Israel Imesema Imetumia Sehemu Ndogo ya Uwezo Wake Kuishambulia Iran, Uwezo Kamili Itautumia Iran Ikijibu

Ndio ujue akili zingine huwa zinashangaza sana😂😂😂😂😂ndege 100 mtu anakwambia shambulio dogo la nguvu ndogo😂😂😂😂🙌🙌🙌.
Kinachoongelewa hapo ni uwezo,kama uwezo alionao ni wa juu kuliko hicho alicho kifanya kwake ni shambulio dogo ndio maana hata Iran wenyewe wanasema wamepata madhara kiasi kutokana na nafasi walionayo.
 
hizi propaganda wala haziwezi kuwarudisha watu nyuma...israeli na iron dome is weak baada ya THAAD wanaona kama wana nguvu ya kushindana na Iran,ngoja tuone majibu...sehemu waliyotumia ndogo kuishambulia Iran hii ni kutaka viazi muone kama israeli mwamba kumbe bure kabisa,jiulize kwanini akipigwa yeye anazuia picha za satelite zisionyeshe alivyobondwa
 
Kinachoongelewa hapo ni uwezo,kama uwezo alionao ni wa juu kuliko hicho alicho kifanya kwake ni shambulio dogo ndio maana hata Iran wenyewe wanasema wamepata madhara kiasi kutokana na nafasi walionayo.
Ndege 100 sio uwezo mdogo.
Bro nenda kapigie mahesabu gharama ya kila ndege na mafuta yalotumika.
Hivi unajua ndege 100 zina uwezo wa kumaliza full out war!?
Tuacheni utani kaka.
 
Akina kimsboy na Ritz wamejificha wapi kuungana na Wairan wenzao kuipigia magoti Israel mbele ya BALAZA LA USALAMA?.
Halafu kesho mje mdanganye watu hapa kwamba Iran ni mwanaume. Nchi zote zilizoizunguka Israel zote ni wachumba tu kwa Israel.

Israel inaamua tu huyu imshambulie hivi huyu hivi kwa wakati gani.

Sikia sasa inapigana pande zaidi ya 5
Sasa fikiria tena nyie Wairan wa namtumbo. Israel iliivuruga Kwanza mifumo ya ulinzi ya Iran na nchi rafiki na Iran za karibu. Ndege zaidi ya 100 za Israel zikatamba kwa uhuru kwenye Anga la Iran. Wakapiga kwa kuchagua maeneo machache tu waliyotaka kuyapiga.
Hapo unajua nini?. Hata wangetaka kuisarambaratisha ikulu nzima. Kairan kote kalikuwa mikononi mwao. Halafu mjisifia madhara ni madogo tu,wakati maamuzi na huruma ya mpigaji anajua namna ya kukupiga,usipoteze mazima
 
Kwa sasa Adui mkubwa wa Israel ni HAMASI na sio IRAN, vita na IRAN haina impact yeyote kwa Israel kwa sababu Ni laisi sana HAMASI kuleta madhara Israel Kuliko IRAN, HAMASI wanaweza kufanya GROUND INVERSION kama walivyofanya october 1 na kuuma waisrael 1200, haya niambie makombora 500 ya IRAN yameua watu wangapi?
 
Your brainwashed by Jews, pathetic
 


Una tatizo la kushindwa kusoma au uelewa wako ni mdogo sana?

Hiyo ya kusema Israel imetumia sehemu ndogo ya uwezo wa jeshi lao, ni maneno yangu au ya Israel?
 
Una tatizo la kushindwa kusoma au uelewa wako ni mdogo sana?

Hiyo ya kusema Israel imetumia sehemu ndogo ya uwezo wa jeshi lao, ni maneno yangu au ya Israel?
Kwahiyo kila anachosema Israel basi kiaminiwe!??
Vitu vingine tumia common sense tu.
Ndege 100 kiuhalisia sio sehemu ndogo ya nguvu ya jeshi.
 
Koşa la İran ni kufadhili vikundi vya kigaidi vinavyoishambulia Israel. Kumbuka Oct 7 Hamas, Hezbollah ndio walianza mashambulizi dhidi ya Israel
 
Acha uzindiki,shida sio hamas tatizo ni USA na UK walienda kuanzisha nchi kwenye ardhi ya watu.


Tatizo watu mnafurahia kuwa wajinga. Jibidisheni kutafuta maarifa ili mjenge hoja reasonably.

Mimi kwa sababu naifahamu vizuri historia ya eneo hilo, ndiyo maana siafiki ujinga wa wale Waarabu wa mwaka 1948 waliosema kuwa Wayahudi hawana haki na hilo eneo, wanatakiwa kumalizwa. Na wala siwezi kuunga mkono kauli ya baadhi ya wayahudi wanaosema kuwa eti waarabu waliopo Palestina hawastahili kuwepo eneo hilo kwa kuwa ni wavamizi. Bali kunatakiwa kuwepo busara ya kuona wanaweza kuishi vipi wote kwenye eneo hilo maana wote wana haki.

Kuna wayahudi ambao wamekuwepo eneo hilo vizazi vyote, japo baadaye idadi yao ilipungua sana kwa sababu wengi wao walihamia sehemu mbalimbali za Dunia. Lakini pia wapo waarabu, ambao zamani walikuwa wachache sana ukilingamisha na wayahudi, lakini kwa vile wao hawakuhama kama kizazi cha Wayahudi, idadi yao ilizidi kuongezeka mwaka hadi mwaka. Hivyo wote wana haki ya aina fulani na eneo hilo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…