Mzee hebu tuassume kuwa sijasoma kitabu chako
Halafu ninakuuliza maswali ambayo wewe ndie mwenye kitabu na hayo maswali ninayokuuliza majibu yake unayo na pia yapo kwenye kitabu chako
Sasa kama majibu yake yapo kwenye kitabu hii maana yake majibu yako unayo wewe
Kujibu kwako maswali yangu hapa kutaonesha kuwa kile ni kitabu makini na kinatoka kwa mtu makini
Lakini unaposhindwa au kuacha kujibu eti hadi nikisome ndipo nipate majibu utakuwa unafanya mchezo wa kitoto
Ni mchezo wa kitoto kwa kuwa kama wewe ndie mwandishi wa kitabu na unauhakika kuna majibu nikitu gani kinakufanya usinijibu maswali yangu sasa?
Huwezi kuona kuwa kujibu kwako maswali yangu nitajua kuwa kuwa huenda kwenye kitabu chako kuna majibu ya baadhi ta maswali yangu na ukanihamasisha kukisoma?
Lakini kama hutaki kunijibu maswali yangu hapa itaonesha mambo mawili
1:Huyu mtu hana majibu
2:Huenda ni mbabaishaji tu
Sasa kama ni hivyo huoni kuwa sitakuwa na sababu ya kukisoma kitabu chako?
Hakutakuwa na sababu kwa kuwa mwandishi wa kitabu hicho ambae ni wewe umeshindwa kujibu maswali ambayo ni simpo sana je kwenye kitabu chako kutakuwa na mpya gani?
Nitakitafuta kitabu chako kwa sababu gani hasa?
Eiyer,
Huenda mie sikukuelewa.
Mimi nilidhani wewe ni mtu hujui sasa unauliza ili upate kujua.
Ndiyo sababu nikakuelekeza ukasome kitabu.
Ingekuwa umesoma kitabu usingeniuliza vipi Nyerere aliingia katika ule mkole
wakati ulikuwa haumuhusu ndewe wala sikio.
Lakini sasa ndiyo natambua kuwa wewe uko hapa kutaka kubishana.
Ikiwa kubishana samahani mimi si mtu wa hivyo.
Niko hapa kueleza kile ambacho hakikuwa kinajulikana.
Unaweza kuniita majina uyapendayo.
Hapana neno.
Hayo ni ya kawaida hapa jamvini.
Hilo la kusoma au kutosoma kitabu changu kwa hapa kitabu kilipofika kwa hakika
si kitu muhimu sana kwangu.
Uamuzi ni wako.
Ni sawa na sheria za afya.
Ukijiweka msafi hutopata maradhi.
Ukijiachia uwe mchafu kitakachokupata unakifahamu.
Ukisoma kitabu changu utaongeza elimu na kujuwa kwako hata kama hukubaliani
na yale niliyoandika.
Sasa usome au usisome kitabu changu kwangu mimi yote ni mamoja.
Nataka nikupe mfano mdogo sana.
Kuna mtu alipata mshtuko wa moyo kusikia kuwa nimesema Abdu Sykes alizungumza
na Chief Kidaha kuhusu kuunda TANU 1950.
Huyu bwana yeye akiamini kuwa TANU alikujanayo Nyerere 1954.
Mimi jibu langu kwake lilikuwa huenda Nyerere hakuwa anajua kuwa Abdu na Chief Kidaha
walikuwa wakishauriana kuhusu TANU kuanzia 1950 hadi 1953.
Huyu ndugu yangu alipomaliza kusoma kitabu changu alinitafuta...
Alinipongeza.
Eiyer,
Uamuzi ni wako.
Wewe ni mtu huru una hakl ya kuamini ukipendacho.