Iringa: Kanisa Katoliki lawazuia waumini walioshiriki kongamano la Mwamposa kutopokea Sakramenti ya Ekaristi Takatifu mpaka watakapoungama

Halafu kwenye ule mkanyagano uliowahi kusababisha vifo vya waumini; kwa harufu ya sasa inaonekana kama zilikuwa ni hujuma zilizofanywa makusudi ili kuichonganisha Serikali ya kipindi hicho na taasisi za dini. Ilitarajiwa kuwa hayati JPM angechukua hatua kali dhidi ya tukio hilo, halafu sasa waliokuwa kazini wangeitumia fursa hiyo ili kuchochea moto upande mwingine ule wa pili.

Mwamposa amekuwa akifanya haya matamasha siku zote na mara zote waumini wake wamekuwa wakiyafanya na kuondoka salama, iweje kwenye tamasha hilo tu watu wakanyagane hadi kufikia kiwango cha waumini hao kupoteza maisha na kwa wingi kiasi hicho? Kwa tukio hili mtumishi huyu inabidi aliangalie kwa jicho la pili

Kwa hili la RC, ni kawaida kabisa hamna cha ajabu kwa sababu RC wenyewe wako very strict na ni watu wa principles tu siku zote. Madhahabu ya Bwana kwenye Kanisa la RC inaheshimika nadhani kuzidi makanisa yote ya Kikiristo; kwa maana kuwa halipo kanisa la kikiristo linaloheshimu madhabahu ya Bwana, kama Kanisa la RC. Nilizaliwa na wazazai wa RC, nikabatizwa RC, nikapata kipaimara RC. Nawajua RC in and out!
 
Unaanzaje kumzuia mtu kumuabudu MUNGU?
He mbona tunaenda kwa waganga na walozi Kisha tunarudi kanisani hatufukuzwi?
Kanisa ni kwa wale tuliowaovu sio wasafi, hata YESU alikuja kwa ajili ya waovu
Umeshasikia mtu kazuiwa kumwabudu MUNGU kisa alifumaniwa?
Hawazuiwa kwenda kumuabudu Mungu, wameambiwa hawatapewa ekaristi takatifu hadi waungame.
Hata ukifumaniwa hukatazwi kumwabudu Mungu ila hutapewa ekaristi takatifu hadi uungame.
Ndivyo mimi nimeelewa, na huo ni utatatibu ukionwa unafanya dhambi inabidi uungame.
 
Na RC HUWA hawatanii utasikia na ukifa hatukuziki hata kama mkisafirisha hatuwapi barua ya utambulisho huko muendako.
Kwani wasiponizika inasaidia nini wakati tayari sipo duniani?kwanza kuzikwa hakuna umuhimu wowote kuhusu kule uendapo kinachoangaliwa matendo yako ulipokuwa hai,wakristo tuamke.
 
Nimeshangaa juu ya tamko lao kuhusu uponyaji wa magojwa, nanukuu:

"Tunakemea na kubeza mafundisho potofu ya uwongo (bandia) kama vile ...kuwaponya wagonjwa, ..."

Yesu mwenyewe alisema:

Yohana 14:12​

Amin, amin, nawaambieni, Yeye aniaminiye mimi, kazi nizifanyazo mimi, yeye naye atazifanya; naam, na kubwa kuliko hizo atafanya, kwa kuwa mimi naenda kwa Baba.

Maana ake kama vile Yesu alivyoponya magonjwa, na wafuasi wake wanaponya magonjwa, nk. Sijajua wanatumia maandiko gani kwa hili!!!
Eti kuwaponya wagonjwa ni mafundisho potofu?! Inashangaza sana aisee
 
Unaanzaje kumzuia mtu kumuabudu MUNGU?
He mbona tunaenda kwa waganga na walozi Kisha tunarudi kanisani hatufukuzwi?
Kanisa ni kwa wale tuliowaovu sio wasafi, hata YESU alikuja kwa ajili ya waovu
Umeshasikia mtu kazuiwa kumwabudu MUNGU kisa alifumaniwa?
Mwamposa pia Ni mganga wa kienyeji anayevaa Suti
 
Mwamposa alisimamisha mkoa wote pale iringa,hakukua na shughuli yoyote iliyoendelea kwa siku 3
Kuna dogo alinyang'anywa Bajaji na bosi wake. Amekaa wiki mbili hana KAZI. Siku Mwamposa ametua Iringa dogo akaenda kuombewa. Ametoka tu kuombewa akapigiwa simu na bosi njoo uchukue Bajaji. Dogo alinisimulia huku anatoa machozi ya furaha. MTU kama HUYO ukimwambia Mwamposa tapeli atakuelewa?
 
Huo ni ushetani sasa
UMEONGEA UKWELI WA MUNGU.

TENA MAPADRI NA MASISTA NDIO WANAONGOZA KWA UCHAWI.
KUNA SHULE YAO MOJA YA WASICHANA IPO MOSHI, UCHAWI UNAOFANYIKA PALE UTASEMA SIO SHULE YA WAKATORIKI!.
 
Halafu kwenye ule mkanyagano uliowahi kusababisha vifo vya waumini; kwa harufu ya sasa inaonekana kama zilikuwa ni hujuma zilizofanywa makusudi ili kuichonganisha Serikali ya kipindi hicho na taasisi za dini. Ilitarajiwa kuwa hayati JPM angechukua hatua kali dhidi ya tukio hilo, halafu sasa waliokuwa kazini wangeitumia fursa hiyo ili kuchochea moto upande mwingine ule wa pili.

Mwamposa amekuwa akifanya haya matamasha siku zote na mara zote waumini wake wamekuwa wakiyafanya na kuondoka salama, iweje kwenye tamasha hilo tu watu wakanyagane hadi kufikia kiwango cha waumini hao kupoteza maisha na kwa wingi kiasi hicho? Kwa tukio hili mtumishi huyu inabidi aliangalie kwa jicho la pili

Kwa hili la RC, ni kawaida kabisa hamna cha ajabu kwa sababu RC wenyewe wako very strict na ni watu wa principles tu siku zote. Madhahabu ya Bwana kwenye Kanisa la RC inaheshimika nadhani kuzidi makanisa yote ya Kikiristo; kwa maana kuwa halipo kanisa la kikiristo linaloheshimu madhabahu ya Bwana, kama Kanisa la RC. Nilizaliwa na wazazai wa RC, nikabatizwa RC, nikapata kipaimara RC. Nawajua RC in and out!
Asante mkuu,RC ndivyo tulivyo.
 
Kuna dogo alinyang'anywa Bajaji na bosi wake. Amekaa wiki mbili hana KAZI. Siku Mwamposa ametua Iringa dogo akaenda kuombewa. Ametoka tu kuombewa akapigiwa simu na bosi njoo uchukue Bajaji. Dogo alinisimulia huku anatoa machozi ya furaha. MTU kama HUYO ukimwambia Mwamposa tapeli atakuelewa?
Unaamini alipata bajaj kwasababu ya mwamposa?
 
Back
Top Bottom