TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

TANZIA Iringa: Mwandishi Mwangosi auawa katika vurugu kati ya Polisi na CHADEMA

sio siri chadema hata kama hamhusiki ni rahisi kabisa kuunganisha hizi vurugu na haya maandamano kumbukeni kuwa watanzania wengi hawajaelimika na msifananishe hata kidogo maandaman yenu na yale yaliyotokea kule Misri kwa sababu zifuatazo:
. maandamano ya misri yalikuwa yanaongozwa na wananchi wa kati( middle class)
.maandamano ya cdm yanahusu vijana ambao hawajui watapata nini siku ya mwisho

Makupa, wewe ni rika gani? Je vijana hao hao wamepata na watapata nini katika ufisadi na usanii wa CCM? Usiwe mwoga mabadiliko muhimu. Wakikosea si tutawapigia kura ya hapana? Tujenge demokrasia ya dhati kwa hiyo hakuna sababu ya kuwaogopa wapinzani wa CCM. Wanawapigania wananchi siyo wapinzani wa wananchi. Remember, a lot more can be achieved for everybody in this country with even less resources. Suala ni kujipanga na kuwa na mikakati inayoeleweka na yenye malengo kwa mtazamo wa haki na kweli iliyotawaliwa na DEMOKRASIA ya kweli.
 
Nalichukia jeshi la polisi hvi mtatua mbaka lini IGP mwema mtatumaliza mbaka lini tumewakosea nini nyie polisi haki yetu ya msingi iko wapi eeh tunahaki kikatiba kufanya mikutano pamoja na maandamano bila kuasili msingi iliyo wekwa kama mungewaacha wamalize mkutano yao mngekosa nini sasa ona ujinga wenu heti jeshi la kisasa msababisha mauaji ya ndugu yangu mpiganaji mwezangu daudi mwangosi nakukumbuka punzika kwa amani manaharakati nakukumbuka usemi wako KILA MUDA NA SIKU WATENDAJI WA SERIKALI WANAOPOTEZA BILA KUTOA HUDUMA KWA MWAJILI WAO AMBAYE NI MWANACHII UTALEJESHWA MABADILIKO NI MHIMU WATAKE WASITAKE UMMA UTACHOKA. R.I.P DAUDI MWANGOSI
 
Nimekosa niandike nini,
Kwani najawa huzuni,

Kosa lipi la marehemu,
Hata atendewe kidhalimu?

Nyinyi ni usalama wa raia?
Katu sitowakubalia,

Nyinyi mbumbumbu wa demokrasia,
Nani sasa tutamtumainia?

Pole kwa wana mabadiliko.
Hakika haya yana kikomo.

Iliyomwagika yake damu,
Igeuke yetu kalamu,

Iandike yote maovu,
Yao hawa wapumbavu.



 
Hamna haja ya kukifuta, Wananchi wenyewe watakifuta kwa kuendeleza siasa za vurugu na kutaka nchi isitawalike.
 
mtanisamee kwa picha niliyoiweka
naandika haya nikiwa natokwa na machozi na siamini kama akili za binadamu zinaweza zikafanya unyama kiasi hiki...
naandika haya ili kila mwenye macho aone na ashuhudie mwenyewe unyama unaofanywa na polisi wetu..
naandika haya ili watoto wetu waone endapo na sisi tutauliwa basi wajue unyama huu ulianza toka zamani...
inaumaaa sanaa
inasikitisha sanaa
huu si ubinadamu..
haiingii akilini kumuuwa binadamu mwenzako kinyama kiasi hiki
ni kulipa kisasi??
maagizo???
au ujeuri???
waandishi wa habari...angalieni,tafakarini..watanzania angalieni tafakarini...
 
Mbona picha ya Slaa na wahuni wenzake haipo?
 
Wewe bahati mbaya gani umemwelekezea mtu bunduki?????????? angalia vzr wewe wawezaje mnyooshea mtu mshale then useme huwa unafyatuka haiitaji akili nyingi kutambua

Huwezi amini shetani anawafuasi kiasi gani mtu mzima na akili zake anasema ni bahati mbaya.....Juzi Morogoro walisema marehemu ameuawa kwa kitu chenye ncha kali..and here we go tuna uawa kama kuku vile.....Heeh! Hivi hii nchi ina viongozi ama ndiyo hivyo kila mtu anaweza fanya anavyotaka....Maisha ya mtu hayana replecement jamani hata ingekuwa vipi kwenye nchi inayojali uhai wa raia huyo askari asingekuwa na ujasiri wa kufanya ama hata kujaribu kufanya alilofanya! Mungu wangu hii hasira leo nisaidie mm moyo usinitoke!
 
yote hii ni dalili ya mabadiliko,sasa watanzania inatakiwa tuamke na wote tuungane katika vuguvugu la mabadiliko(m4c)

mungu ailaze mahala pema peponi roho ya marehemu mwangosi.amina
 
Mkutano mwingine ni zamu ya Slaa,haiwezekani asababishe yote haya halafu yeye anabaki pembeni wakati wananchi wanakufa. Huyu mzee anatakiwa apelekwe pale mnazi mmoja akachapwe viboko kama mtoto wa shule. Labda akili zitamrudi

Punguani wewe,tutakuanza wewe kwanza na hivyo viboko, onyesha sura yako sio una comment kwenye keyboard
 
zomba wakati mwingine ni vema ukakaa kimya! Wengine tunasikitishwa na hayo yanayofanywa na vyombo vya dola! Hebu zungumzia mauaji ya mwandishi wa habari Iringa. Mtu mwenye akili timamu utasema kweli kuwa ameuawa na chadema? Wakati mwingine tuache ushabiki wa kisiasa na tukemee maovu dhidi ya raia.

Serious huyu jamaa hana akili hata kidogo, coz anachafuwa watu humu ndani, watu wapo kwenye majonzi yeye analeta mambo yake yakijinga hapa.....Stupid....
 
K........mamake yaani propaganda hadi kwenye haki za msingi za watu.Yaani mnaua makusudi tu halafu mnaleta propaganda kweli hii nchi tume
jaaliwa upole na utulivu tu sababu kitu amani hamna ukisema TZ kuna amani na Botswana,Ghana,Mauritius,Malawi utasema kuna nini.RIP kaka Daudi Mwangosi!
 
Mkuu,nilishawi kutoa ushauri hapa JF wa kumsaidia yule babu kupima afya ya kichwa wafuasi wake watiifu wakatukana.

mingoi, picha unayotumia inafanana na vazi la kichungaji...kauli unazotoa ni za kishetani...una agenda ya kudhalilisha ukristo?
siku zote anayeuawa huonekana kuwa mwovu kwa yule anayeua...wayahudi walimwona yesu kuwa mwovu wakamuua...kwako wewe na wenzako kila anayeunga mkono chadema anastahili kifo au kipigo. kumbuka kuwa sio kila kinachoitwa haki ni haki kweli na sio kila kinachoitwa utii wa sheria ni utii wa sheria. nawaonea huruma polisi kwa sababu kazi yao haiwapi nafasi ya kuhoji amri wanazopewa na wakuu wao.
 
Wadau wa siasa hivi jamani haya mauaji kwenye mikutano ya CDM mpaka lini? Hivi visingizio vya mazuio je ni halali kwa police kuhukumu raia kwa kuua?. Haijalishi ni kosa gani, police hawapaswi kuwa mahakama ya maandamano na mikutano ya vyama vya siasa. hawa wananchi hawajaua wala kujeruhi. yani mbinu zote za kuzuia maandamano pia hawana isipokuwa kuua. I think there is something need to be done to show that pple are conscious of their rights.
 
Polisi wa Tanzania chini ya uongozi wa kikwete wamekuwa ni ma vampire, wanaitamani sana damu yetu, badala ya kutulinda wanatuangamiza.
Wadau wa siasa hivi jamani haya mauaji kwenye mikutano ya CDM mpaka lini? Hivi visingizio vya mazuio je ni halali kwa police kuhukumu raia kwa kuua?. Haijalishi ni kosa gani, police hawapaswi kuwa mahakama ya maandamano na mikutano ya vyama vya siasa. hawa wananchi hawajaua wala kujeruhi. yani mbinu zote za kuzuia maandamano pia hawana isipokuwa kuua. I think there is something need to be done to show that pple are conscious of their rights.
 
Wadau wa siasa hivi jamani haya mauaji kwenye mikutano ya CDM mpaka lini? Hivi visingizio vya mazuio je ni halali kwa police kuhukumu raia kwa kuua?. Haijalishi ni kosa gani, police hawapaswi kuwa mahakama ya maandamano na mikutano ya vyama vya siasa. hawa wananchi hawajaua wala kujeruhi. yani mbinu zote za kuzuia maandamano pia hawana isipokuwa kuua. I think there is something need to be done to show that pple are conscious of their rights.

dawa ya moto ni moto kuanzia sasa polisi wameshatangaza kuwa kwenye mikutano ya kisiasa ni eneo la hatari kwahiyo kila raia abebe silaha yake kibindoni yeyote atakayenyanyua silaha kutaka kukudhuru basi akikisha umpi nafasi ya kukudhuru. polisi atakayenyanyua bunduki yake kuku shoot akikisha unamwahi yeye in what so called selfdefence.
 
Hapan ukifanya hivyo utakuwa huna tofauti nao. Haya yote iko siku yataisha tu. Watanganyika tumlilie Mungu. Mie kwanza sidhaani CCM imewatuma kuua watu. Ni wao tu!! Na Mungu atashughulika nao siku moja. Tukianza kufanya unavyosema Mungu atatuacha na itakuwa hatari zaidi. Wao wana live ammunition. Kwani hujasikia kilichotokea afrika kusini! Polisi wameua wachimba migodi 40 halafu wenzao wameshtakiwa kwa kuua wakati walioua ni polisi!! Ila jana wamefutiwa mashtaka baada ya watu kupiga kelele sana. Wachimba migodi wale walikuwa na silaha za jadi na polisi wakawamiminia risasi. Usihamasishe hivyo kwani itakuwa hatari sana.
dawa ya moto ni moto kuanzia sasa polisi wameshatangaza kuwa kwenye mikutano ya kisiasa ni eneo la hatari kwahiyo kila raia abebe silaha yake kibindoni yeyote atakayenyanyua silaha kutaka kukudhuru basi akikisha umpi nafasi ya kukudhuru. polisi atakayenyanyua bunduki yake kuku shoot akikisha unamwahi yeye in what so called selfdefence.
 
is soo sad,huo uzi nanadhani upo na umeandikwa POLISI WAJIANDAA KUUA IRINGA

Kwa kuwa polisi ni binadam na wanaishi ndani ya jamii na sisi. Kuna taarifa zisizorasimi kutoka kwa baadhi ya watumishi wa jeshi la polisi ambao ni wapinzani wa mauaji haya (japo maadili hayawarusu kuvujisha taarifa za kazi zao) kuwa polisi walipata maagizo ya kuua kutoka juu, na wakubwa wao pale mkoani wakajigamba wenyewe watajibia mauji. na ndivyo walivofanya hata Songea kipindi cha nyuma. kwa hiyo ukiunganisha taarifa hii na thread hiyo hapo juu unapata wanachofanya polisi wetu. But all in all polisi kutekeleza kila agizo kutoka juu ni udhaifu pia wa jeshi letu la polisi. Tuendelee kutafiti ili tujue ukweli zaidi.
 
Back
Top Bottom