Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

🚨 The occupation forces carried out an airstrike targeting an apartment in the Five Wings area of Choueifat in Beirut without prior warning.
 

Attachments

  • Screenshot_20260305_000545_Telegram.jpg
    87.8 KB · Views: 9
Yap yap, pia na international pressure ilichangia
 
Hao jamaa Iran ilisema toka zamani wanatumika na US , Saudi, UK na Israel, kama proxy wa kufanya intel zao. Miaka ya 2000s early.

Turkey pia wanasema Wakurdi wana muunganiko na US.

Hivyo Turkey na Iran walifanya kitu wanaita Iran–Turkey High Security Commission miaka ya 2006/7 hapo . Na waliwatandika balaa na kuwapa mazingira magumu sana hao Wakurdi, jeshi la Turkey waliwafuata huko milimani Kaskazini mwa Iraq mpakani Iran, Iran ikarusha ndege kuwapiga, kuna hilo kundi wanaitwa PJAK na lingine PKK hao wote ni Kurdi na ni marafiki, hao PJAK baada ya kuona mazingira magumu, wakasema wao hawahusiki na kushambulia raia wa Turkey bali ni PKK.

Ikaja kuonekana PKK na PJAK lao lote ni moja.

Wakati wa G W Bush walikuwa wanawezeshwa hao Kurdi, sera wakati wa Obama ikabadilika , 2009 united States department of the treasury walilitambua hilo kundi ni la kigaidi, PKK wana muingiliano na PJAK, na wana ideologies zinazofanana, EU wanatambua PKK ni terror group.

US inalitambua PKK pia kama kundi la kigaidi.

Sasa tujiulize , watu wanaopiga kelele, hapo nani mfadhili ugaidi, na kuna habari hapa, ndege flani inaweza kuwa ya US ama Israel imekwenda eneo la hayo makundi na kurusha mizigo kutoka angani , probably ni silaha, askari wa Iraq waliokuwa kwenye doria kusogea kwenda kuangalia kulikuwa na kitu gani, nadhani wakiwa na gari wakashambuliwa na kufariki kwa airstrike, unaweza kuona hao washenzi nyuma ya pazia walivyo na roho za kigaidi.

US na Israel ina fund terror group kupambana na Iran.
 
Dah mkuu mpaka nimeogopa haya mambo unaweza kuyachukulia poa tu lakini ukijipa mda utaanza kuuona ukweli taratibu na siku zote penye ukweli uongo huwa na tabia ya kujitenga. Hapo mashariki ya kati hapatakuja kupoa ni vita juu ya vita tena ni vita vya kuchonganishwa mataifa ya hapo.
 
Wanachoongelea ni Ile video ya wanajeshi wapo shule kwamba Jeshi la Iran lipo shule,

Baada ya Ile shule kupigwa msemaji wa Serikali na wanajeshi walienda kutoa hotuba pale pale so Wana spin habari ionekane kama vile Jeshi lilikua limejificha pale.
 
Hapo ni hatari, ukiona hadi US na Israel wanakwenda fund terror group ufahamu mchezo umekuwa mgumu kwao.

Na waliua hao askari kupoteza ushahidi. Hatari sana, kuua hao askari tu ni ugaidi wewe unaaje askari yupo kwenye majukumu yake ya kusimamia usalama wakat huu wa vita middle east? jamaa nyuma ya pazia wanafanya mission za kigaidi sana. Ni basi tu watu hawafahamu ukweli.
 
Wanachoongelea ni Ile video ya wanajeshi wapo shule kwamba Jeshi la Iran lipo shule,

Baada ya Ile shule kupigwa msemaji wa Serikali na wanajeshi walienda kutoa hotuba pale pale so Wana spin habari ionekane kama vile Jeshi lilikua limejificha pale.
Hali ya kuwa kuna ujio wa kiongozi lazima apewe ulinzi na wanafunzi waliokuwepo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…