Ismael Jussa amesema kuwa Nyerere ndiye aliyemuua Abeid Karume, yana ukweli haya? Na kama siyo mbona bado anazunguka mitaani, akamatwe

Ismael Jussa amesema kuwa Nyerere ndiye aliyemuua Abeid Karume, yana ukweli haya? Na kama siyo mbona bado anazunguka mitaani, akamatwe

Nimewahi kusikiliza online TV inaitwa Zanzibar Kamili, kuna mahojiano ya huyo anayeitwa Ismael Jussa ( Nadhani nimetaja jina lake la pili vizuri), huyo Jussa wakati akifanya uchambuzi wa vitabu, kuna sehamu amesema kuwa Nyerere alikuwa anawakandamiza viongozi wa ZNZ kuanzia wakati wa vuguvugu la Jumbe, Salmin Amour, na wengine, halafu akarejea kuwa pia alihusika wakati wa mapinduzi na wakati wa mauaji ya Karume.

Ninavyoelewa Karume aliuawa na Kanali Humudi na sababu wanazijua fika, kusema Nyerere kahusika ili aendelee kuinyonya ZNZ inahitaji ushahidi ambao kimsingi huyo Jussa na hiyo TV Kamili ya ZNZ wanapaswa kuuleta.

Kuna mengi yanaongewa ambayo yametiwa chumvi na hilo kundi la Jussa na wenzake akiwemo yule anayeitwa OMO, badala ya kufanya kazi ya kuijenga nchi ya Zinjibari anazunguka huko na huko kuichafua Serikali na Rais wa ZNZ.

Kuna kipindi kimoja Jussa alikaririwa akisema kuwa Waarabu hawakuhusika na biashara ya watumwa, akawatupia lawama wananchi Waafrika weusi, aka-justify kuwa Zanzibar ilikaliwa kwanza na Waarabu....yaani ndiyo first people. Wengine wote, yaani Waafrika weusi walikuja kutoka Bara na kuwa huwezi kutenganisha ZNZ na Uislaam, yaani Serikali na dini ni kitu kimoja....Ni ya kweli hayo?

Eti kuna mtu mweusi alikuwa akimiliki watumwa ndiyo moja ya justification kwamba kila mtu alihusika na biashara ya utumwa, lakini akikataa kuwa waarabu siyo wahusika...atuthibitishie hayo.

Lingine alisema kuwa Waingereza walishindwa kwenye vita vya SUEZ CANAL na misri ndiyo maana walikuwa na hasira na ZNZ, Wakati kila mtu anajua kuwa Egypt ilipigwa na mfereji ukafunguliwa kwa meli zote zipite hapo hadi leo hakuna anayethubutu kuufunga tena....Hata hajui hiyo ilikuwa ile vita iliyoitwa " Six day war" au Yom Kippur. Kwanini anatudanganya?

Kuna mengi ambayo anahitaji kuthibitisha....mpelekeni polisi akathibitishe, ila safari hii msimvunje miguu tena.
Kwanini mnaruhusu non-credible sources of information katika nchi hii iendelee kueneza uongo wa mtu mmoja au wawili wajinga
 
Wanasema Karume alitaka kuvunja Muungano-
1.Mchonga alimula kichwa Karume
2.Anco Ben akamula kichwa Mchonga
3.Dr.Omary Juma akaliwa kichwa na Boys II men
4.Jiwe akamula kichwa Anco Ben
5.Jiwe akaliwa kichwa na Msoga boy

Zote ni propaganda but inakupaswa uamini natural death kwa viongozi duniani kote 1%,percent zinazobaki huwa ni assassination.
 
Haya tuhusu sisi tunataka muungano fake huu uvunjwe haraka
Nani atauvunja? Hiyo ndiyo ile wishful thinking....haitakusaidia utapata presha bure kaka wewe katafute kazi siyo kushinda kwenye Jamii forum ukitegemea watakusaidia kuvunja muungano. Pia ukiendelea kuwasikiliza hao wanaokupa moyo hivyo utawehuka.
 
Inategemeana kama upande huu mwingine utakubali, kitu ambacho ni ndoto. Hata huko wanakopiga kelele, wakiweza sana ni asilimia 55, kama kura ya maoni ya kutaka kujitenga ni asilimia 95, mtaifikia hiyo kaka? Siyo rahisi kama kutaliki mke huko uswahilini.
Hebu ipitiahwe kwanza ndio tujue itafikiwa ama la
 
Yes inawezekana ni ukoloni kama unavyofikiri, nyiye mmeshadanganywa sana na Maalim Seif, Jussa na huyo domo mwingine OMO kuwa tunapata mamlaka kamili...Angalieni articles za muungano ulikuwa ukisema nini? Muungano siyo ndoa kama za huko kwenu unataliki asubuhi jioni una mke mwingine., Muungano unaangalia maslahi mapana ya walioungana. Huwezi kuamka asubuhi na kuanza kupiga makelele misikitini kuwa tunataka Zanzibar kamili, mbona hao wanaowaambia hawawezi kuwapa mamlaka kamili? Ndio maana nasema shule kwenu ni tatizo, mna midomo tu lakini vichwani mpo bwerere...hamna kitu, maboga tu.
Kuna makubaliano yaliyofanyika mwaka 1964, na anayevunja anatakiwa awe upande wa hasara....Ndiyo maana ya "binding agreement" Najua articles za muungano, lakini mpo tayari kupoteza kama articles za muungano zinavyosema? Ndiyo maana nakuelewesha kuwa usidhani muungano ni kama wanawake mnaowaoa huko wa kuwaacha asubuhi na kuoa tena jioni, hapa unaongelea maslahi ya nchi ambayo kwanza kujaribu kuyapinga ni kosa kubwa. HIYO NI TREASON, na unajua adhabu za treason case ni nini?
Mmedanganywa na mnaendelea kudanganywa na huyo OMO, Jussa na marehemu Maalim. Angalia historia ya nchi au sehemu zilizotaka kujitenga, mfano Marekani hadi kusababisha Civil war (Southerners walitaka kujitenga kupinga biashara ya utumwa kusitishwa).

Hao wanaowadanganya, hawawasaidii, masharti ya kuvunja miungano ni migumu, imefanyika kila mahali lakini imeshindwa.....Kuanzia USA, UK, Spain nk. Hivi ukiambiwa kuwa ili kuvunja muungano kunatakiwa kuwa na kura ya maoni ya asilimia 99.9...mtaipata hiyo? Ebu nenda kalale wewe, uamke kesho asubuhi ukatafute kazi...angalau itakusaidia kuliko kuwa na "wishful thinking".

Kama Marekani imeshindwa kuikalia Afghanistan ikafunga virago na kuondoka baada ya miaka 20, nyie machogo mtaweza kubaki Zanzibar?
 
Elimu yenu bado ndogo sana, Sultani yaani achukue eneo letu kwa mkataba gani? Kumbe ndivyo mnavyodanganywa...Duuh kweli bado mpo nyuma sana. Sultani wa wapi wewe Samaki wa urembo? Halafu kuhusu ziwa Nyasa kwa taarifa yako ile mipaka ilikuwa ikifahamika na pia kuna taratibu za mipaka kwenye sehemu za maji (waterbodies) aidha ziwa na mito, sheria inasema inakatisha maji si lazima ziwe kati kwa kati inaweza kuwa sehemu ndogo ya ziwa. Kwa taarifa yako sehemu yetu ya ziwa Nyasa meli za hao unaowasema huwa hazikanyagi hapo. Na miji ya Mbamba bay ipo ziwani na mingineo. Kwa hiyo jipe moyo na endelea kusikiliza uongo.
Mjeruman uingereza walikubaliana mpaka uwe kwenye ukingo wa ziwa nyasa upande wa tanganyka ushaidi upo
Screenshot_20220613-193741.jpg
 
Elimu yenu bado ndogo sana, Sultani yaani achukue eneo letu kwa mkataba gani? Kumbe ndivyo mnavyodanganywa...Duuh kweli bado mpo nyuma sana. Sultani wa wapi wewe Samaki wa urembo? Halafu kuhusu ziwa Nyasa kwa taarifa yako ile mipaka ilikuwa ikifahamika na pia kuna taratibu za mipaka kwenye sehemu za maji (waterbodies) aidha ziwa na mito, sheria inasema inakatisha maji si lazima ziwe kati kwa kati inaweza kuwa sehemu ndogo ya ziwa. Kwa taarifa yako sehemu yetu ya ziwa Nyasa meli za hao unaowasema huwa hazikanyagi hapo. Na miji ya Mbamba bay ipo ziwani na mingineo. Kwa hiyo jipe moyo na endelea kusikiliza uongo.
Sultan alipewa km 10 kuja bara siku zanzibar tukiwa huru tutachukua kigambon yetu mkataba upo ndio maana mnatupiga mbinyoooo ili tusiwe huru mikataba ipo
Screenshot_20220613-192634.jpg
 
Hata akileta ushahidi nyerere ameshakufa sasa atafanywa nini?
Karume pia kafa saa hizi wanadaiana huko kama ni kweli🤣
Nashauri tuendelee kutafuta hela mengine tuwaachie wenyewe
 
Kabla ya biashara ya Utumwa kulikuwa na biashara iliyoanzishwa huko China ya kuuza na kununua vitu
Ilikuwa inaitwa SILK ROAD ilianza 130 BC
(Mwaka 624) kama Niko sawa na baadae Wa Misri nao walikuja na kufanya biashara ya kununua vitu huku wengi wakinunua Meno ya Tembo mpaka wachina wamebeba sana miaka ileeee
Na watumwa ilikuwa biashara tu

Waarabu wamekuja baadae kidogo na kuendeleza biashara zote hizo
Miaka ya 1700 Mbona juzi tu ukilinganisha na Silk Road ?

IMG_7007.jpg

IMG_7006.jpg
 
Wachina wasembe sanaa mbona hawakuwapelekea moto bibi zetu watuachie mbegu zao
 
Kumsingizia marehemu mambo mabaya, kunapelekea kupata karma mbaya. Karume aliuliwa na Humudi, kisa cha Humudi kufanya mauaji hayo kinafahamika, unless ni mseme by that time intels zote za Zanzibar zilikuwa zinasimamiwa na TISS ya Bara na TISS walijua kila kitu na Nyerere was informed kuhusu mipango hiyo but he did nothing kuzuia, hilo linafikirika!, ila kwenye usalama wa nchi, kiongozi mkubwa akitoa kauli hatarishi kwa muungano wetu adhimu, by then even to think tuu kuwa muungano wetu adhimu unaweza kuvunjika ni uhaini tosha!, hivyo ukisikia mipango ya kumu eliminate mtu mwenye fikra ya uhaini dhidi ya uwepo wa JMT, na hukuzuia such elimination, then huko kutahesabika ni part and parcel ya kuulinda muungano. Ukisikia kuwa "tutaulinda muungano kwa gharama yoyote", kiusalama gharama hizo zinaweza kuwa ni pamoja na machozi, jasho na damu.
Katika kuulinda muungano, wengi wamegharimika akiwemo Abdul Jumbe.
P

Mkuu Pascal kwanini unapenda kuzirusha akili muda mwengine? Mauji ya Karume yalitokana na jaribio la Revolution kutoka Umma Party, Na Nyerere alikua ana majasusi ndani ya hilo kundi wakiwemo akina Canal Ali Mahfoudh na Salim A. Salim, Kwahiyo alijua kila kilichokua kinaendelea from day One.

Jaribu kufatilia kwa ukaribu lile tukio utugundua Connection ya Mwalimu moja kwa moja ndani yake.
 
Mambo mengine ni watu wa intelligence ndio wanayajua sisi watu wa kawaida hayo tutayajuaje, tunachojua ni mauaji ya Karume ni visasi, mmatumbi alitaka kumtwaa dada wa Humudi awe mkewe, Baba wa binti akagoma, Mzee mzima akaingia front, ikapigwa action fulani huku Humudi akishuhudia, akajiapiza atalipiza kisasi, akajinga jeshi, muda muafaka akatimiza lengo.
Hayo mengine hatuyajui!.
P
 
Usipende kusikiliza vichaa, nawe utageuka kichaa. Ni hayo tuu
Nyinyi ni watoto katika kesi ya uhaini ya waliomuuwa Karume Nyerere akiitwa Mr X , alihusika katika mpango wa mauwaji sio Siri , jaribu kumuuliza Bibi yako atakuambia
 
Mkuu field marshall1 , it's good ungeleta links, tukamsikia na sio hii hearsay uliyoleta. Hongera JF kwa Whistleblow, JF tubadilike, tusichafue majina ya Watu kwa tuhuma za Hearsay zisizo na Uthibitisho, Ukituhumu, Weka Uthibitisho

Kuna ukweli kwenye hili, biashara ya utumwa ilikuwa na stages 3.
1. Wakamata watumwa, hawa hawakuwa Waarabu, hawa walikuwa wenyeji na machifu wetu, waliwakamata watu, miongoni mwao wahalifu na mateka, na kuwauzia Waarabu akina Tippu Tip ambao hao waliwanunua watumwa toka kwa wenyeji na kuwasafirisha mpaka soko la Bagamoyo kisha kupelekwa soko Kuu la Zanzibar.
2. Wachuuzi wa watumwa, hawa ndio Waarabu, waliwanunua Watumwa kwa wenyeji na kuwasafirisha hadi soko la Bagamoyo kisha kupelekwa soko kuu la Zanzibar.
3. Wanunuzi wakubwa wa watumwa, hawa pia sio Waarabu, ni Wahindi, Waarabu na Wazungu, waliokuja soko la Zanzibar na meli kubwa, kuwanunua watumwa na kwenda kuwauza masoko ya Europe, India na Arabia.

Hii sii kweli, Wenyeji halisi wa asili wa Zanzibar ni Wahadimu ambao asili yao ni huku bara, kiongozi wao aliitwa Mwinyi Mkuu. Wareno walivamia Zanzibar, hivyo Mwinyimkuu akaomba usaidizi wa Waarabu kuwapiga Wareno, baada ya kuwashinda Wareno, ndipo mwaka 1732 Sultan Seyyid Said, akahamishia makao makuu ya Sultanate yake from Oman to Zanzibar na kuvitwaa visiwa hivyo as if wameviokota, sijui walimfanya nini Mwinyimkuu, ila mwaka 1964 wajukuu wa Mwinyimkuu walilipiza kisasi na kuvirejesha visiwa hivyo kwa wenyewe kupitia yale Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

It's true, huwezi kutenganisha Zanzibar na Uislamu kwasababu ya Waarabu, baada ya Sultanate ya Oman kuhamia Zanzibar, Zanzibar iliyokuwa ni Islamic nation. Ni muungano wetu ndio umeifanya Zanzibar kuwa a secular state.

It's very true kuna watu wetu wakaichangamkia biashara hii akiwemo Tippu Tip, Baba Mwarabu na mama Mnyamwezi.QAaa

Anza na kutuletea huo ushahidi humu, tuna wataalamu wa kutosha wa ku ascertain criminal liabilities, tutashauri, na tuliwahi kushauri humu, kama tuhuma zozote zenye criminal liabilities, ukileta tuhuma humu lazima ulete ushahidi, ukileta tuhuma humu bila ushahidi, usitaje majina na kuchafua watu bure bila ushahidi. Hongera JF kwa Whistleblow, JF tubadilike, tusichafue majina ya Watu kwa tuhuma za Hearsay zisizo na Uthibitisho, Ukituhumu, Weka Uthibitisho
P

Pascal umeandika wahadimu asili yao ni bara, unaweza kutuambia ni kabila lipi bara ni wahadimuu?
 
Kumsingizia marehemu mambo mabaya, kunapelekea kupata karma mbaya. Karume aliuliwa na Humudi, kisa cha Humudi kufanya mauaji hayo kinafahamika, unless ni mseme by that time intels zote za Zanzibar zilikuwa zinasimamiwa na TISS ya Bara na TISS walijua kila kitu na Nyerere was informed kuhusu mipango hiyo but he did nothing kuzuia, hilo linafikirika!, ila kwenye usalama wa nchi, kiongozi mkubwa akitoa kauli hatarishi kwa muungano wetu adhimu, by then even to think tuu kuwa muungano wetu adhimu unaweza kuvunjika ni uhaini tosha!, hivyo ukisikia mipango ya kumu eliminate mtu mwenye fikra ya uhaini dhidi ya uwepo wa JMT, na hukuzuia such elimination, then huko kutahesabika ni part and parcel ya kuulinda muungano. Ukisikia kuwa "tutaulinda muungano kwa gharama yoyote", kiusalama gharama hizo zinaweza kuwa ni pamoja na machozi, jasho na damu.
Katika kuulinda muungano, wengi wamegharimika akiwemo Abdul Jumbe.
P
Mkuu pascal mayalla nlikuwa nakuheshimu sana na kukufuatilia contents zako ila kwa hili umeniacha hoi.umeshindwa nini kusema tu mwalimu alihusika kwa asilimia zote ???? Hadi unazunguka zunguka.???.......comment yako ina double standards mzeee.kama teacher alijua kinachoenda kwann alipiga kimya.??? Nyie watu wabara mbona sio wa kweli.....mwenzenu kamla kichwa karume .full stop. Acheni kuficha ficha mambo dunia nzima inajua labda nyie tu ndio mnaona kitu cha uongo..........

Na huyo teacher ni maagizo kutoka mbele.

Kuhusu suala la waarabu na biashara ya utumwa sio kweli.ni kichaka cha kujifichia na kuwalinda wazungu.waarabu walijiingiza pwani huku kufanya biashara ila lengo lao kubwa ni kusambaza elimu .ndio maana athari ya elimu ya dini ya kiislamu ni kubwa kwa miji ya pwani ni kubwa kuliko mbeya na iringa.

Sent from my vivo 1907 using JamiiForums mobile app
 
Nyinyi ni watoto katika kesi ya uhaini ya waliomuuwa Karume Nyerere akiitwa Mr X , alihusika katika mpango wa mauwaji sio Siri , jaribu kumuuliza Bibi yako atakuambia

Kwenye Siasa shutuma za maauji hata wewe ukiingia utapewa.

Kuendekeza wapumbavu ni upumbavu, sasa Kama Nyerere ndio nafanya hayo Sisi tufanyaje?
 
Back
Top Bottom