JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 2,780
- 6,607
Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Queen Sendiga ametangaza kuwasaka wale wote wanaojihusisha na vitendo vya ukatili ndani ya mkoa huo.
Pamoja na msako huo amedai ukatili wa baadhi ya wanaume hasa wanaolewa kupindukia kunyonya maziwa ya wake zao wanaonyonyesha kwa imani ya kukata pombe unaendelea kupungua na kuwashauri wanaume hao kuacha tabia hizo.
Akizungumza jana Mei 15, 2022 wakati wa Siku ya Familia Duniani alisema Mkoa wa Iringa umejiwekea mikatika ya kukomesha matukio ya ukatili yanayojitokeza kwenye jamii na kutaka Wananchi wasikubali kufumbia macho vitendo vyovyote vya ukatili kwenye maeneo yao.
Sendiga alisema kutokana na elimu inayoendelea kutolewa dhidi ya ukatili Iringa idadi ya wanaume wanaofika dawati la jinsia kulalamika kufanyiwa ukatili na wake zao imeongezeka tofauti na mwanzo ambapo wanaume walikuwa wakiona aibu kwenda Polisi kutoa taarifa za wao kufanyiwa ukatili na wanawake.
"Tunapoona wanaume wanajitokeza kwenda dawati kulalamika kufanyiwa vitendo vya ukatili tunaamini elimu imefika na ni mwanzo mzuri wa Matukio ya ukatili kuendelea kupungua mkoani kwetu," alisema.
Hata hivyo alisema bado ukatili kwa wanawake na watoto umeendelea kuwepo japo si kwa kasi kubwa kama zamani na kutaka jamii kuendelea kuwaibua wanaofanya ukatili .
Mkuu wa Mkoa alisema iwapo wazazi watazingatia ushauri mbalimbali unaotolewa na Viongozi wa Serikali na vyombo vya usalama Kuhusu uangalizi wa watoto wao itasaidia kupunguza kabisa Matukio ya ubakaji, ulawiti na mengine kwa watoto nyakati za usiku.
Alisema vitendo vya baadhi ya wazazi ama walezi kuwatuma watoto usiku kwenye madukani ni moja ya sababu inayochochea ubakaji na ulawiti kwa watoto nyakati za usiku.
Chanzo: MATUKIO DAIMA
========================================
RIPOTI YA MWAKA 2021, WANAUME WANAONYONYA MAZIWA YA WANAONYONYESHA
Baadhi ya wanaume wenye tabia ya kunyonya maziwa ya wake zao baada ya kulewa kwa imani ya kukata pombe waonywa kuachana na tabia hiyo kwani wanamaliza lishe bora ya watoto.
Kuwa tabia hizo zisizofaa za baadhi ya wanaume wanaoendekeza ulevi wa kupindukia na hata kunyonya maziwa ya mama anayenyonyesha kwa imani ya kukata pombe kuwa si sawa maana hawawatendei haki watoto ambao wanastahili kunyonya maziwa hayo kwa lishe bora.
Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Wanawake wa Chama cha Mapinduzi Tanzania (UWT), Queen Mlozi aliyasema hayo jana wakati akifungua kongamano la lishe mkoa wa Iringa lililoandaliwa na asasi siyo ya kiserikali inayojishughulisha na masuala mbalimbali ya kijamii ikiwemo vita ya lishe bora ya Tanzania Home Economics Association (TAHEA-IRINGA).
Alisema wakati mapambano hayo ya lishe wanaendelea bado kuna haja ya elimu kwa wanaume wanaoendekeza ulevi akikemea ili wasiendelee kumaliza lishe ya watoto kwa kunyonya maziwa ya mama anayenyonyesha.
Pia suala la wanawake kuwapa pombe ya ulinzi watoto ili wakala wasisumbue wakati wao wakiendelea na majukumu mengine kuwa si nzuri.
Mlozi alisema UWT wanatambua na kupongeza kazi inayofanywa na TAHEA chini ya mkurugenzi wake, Lediana Mafulu Mg'ong'o ambae ni mmoja wa viongozi ndani ya UWT imekuwa ni chachu kubwa katika harakati za vitendo katika kutoa elimu kwa jamii juu ya lishe bora jambo ambalo ni la kupongezwa na kuigwa.
Alisema kuwa suala mkurugenzi huyo amekuwa ni mfano mwema na ni msaada mkubwa kwa UWT si tu kwa mkoa wa Iringa bali kwa Taifa zima kutokana na harakati zake nzuri za kusimamia mambo ya msingi ambayo ni Ukombozi kwa mwanamke ,watoto na watanzania kwa ujumla juu ya lishe bora.
Mlozi alisema wakati TAHEA inaendeleza mapambano dhidi ya lishe bora bado kuna haja ya mkakati huo kuchukuliwa na mikoa yote kuona elimu bora ya lishe bora ambayo watoto wanapaswa kupewa inaendelea kutolewa ili kuliepusha Taifa na tatizo la udumavu na utapiamlo ambao umeikumba baadhi ya mikoa inayoongoza kwa uzalishaji wa mazao ya chakula kama mkoa wa Iringa ,Njombe ,Mbeya na mikoa mingine jambo ambalo ni aibu kubwa.
"Kwa niaba yangu mwenyewe na kwa niaba ya mwenyekiti wetu wa UWT Taifa mama Gaudensia Kabaka naomba nikupongeze sana mjumbe wetu wa baraza Taifa Lediana Mafulu Mng'ong'o kwa kazi nzuri unayoifanya ndani ya mkoa wa Iringa maana hata inayofanywa ni mambo makubwa na mazuri ambayo tunataka na kuhitaji kwa maana sisi tuliposema tunawaita wewe ulikuwa umekwisha anza kwa sababu si kitu rahisi kufungua ofisi zinazozingumzia masuala ya lishe ndani ya mikoa 21 Tanzania sisi tunatambua kazi yako kubwa nawe ni hazina kubwa kwa Taifa " alisema katibu mkuu UWT Taifa
Kuwa kazi za mkurugenzi huyo wa TAHEA zinaonyesha wazi kuwa zimelenga kumkomboa mwanamke ni ni dhahiri zinaonyesha jinsi ambavyo Mungu alivyoumba kuwa mwanamke ni kuwa msaidizi wa familia huku baba ni kichwa cha nyumba hivyo lishe bora kwa familia ni hitaji la Taifa .
Hata hivyo Mlozi alipongeza pia kazi zinazofanywa na mkuu wa mkoa wa Iringa Ally Hapi na katibu tawala wa mkoa huo Happines Seneda katika harakati za kuunga mkono jitihada za lishe bora kwa mkoa wa Iringa na kuwaomba kuzidisha mapambano hayo .
Akizungumzia wanaume wananyonya maziwa ya wake zao wanaonyonyesha ili kukata pombe alisema kuwa wanaume wenye tabia hizo wanapaswa kubadilika na kuwa tabia hiyo zaidi ameisikia mkoa wa Iringa japo anaamini ulevi upo mikoa yote hivyo ni vizuri wanaume kujitambua na kuacha tabia hiyo kwani ina mnyima lishe bora mtoto .
Awali wakizungumza katika kongamano hilo mwenyekiti wa UWT Mkoa wa Iringa Nicolina Lulandala, Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Asia Abdallah na Makamu Mwenyekiti wa ALAT Taifa, Stephen Mhapa walisema TAHEA imeonyesha njia ya kila makundi kufanya kazi ya elimu ya lishe sehemu yake.
Huku Naibu Meya wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa, Joseph Ryata akiahidi kufikisha elimu hiyo katika baraza la madiwani ili iwekewe mkazo na kutungiwa sheria ndogo itakayosimamia lishe bora ndani ya Halmashauri hiyo.
Kongamano hilo la aina yake lilishirikisha makundi mbali mbali ya jamii kama wanasiasa kwa maana ya viongozi, wanahabari, wasanii, viongozi wa dini na makundi mengine.
A