Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Marekani ni mtu mbaya mnooo, ukatili wake huenda ukamzidi genghis khan na mongolia yake ya kale
 
Iran sijui na dini inawalemaza, sawa hampigi raia ila ikiwezekana miundombinu yote fumueni, we unadhani israel na mmarekani wangekuwa kwenye nafasi yao ingekuwaje?
 
Mie nahisi marekani ndio shetani mwenyewe.
Huwezi fanya unyama kama ule kisa interest zako, umeme sio wa rais ni wananchi wote wanategemea hapo
Uzuri Wairan walikuwa werevu wakakataa kumeza ndoana zake kuwa anawapa serikali yao, somo zuri liko Libya, Iraq, Sryria na Yemen. Ni ujinga wetu tu kujishindwa kukumbuka historia vizuri kabla ya kuafikiana na USA.
Halafu mbele ya kadamnasi anajinasibu kupigania haki za raia mpuuzi yule.
 
Na kuuwawa kabisa
Sijui kwanini dunia bado inamchekea USA pamoja na ufedhuli wote huu anaoufanya waziwazi hivi.
 
Wizara ya Mambo ya Nje ya Lebanon imetangaza kufuta ithibati (accreditation) ya balozi wa Iran, Mohamed Reza Cheibani, na kumtangaza kuwa “mtu asiyetakiwa” (persona non grata), huku ikimtaka aondoke katika ardhi ya Lebanon kabla ya siku ya Jumapili.

Taarifa ya wizara hiyo imesema kuwa uamuzi huo umechukuliwa ndani ya mamlaka ya kidiplomasia ambayo taifa linayo.

Wizara hiyo pia imetangaza kumwita balozi wa Lebanon aliyepo Tehran kwa mashauriano, ikieleza hatua hiyo kuwa ni kutokana na kile ilichokitaja kama ukiukwaji wa “desturi za kidiplomasia na taratibu zilizokubalika” kati ya nchi hizo mbili uliofanywa na Tehran.
 
US Ford inarudi US kwa ajili ya matengenezo ambayo itawachukua zaidi ya miezi 14.
Hizi cheap propaganda zinawasaidia nini hasa?

USS Gerald R. Ford ilipata moto ndani na inaenda kufanya matengenezo, lakini moto huo haukusababishwa na Iran na meli bado ina uwezo wa kupigana.

Pia inaenda Greece (Crete) kwa matengenezo ya muda mfupi, sio Marekani kama unavyodanganya.

Hilo la kusema itachukua miezi 14 ni makadirio ya baadhi ya wachambuzi uchwara pro Iran, si taarifa rasmi ya jeshi la Marekani.
 
ISFAHAN: KIWANDA CHA TEKNOLOJIA YA KIJESHI "SAIRAN" CHAPIGWA!

Video iliyosambazwa na ukurasa maarufu wa Telegram wa "Vahid Online" leo mchana, imeonyesha uharibifu mkubwa katika jengo la Optics Sairan (Isfahan Optics Industries) mjini Isfahan. Hili ni pigo lingine la kimkakati dhidi ya uwezo wa kiteknolojia wa Iran.

Kwanini Sairan imeshambuliwa?

Optics Sairan si kiwanda cha kawaida; ni kampuni tanzu ya Iran Electronics Industries (IEI) iliyo chini ya Wizara ya Ulinzi ya Iran.

Kiwanda hiki kinajulikana kwa kutengeneza:

Vifaa vya Macho (Optics)

Mitambo ya kuona usiku (night vision), lenzi za droni, na mifumo ya kuelekeza makombora kwa kutumia leza (laser guidance).

Vifaa vya Kielektroniki

Teknolojia inayotumika kwenye vifaa vya kijeshi vya kisasa.

Uhusiano na IRGC

Ni kiungo muhimu katika kuimarisha droni na makombora ya Iran yaweze kupiga kwa usahihi.
 
Tunachotaka ndio ichi Vita viendelee hakuna poooo

mpaka sasa team Iranian tunaenda kushinda mtanange Trump yupo njia panda!!.

Tumpe siku mbili tu zaidi tuone Marekani itakuja vipi muhimu kabanwa vibaya🤠🤠

Washirika wake wanalalamika kitendo cha Trump kuichokoza Iran na sasa hawezi kuzima Vita..
 
Sijui upo dunia gani.


View: https://m.youtube.com/watch?v=xsWomTQchgo&pp=ygUPdXMgZm9yZCBiYWNrIHVz

View: https://m.youtube.com/watch?v=_frX5ezPdcQ

View: https://m.youtube.com/watch?v=wv6R9_XUe5s
Kituo cha kwanza Ugiriki kwanza wanaifanyia repair ndogo ndogo then wairudishe kwao kwa ukarabati mkubwa.

Matengenezo ya mfupi miezi kumi na nne? Mlipuko mdogo ila watu 200 wamejuruhiwa na iliwachukua masaa zaidi ya 30 kuuzima.Hapa labda uwe ujitoe ufahamu ila mwenye akili kaelewa kilicho wakuta. Lincoln sasa hivi hatuisikii kabisa.

Wewe unategemea taarifa rasmi, hivyo vyombo vyao Secretary of Defence kavipiga mkwala kuvifungia, sababu vinaongea ukweli anaona kama havina uzalendo? Wewe unategemea upate maelezo ndani ya siku tano ndege tatu mbili za F-15 moja ni F-15,zimepigwa na video zake wakati zikipigwa watu wameshare, vipi US walitoa maelezo? Atoe maelezo aharibu biashara yake ya silaha.
 
China inaenda kuwaTaifa kubwa Duniani 🤠🤠 mzozo wakujitakia unaenda kusomba Uchumi wa Marekani Gulf States!!!

nguvu kuu ya pesa yao vinaenda zikwa kwa pamoja. Vyovyote viwavyo Marekani itajutia kumchagua Trump.

Na sifa za Trump zimeenda na maji.!!!

Kuna uwezekano baada ya Uchaguzi wa Mabunge chama cha Democratic kinaenda shinda!!!

.na uyu Mlokole Trump watamtimua kupitia Bunge jipya,,
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…