TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

Tukio leo proves kuwa bara tuu mazoba compared na zenji
 
DAUD MWANGOSI......kapigwa na bomu wakati akiwa kazini kwenye kufungua shina na ofisi ya CHADEMA....KAFARIKI HAPO HAPO NA UTUMBO KUTOKA NJE..RPC ALIHOJIWA NA ITV NA HAKUTOA JIBU NA KUKATA SIMU...!! NGOJA TUSIKILIZE CHANNELL TEN SASA HIVI TUTAWAJUZA MORE.

haya mdau,,,pamoja na kusikiliza nakushauri pia utazame na tukio lilivokua
 
Swali lako ulilojibiwa uliuliza sababu na siyo ameuwawa na kitu gani,don't confuse yourself.Swali la kuhusu ni kitu gani kilimwua pia ulishajibiwa,wewe ulisema inakuwaje bomu limuuwe peke yake.Sijui huwa unafikiriaje wewe?!unatumia vitu gani?are you on medication?

Wewe mpuuzi usijifanye kila kitu hunajua hii forum habari ni nyingi kuhusu ili tukio kuna habari ingine humu inasema kauuwa kwenye vurugu, kuna habari zingine zinasema kapigwa risasi, kuna habari zingine zinasema kapigwa bomu, mie kuhoji imekuwa tatizo wa ngapi wamehoji ujawajibu..wewe mbona umesema nchi hatawaliki tena si maoni yako upo uhuru, mie kuhoji tatizo acha upuuzi wa kitoto.
 
kama kweli hayo yanayowauwa watu ni mabomu ya machozi,basi wanafunzi wa vyuo wangekuwa wameshakufa sana aisee,mana huwa wengine wanayatuliza kifuani na kuyapigadana dana! hizi ni risasi ndo zinatumika hapa! ila ngoja tu watakuja kuichukia hiyo kazi ya upolisi one day
 
Mwandishi wa habari Daudi Mwangosi amefariki dunia baada ya kupigwa bomu na askari polisi, mwili wake upo katika hospitali ya Mafinga. Na mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe anaitwa Mushi amekamatwa yupo chini ya ulinzi. Huyu Daudi Mwangosi ni Mwenyekiti wa waandishi wa habari Iringa. Tukio limetokea maeneo ya Nyololo. Source-Radio Ebony Iringa
 
Huyu kamanda si ndio katoka Ruvuma baada ya yale maandamano na mauaji ya kijana wa boda boda!
Nazani apelekwe Syria maana ana hamu ya kutoa amri ya kuua watu
 
[h=3]"wajumbe hii nimeipata sehemu nadhani itasadia katika updates za tukio"

HIVI NDIVYO MWANAHABARI DAUD MWANGOSI ALIVYOPOTEZA MAISHA LEO KTK VURUGU ZA CHADEMA NA POLISI
[/h]


Hapa polisi wakiwataka wafuasi wa Chadema kutawanyika eneo la tukio ofisi za Chadema Nyololo Mufindi

Mwili wa mwanahabari Daud Mwangosi ukiwa chini


Daud Mwangosi kulia enzi za uhai dakika 20 kabla ya kuuwawa kwake
Mwandishi wa habari wa Chanel Ten mkoa wa Iringa na Mwenyekiti wa chaa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa Daud Mwangosi ameuwawa katika vurugu za Polisui i na wafuasi wa Chadema katika kijiji cha Nyololo wilaya ya Mufindi mkoani Iringa leo

Mwanahabari huyo Daud Mwangosi aliuwawa majira ya saa 10 jioni katika ofisi za Chadema Nyololo huku askari mmoja akijeruhiwa vibaya kwa risasi .

Kabla ya kuuwawa kwa mwanahabari huyo mabomu yaliweza kupigwa eneo hilo kuwatawanya wafuasi hao wa Chadema ambao walikuwa wakigoma kutawanyika eneo hilo na kuamua kukaa chini kuwa haapo tayari kuondoka katika ofisi yao.

Chanzo cha mwanahabari Mwangosi kuuwawa klitokana na kukamatwa kwa mwandishi wa habari wa gazeti la Nipashe mkoa wa Iringa Godfrey Mushi na hivyo mwanahabari huyo kkutaka kuhoji polisi sababu ya kukamatwa kwa mwanahabari huyo ndipo askari hao walipoanza kumshambulia kwa kichapo na baadae mlio kama wa bomu ulisikika eneo hilo na mwandishi huyo na askari mmoja waliaguka chini .

Ndani ya dakika tano ilisikika sauti kutoka kwa askari huyo kuwa afande nimekufa ndipo walipomchukua na kumpeleka Hospitali ya wilaya ya Mufindi huku mwili wa mwanahabari huyo ukipelekwa chumba cha kuhifadhia maiti .

Katika vurugu hizo zilizodumu kwa takribani dakika 30 kwa askari na wafuasi wa Chadema kurushiana mawe kwa mabomu zaidi ya magari matano ya Chadema na ya wananchi yameharibiwa huku watu kadhaa wamejeruhiwa na mwanahabari mmoja Godfrey Mushi akijeruhiwa vibaya.

Hii ni taarifa ya Jeshi la polisi kabla ya tukio kwa vyombo vya habari


JESHI la polisi mkoa wa Iringa limesema limezuia mikutano ya vyama vya siasa kwa vyama vyote na sio kwa chama cha Demokrasia na maendeleo (CHADEMA) pekee hivyo laonya vyama vyote kutii sheria bila shuruti.

Hata hivyo jeshi hilo la Polisi limesema kuwa halifanyi kazi kwa matakwa ya chama chochote cha siasa na kuwa si kweli kama wanavyodai viongozi wa Chadema kuwa jeshi la polisi linatumiwa na chama cha mapinduzi (CCM) kuzuia mikutano hiyo.

Kamanda wa polisi wa mkoa wa Iringa Michael Kamuanda ametoa kauli hiyo leo ofisini kwake alipozungumza na waandisha wa habari kuhusu zuio la mkutano wa Chadema uliopangwa kuanza leo katika wilaya ya Mufindi.

" Nawatangazia wanasiasa na vyama vyote vya siasa pamoja na wananchi wa mkoa wa Iringa kuwa hakutakuwa na mikutano ya kisiasa kutokana na shughuli za sensa zinazoendelea ....hivyo basi nawaomba wananchi wote kutoshiriki mikutano yoyote ya kisiasa itakayoitishwa na wanasiasa "alisisitiza

Kuwa mikutano hiyo imezuiliwa kwa kipindi hiki cha sensa kilichoongezwa hadi hapo tamko litakapotolewa tena na msajili wa vyama vya siasa John Tendwa kama alivyokwisha kutoa tamko la kuzuia shughuli hizo za vyama vya siasa kwa kipindi hiki cha sensa.

"Wananchi wote wa mkoa wa Iringa mnaombwa kutii sheria bila shuruti hii ni amri ....nawaombeni sana wananchi kutodanganywa na wanasiasa kwa kuvunja sheria "aliongeza kamanda huyo wa polisi.

Hata hivyo alisema kuwa kimsingi zoezi la sensa lilipaswa kuhitimishwa Septemba mosi mwaka huu ila kutokana na serikali kuongeza muda wa zoezi hilo bado jeshi hilo la polisi linazingatia maagizo ya Msajili wa vyama vya siasa kama alivyoyatoa kwa jeshi hilo.

Kamanda Kamuanda alisema kuwa jeshi hilo la polisi wala msajili wa vyama vya siasa hajazuia vyama vya siasa kuendelea na vikao vyao vya ndani kwa kipindi hiki na kuwa hata Chadema wakiwa mkoani Iringa wameendelea kufanya vikao vyao vya ndani katika kata mbali mbali za mkoa wa Iringa na hakuna mtu aliyewazuia kuendelea kufanya hivyo.
Majibu ya Dkt Slaa
Wakati jeshi la polisi likipinga shughuli hizo za vyama vya siasa kufanya mikutano ya hadhara katibu mkuu wa Chadema Taifa Dkt Willbroad Slaa ameibuka na kusema kuwa chama chake kitaendelea na mikutano kama kilivyojipangia na kuwa wapo tayari kwa lolote litakalojitokeza .

Dkt Slaa alisema kuwa walivumilia mara ya kwanza walipozuiwa mikutano hiyo mkoani Iringa na kuvuta subira hadi jumamosi zoezi hilo lilipomalizika sasa anashangazwa kuona jeshi hilo likiendelea kuzuia mikutano hiyo tena.

"Tumemsikiliza kamishina wa sensa Hajati Amina Mrisho Said kuwa hadi sasa watu asilimia 95 wameandikishwa huku akiwata wale ambao bado kuwapigia simu wenyeviti wa mitaaa na vijiji ili wakaandikishwe na makarani wa sensa ....sasa jeshi la polisi linataka kutuambia kuwa hao watu asilimia 5 waliobaki wapo Iringa peke yake hadi wakazuia mikutano yetu? tunasema hatutakubali tutaendelea na mikutano yetu kama kawaida hatupotayari kabisa kusubiri hadi tarehe nane" alisema Dkt Slaa.

Pia alisema kuwa kama ni uzalendo sasa umefika kikomo na kuwa wataendelea na ratiba zao za mikutano kama ilivyopangwa na watapambana kwa lolote .
MWISHO



Imewekwa na Francis Godwin ni Iringa na matukio 0 Maoni Links to this postEmail ThisBlogThis!Share to TwitterShare to Facebook




[TABLE="width: 100%"]
[TR]
[TD="class: reactions-label-cell, width: 1%"]UNAMAONI GANI ? [/TD]
[TD][/TD]
[/TR]
[/TABLE]




[h=3]BREAKING NEWssssssss MWENYEKITI WA IRINGA PRESS CLUB DAUDI MWANGOSI AMEFARIKI DUNIA KATIKA VURUGU ZA CHADEMA IRINGA[/h]

Habari za hivi punde; Mwenyekiti wa Chama cha Waandishi wa Habari Mkoa wa Iringa (IPC), Daudi Mwangosi, pichani - amefariki dunia kijiji cha Nyololo, Mufindi, Iringa baada ya kutokea vurugu baina ya polisi na wafuasi wa chama cha Chadema.Habari zilizotufikia kutoka huko, zinadai kuwa Mwangosi, ambaye ni mwandishi wa habari wa kituo cha Televisheni cha Channel ten, amefariki papo hapo.




Mtandao huu utazidi kukupatia habari zaidi na picha kuhusu tukio lenyewe


 
CHADEMA itatumaliza watanzania!
Hiki chama hakitufai ata kidogo aise.......

CDM ndiyo wameua au polisi? Sijawahi kusikia hata siku moja CDM imetoa mtu hata damu na ingekuwa hivyo ungekuta kimefungiwa maana mnakiogopa kama ukoma. Na sasa jueni kuwa SSM kutumia polisi kua ndiyo mnajimaliza. Watanzania wajana si wa leo au wa leo asubuhi si wa leo jioni. Subirini 2015. SSM haina mapenzi na watanzania na ndiyo maana mnatunia polisi kuwatesa na kuwaua.
 
Juzi ameuliwa mwuuza magazeti akiwa anajitafutia mkate wake,leo mwandishi wa habari akiwa kazini! Wote hawa wawili wameuliwa chama cha CDM kikiwa ktk shughuli halali ya kisiasa kwa kujitangaza na kupata wanachama wapya. Hivi huyu Kamanda Kamuhanda siye aliyeongoza mauji mengine mwaka jana kule Songea?
 
Itakuwa kuna kikosi maalumu cha kufanya haya mambo maana yanafanyika kwa mfululizo. RIP ndugu mwandishi.
 
Mwwenyekiti na Chama cha Waandishi wa habari mkoa wa Iringa na mwandishi wa habari wa Channel 10 amepigwa risasi na polisi kwenye mkutano wa CHADEMA Mufindi

Thanks God Thanks Police RIP mwandishi wa habari kweli Mungu yu mwema na Tanzania na anaipenda Tanzania. Kweli yu mwema nadhani waandishi watafunguka sasa na kuachia bahasha. Polisi nafikiri watasema kapigwa na nondo langu Jicho
 
Ulitake wafe wangapi? Au kwa kuwa wewe upo upande wa Jeshi la Polisi la Kua Wananchi, yaani nguvu ya SSM? Kifo ni kifo tu na ni lazima tusikitike hata kama tuko na itikadi tofauti ya siasa. So sad. Haya mambo yataisha lini Tanzania?

Nani kafurahi kifo mie nimeuliza tu, hata siku moja siwezi kufuarahia mauaji, kwanza aliokufa sio mfuasi wa vyama vya siasa ni muandishi wa habari ushabiki utoke wapi.
 
chadema au polisi ndo watatumaliza! sababu ya kutumia risasi hapo ikowapi? yani wanashindwa njia za kutuliza vurugu mpaka utumie risasi ndugu, tusilete uchama kwenye maswala ya msingi mkuu! hawa jamaa wanatumia nafasi ya upolisi kinyume na kanuni za kazi yao
Sasa kama waliambiwa watawanyike wao wakakaidi ni vipi tuwalaumu police?
 
Wewe mpuuzi usijifanye kila kitu hunajua hii forum habari ni nyingi kuhusu ili tukio kuna habari ingine humu inasema kauuwa kwenye vurugu, kuna habari zingine zinasema kapigwa risasi, kuna habari zingine zinasema kapigwa bomu, mie kuhoji imekuwa tatizo wa ngapi wamehoji ujawajibu..wewe mbona umesema nchi hatawaliki tena si maoni yako upo uhuru, mie kuhoji tatizo acha upuuzi wa kitoto.

Mpuuzi ni wewe fisadi gaidi.Na mtoto ni nanihii wako...unamjuwa.
 
Kwel hii ni laana. Safar ni mwandish? Siku zile ni muuza magazet. Hapa tasnia ya habari ijiangalie.
 
kama kweli hayo yanayowauwa watu ni mabomu ya machozi,basi wanafunzi wa vyuo wangekuwa wameshakufa sana aisee,ana huwa wengine wanayatuliza kifuani na kuyapigadana dana! hizi ni risasi ndo zinatumika hapa! ila ngoja tu watakuja kuichukia hiyo kazi ya upolisi one day

hahahahaaa,,,,mdau umenikumbusha udsm 2009,,,jamaa walikua wanayakung'uta hadi kwenye makazi ya wanafunz,hall I,II,iii na IV,,,,,
ILA KWA SASA NAONA POLISI WAPO FASTA NA ROHO ZETU,,,,,SIJUI HAWA WA LOTOKA DEPO JUZI
 
wewe mbona unakua hivi??

kwahiyo kama alikua katikati ya umma ni sawa kuuwawa sio??........... do you want to justify police shooting people ?

this is the stupidest comment i have ever read in JF


Janjaweed, nimejibu kwenye post ya nyuma kidogo. Ni vema kusoma mwelekeo wa polisi kwa sasa. It is very likely polisi ina-target waandishi wa habari kama njia moja ya kuchonganisha wana habari na CHADEMA na pia kufanya waandishi wa habari waanze kuindika vibaya CHADEMA.

Nimepitia hii link Francis Godwin Mzee Wa Matukio Daima inaelekea polisi wako kwenye kazi moja tu - to kill.
 
Back
Top Bottom