TANZIA Iringa: Katibu wa CCM Kilolo avamiwa na kuuawa na Watu wasiojulikana

TANZIA Iringa: Katibu wa CCM Kilolo avamiwa na kuuawa na Watu wasiojulikana

Sasa hv nan anafanya?
Wanafanya wananchi ambao wanaamini kuteka na kuua ndiyo njia ya kuwashinda wapinzani wao wa kisiasa au kibiashara kama alivyokuwa anafanya Magu.

Kama hukupata NECTA japo D 2 huwezi kuelewa
 
Watu Wasiojulikana Wanadaiwa wamemvamia aliyekuwa Katibu wa Chama Cha mapinduzi (CCM) Wilaya ya Kilolo Mkoani Iringa, Christina Kibiki na kumuua kwa kumpiga risasi.

Taarifa ambayo Matukio Daima Media tumeipata inadai kuwa watu hao Wasiojulikana wamefanya uvamizi huo usiku wa kuamkia leo Novemba 13, 2024 katika Kitongoji cha Banawanu, Kijiji cha Ugwachanya, Kata ya Mseke Tarafa ya Mlolo nje kidogo na Mji wa Iringa ambako alikuwa akiishi.

Kuwa baada ya kumshambulia kwa risasi alikimbizwa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Iringa ya Tosamaganga ambako amefariki Dunia.

Matukio Daima Media imezungumza kwa njia ya simu na Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kilolo, John Kiteve amesema tukio hilo limemgusa sana na amesikitishwa na tukio hilo.

Huku Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi hajapatikana ili kuthibitisha tukio hilo, bado Matukio Daima Media inaendelea kufuatilia zaidi.

Chanzo: Matukio Daima Media

==============================

JamiiForums imemtafuta Kamanda wa Polisi Mkoa wa Iringa, Allan Bukumbi, simu imepokelewa na msaidizi wake ambaye baada ya kuelezwa kuhusu tukio hilo akasema “Kamanda yupo kikaoni, tukio hilo bado hajalizungumzia.”


Pia, Soma:
Safi sana. Natamani wauwawe viongozi wa CCM kwa idadi inayofikia wapinzani wote waliouliwa na vyombo vya dola na wale waliouliwa na makada wa CCM, ingependeza sana halafu ndiyo tukae chini tufanye maridhiano.
 
Kama ambavyo tunapiga kelele haya kutokea kwa viongozi wa CDM, vivyo hivyo kwa CCM.

Haya hayapaswi kutokea katika jamii yetu, tuungane kuupinga unyama huu.
Kiongozi wa CCM akifanyiwa chochote siku hizi sitapiga kelele kwa sababu wao wanakuwa kimya wengine wanapouawa. Tena wanakejeli.
 
chairman alishaga waambia sumu haionjwi kwa ulimi walioskia narkutii wameskia, walioshupaza shingo ndiyo hivyo tena huku mwenyewe akiendelea kushushia nyagi, barafu na ndimu 🐒
Sisiemu mwenzenu na anajulikana kitambo kuwa ni wa kwenu .
 
Back
Top Bottom