TANZIA Iringa: Katibu wa CCM Kilolo avamiwa na kuuawa na Watu wasiojulikana

Inasikitisha sana
 
Kura za Maoni?
 
Kama ni mccm poa tu wacha wamalizane tu,alikuwa mtia nia wa ubunge.
 
CCM wanapenda kuuwana...nakumbuka wakati wa uchaguzi wa ndani wa Mwanza kuna mgombea mmoja aliweka walinzi wa Bunduki kwake mpaka uchaguzi ulivyoisha... 😭😭
 
Pole kwa familia ya marehemu, Mungu awape faraja kipindi hiki kigumu wanachopitia kwa kumpoteza mpendwa wao.
 
Watu Wasiojulikana wamemvamia aliyekuwa katibu wa Chama Cha mapinduzi CCM wilaya ya Kilolo mkoani Iringa Christina Kibiki na kumuua kwa kumpiga risasi .

Taarifa zinasema kuwa watu hao Wasiojulikana wamefanya uvamizi huo usiku wa kuamkia Leo katika Kijiji Cha njia panda ya Tosa wilaya ya Iringa Vijijini nje kidogo na mji wa Iringa ambako alikuwa akiishi.

Mwenyekiti wa CCM wilaya ya Kilolo John Kiteve amesema tukio Hilo limemgusa sana na amesikitishwa na tukio hilo huku akilaani waliohusika kuchukua uhai wa kiongozi wao.


Chanzo: Nuru FM
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…