Mkuu Nguruvi3: Gaza inafanywa magofu....Hiyo Nguvu ya Iran iko wapi? Unasema Israel bila US haiwezi kusimama, Je Hamas bila msaada wa Iran inaweza kusimama....Nguruvi3 I always respect the way put your arguments kwenye mada nyingine, hili limekushinda!.
Kuna nyakati kuna mijadila isiyofurahisha 'uncomfortable' , ni lazima.
Kwa wengine ukweli unatuongoza si mihemuko ya kipuuzi kama ya udini.
Tunafuatilia habari hizi kwa undani kutoka vyanzo tofauti hivyo perspective yangu na yako ni tofauti.
We can agree to disagree lakini hatuwezi kuwa na disputes katika facts.
Ni kweli mabomu yaliyopigwa Gaza yameiguza magofu. Hii wanaita 'indiscrimite bombing' wakitumia mabomu yanayoitwa 'dumb bomb' waliyopewa na Marekani. Upo Mkataba wa kimataifa wa kutoyatumia kwasababu hayana 'precision' lakini Israel inayatumia ''with impunity'' kama unanielewa.
Marekani inakingia kifua Israel kwa namna zote, UN kwa kura ya Veto, Intelejensia na silaha vitani .
Katika 'war room' mipango ni CIA na Pentagon kwa kushirikiana na IDF na MOSAD
Ikiwa Israel ina nguvu za kijeshi na kiintelejensia kama tunavyoaminishwa, Marekani inafanya nini katika War room?
Tofautisha kati ya Hamas na Hezbollah. Pili, Gaza ipo chini ya Israel hakuna kinachoingia au kutoka bila Israel kujua.
Mabomu ya Hamas ni 'local made' ndiyo maana haya 'precision'.
Influence ya Iran kwa Hamas ni kupitia Hezbollah, hakuna msaada wa moja kwa moja kama ilivyo Israel kwa USA
USA ina Fleet Carriers mbili katika Bahari ya Mediterranean pwani ya Israel.
Meli zinatoa msaada wa intelejensia na vifaa kwa Israel. Inatosha kusema ni '' Marekani Vs Hamas '' kupitia Israel
Kwasasa kuna vita kaskazini kati ya Hezbollah na Israel. Hezebollah wanatumia zana kutoka Iran na zina precision ya hali ya juu, Israel imekiri.
Kwamba wiki kadhaa wameweza kupiga vituo vya mawasiliano vya Israel kwa uhakika wakikwepa ' Iron dome' inayotumika kuzuia makombora ya Hamas ya Katush. Wameingiza drone na zimerudi kutoka Israel
Tishio la Hezbollah limelazimu Israel kuita askari 350,000 wa akiba. Fikiri kwamba hili ni Taifa linalosadikika kuwa na nguvu na vifaa . Hii ina maana hali si njema na wanahofia mzozo ukisambaa Iran ikaingia Israel ina wakati mgumu . Wataweza kusaidiwa na Marekani lakini wenyewe hawawezi kusimama kidete na Iran
Eneo la Israel ni sababu nyingine ya kuwafanya wawe Vulnerable. Sijui kama unajua eneo leneyewe linaukaribu wa Bagamoyo, Dar, Pwani . Hivyo Kombora moja linakuwa tishio.
Iran ilipiga kombora kwa kambi ya Marekani baada ya kumuua kiongozi wao Iraq. Unajua nini kilitokea, mamia ya askari wa Marekani walipata 'concussion' na madhara mengine. Kombora hilo lituua Tel Aviv ni madhara tupu.
Nadhani nimekusaidia kuona picha kwa ukubwa wake na si kwa jicho la ' kukaririshwa, headlines, dini '' n.k.