Huyu Rais wa Marekani hata haeleweki na kuna kila dalili kwamba aliburuzwa na Netanyahu kuingia kwenye hii vita.
Mara aseme anataka unconditional surrender, mara anasema Iran asipofungua Hormuz basi atalipua kila kitu ndani ya Iran, mara atoe siku tano, mara aziongeze tena hizo siku tano hadi siku sijui kumi na ngapi, mara aseme Iran wanambembeleza wafanye mazungumzo naye, na sasa kaja na hii ya kwamba hata Hormuz isipofunguliwa anaweza akamaliza vita!
Ukisikia kukurupuka ndo huku sasa! Unakuwa hata hueleweki unachokitaka ni nini.
View attachment 3564850