Isabella Mwampamba, mgonjwa wa kwanza kugundulika Corona Tanzania aomba msamaha kwa Watanzania

Isabella Mwampamba, mgonjwa wa kwanza kugundulika Corona Tanzania aomba msamaha kwa Watanzania

Je kuna uwezekano wa kuwa makini na serious na maisha ya watanzania bila kuingiza siasa katika nchi yetu? Huyo Polepole alisikika akisema kuwa CCM inaacha mikutano ya kisiasa halafu baadaye akaendelea kuwananga CHADEMA au Mbowe kuwa hicho chama au kiongozi wake anataka kufanya mikutano wakati kuna magonjwa, Je haitoshi tu kusema sisi CCM tumefuta mikutano yetu...kwani lazima aisemee chama kingine? Hicho chama nao kwa muda wao si watatangaza updates zao?

Tuache hayo ya siasa za kijinga kwenye mambo ya muhimu. Nimeona wakati huyo waziri wa Afya, Ummy Mwalimu akitangaza kuhusu mgonjwa wa CORONA, mbona alikuwa anacheka? Kulikuwa na jambo gani la kuchekesha? Niliona tofauti kidogo wakati Donald Trump, Boris Johnson, Trudeu wa Canada, Scott Morrison wa Australia, Kenyatta wa Kenya na wengine wengi wakitangaza hilo janga kwenye mataifa yao na jinsi ya kukabiliana na janga hilo, wengine walienda mbali zaidi wakasema na kiasi walichopanga kutumia kumaliza hilo janga na kujikinga na maambukizi zaidi.
Kwetu hatukumuona rais akitangaza hili janga na mikakati ya kuzuia na kutibu badala tunamuona waziri wa Afya ambaye alituambia kabla kuwa likitokea janga kama nchi hatuna la kufanya bali tuombe Mungu, lakini akasema kwenye prevention kwenye viwanja vya kuingilia nchini tumejiandaa na tupo vizuri sana.

Sarakasi ya kwanza, Mgonjwa wa kwanza aliyepatikana.....Maelezo yake hayaeleweki vizuri kiasi kwamba dots haziunganiki. Alipita pale KIA halafu zile temperature scanners zikashindwa kumgundua hadi akaenda mwenyewe kwenye self isolation.....Ilikuwaje wakashindwa kumtambua na tulijiandaa vizuri?

Sarakasi ya Pili, Tumemsikia mgonjwa akiomba msamaha kwa waziri na kwa watanzania kwa sababu ndiye kaleta ugonjwa huu hapa nchini....SIJAELEWA, kwani ameuletaje? Yeye si mgonjwa mwenyewe na hakuna ushahidi wa mtu mwingine aliye karibu yake ambaye ni mgonjwa? Sasa ameletaje ugonjwa wakati mgonjwa ni yeye pekee?

Sarakasi ya Tatu, Anawaomba msamaha watanzania....Kwa kosa gani? Yeye ndiye alitakiwa apewe pole kwa kuugua! Mbona inakuwa vice versa? Hiyo press conference ya waziri kuunganishwa na huyo mgonjwa ilikuwa na nia gani? Mwenye kujua labda atueleze, sijaona protocol kama hiyo duniani, mgonjwa anawekwa kwenye simu akiomba msamaha.

Sarakasi ya Nne, Waziri anatuambia kuwa huu ugonjwa umekuwa imported hapa nchini......Kwani hakuna asiyejua kuwa umeanzia China? Kulikuwa na umuhimu wa kusema ulikoanzia? isitoshe alisema kwa vile umekuwa imported itakuwa rahisi kuudhibiti.....Hapo hakuna ukweli kote duniani isipokuwa China huu ugonjwa umesambaa(imported kama alilvyosema waziri) mbona unaua kwa rate kubwa kuliko hata ulipolipo-lipukia?

Kulikuwa na taarifa kuwa kuna watu zaidi ya mmoja waliokuwa wakiugua ingawa hizi taarifa zilikuwa zikikanushwa na vyombo vya serikali ingawa kulikuwa na rumors kuwa namba ni kubwa, kwanini pia rais asitangaze kuwa hilo ni janga la kitaifa kama walivyofanya marais wengine badala yake anamwachia waziri asiye kuwa serious?

Hili janga ni kubwa juzi alikuwa mtu mmoja, jana wawili, leo watatu wapya .....na kama kawaida walihusishwa na kutoka nje ya nchi (Ni sawa lakini) waliopata hapa ndani ni wangapi na je kulikuwa na haja waziri kusema hizo cases zimekuwa imported...kuna lililojificha ndani ya hiyo statement?

Leo tumeambiwa sita, na tatizo la ugonjwa huu unasamba exponentially, juzi, mtu mmoja, jana wawili wapya, leo watatu wapya (wote wana historia ya kusafiri) je wagonjwa walioambukizwa ndani wapo wangapi? hatujui kesho watakuwa wangapi.

Serikali yetu inahitaji kuwekeza nguvu za kutosha ili kupunguza au kuzuia kabisa maambukizi. Wamachinga waondoke mitaani wafanye kazi zao kwa utaratibu, sheria ziwekwe na zifuatwe na kila mmoja wetu. Serikali iwe wazi isifichefiche.Hili ni janga (Pandemic) la dunia nzima.

Samahani kichwa cha habari kilipaswa kuwa:
Kwanini mambo ya Ugonjwa yanachanganywa na siasa, Je kulikuwa na umuhimu wa mgonjwa wa CORONA kuomba MSAMAHA?
 
Huyu mgonjwa anataka kick kwa kutumia ugonjwa hakuwa na haja ya kufanya press conference halafu anasema Yuko tayari kufanya kampeni ya Corona amefanya ujinga halafu anataka kutufanya wajinga
 
Zamani sana utamuona kwenye matangazo ya sabuni na kiwi.
Kabisa yaani, kama aliyevunja Sheria na kuingia kiwanjani kumshika mkono mcheza kawa hivyo huyu atakuwaje, nachukizwa na hili neno hata kuliandika sitaki waandishi wanalitumia vibaya sana maana wao ndio wanaokuza.mambo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua tunapishana wp mm na ww?tunapishana pale ww unaposema asilaumiwe,lazima tumlaumu kwa yy kujua ana Hilo tatizo na kuja kufanya makusudi,ndiyo mm naita makusudi maana alojua na ndiyo maana akachukua tax kwenda kujifungua hotelini,tusiongee kwa ushabiki bali reality ingekuwa nduguyako anafanya kazi Ile hoteli u gejisikiaje? Pia bila kujali ugonjwa no hatari ama laa tahadhari ni muhimi jamanii

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua tunapishana wp mm na ww?tunapishana pale ww unaposema asilaumiwe,lazima tumlaumu kwa yy kujua ana Hilo tatizo na kuja kufanya makusudi,ndiyo mm naita makusudi maana alojua na ndiyo maana akachukua tax kwenda kujifungua hotelini,tusiongee kwa ushabiki bali reality ingekuwa nduguyako anafanya kazi Ile hoteli u gejisikiaje? Pia bila kujali ugonjwa no hatari ama laa tahadhari ni muhimi jamanii

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu mama ni muuaji kama wauaji wengine, nashangaa wanamnyenyekea, kwa makusudi mazima aliamua kuuleta Tanzania waathirike wengine Ila sio familia yake,

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Politics is top of all other games. Ila hili gonjwa linabaki kuwa mafua pekee na kwa mwafrika haijawahi kuwa akafa kwa mafua. Kuku wa chienyeji maradhi mengine hayampati ila kwa hawa mabroiler unakuta kuna store ya dawa utafikiri pharmacy. Mnenielewa sijui
 
Aisee!
Hili tukio nimelichukulia kama ile press ya kutekwa Mo ambayo kama tunavyokumbuka Mh. rais aliishia kucomment kuwa "msidhani watz ni wajinga". Kiuhalisia hii ndio hali tuliopo kwa sasa na tunabakia kumtegemea Mungu huku tukisahau Italy ambako ndiko makao makuu ya Kanisa wana hali mbaya!

Kumkumbusha tu wazri, bofya hapa>>> Africa Live: WHO warns Africa to 'prepare for the worst'
Umesema ukweli.
 
Back
Top Bottom