstari wa 22 na 25

Waache wafuate imani wanayoona inawasaidia maishani mwao!!
Wa kwako ndio utumbo zaidi. Uhuru wa kuabudu hauna maana ya kanisa kuunga mkono mafundisho potofu. Kanisa Katoliki linaamini kuwa kinachofanywa na akina Mwaposaya and the like ni upotofu. So haliwezi kuacha waumini wake wakimbilie kwenye imani potofu. Wanachoweza kufanya wale wanaoona Mwamposya yuko sawa, ni kuacha mazima imani ya Kikatoliki then wakajiunge na hiyo imani ya kununua mafutas na maji!
 
Kama hakuna ushahidi wa kujitosheleza, hizo zitaendelea tu kubakia kama tetesi. Ila taratibu za Kanisa ziko wazi kabisa. Wapo maelfu ya Watawa, Mapadre na pia Maaskofu walio ondolewa/ kufukuzwa kwenye hizo nafasi zao baada tu ya kukiuka miiko ya viapo vyao.
Komeo lilifungwa kwa nje,na paroko alithibitisha,hazikuwa tetesi
 
Komeo lilifungwa kwa nje,na paroko alithibitisha,hazikuwa tetesi
Hilo siwezi kulisemea maana sikuwa mmoja wa mashuhuda. Ila binafsi nimeshawahi kushuhudia watawa zaidi ya wawili waliofukuzwa utawa kwa ujauzito, nk.

Na jambo hilo siyo la kushangaza. Maana na wenyewe ni binadamu. Hivyo kama wameshindwa kuishi maisha ya utawa, wanaruhusiwa kuwa Walei kama sisi.
 
RC wapo sahihi Kabisa

Waumini wa RC wanaotaka kuhamia kwa Mwamposa au Imani nyingine wapo Huru kufanya hivyo muda wowote ila hawataruhusiwa kurudi RC na kuendelea kuwa Waamini hadi watubu dhambi zao
Unamaanisha kuwa dhehebu jingine la kikristo, nje ya ukatoliki ni dhambi ?
 
Back
Top Bottom