Tatizo huwa mnakua na hisia zaidi na matamanio fulani badala ya uhlisia sababu hii vita haituhusu.
Unassma Israel na marekani wanashambulia vyuo, maprofesa, sinagogi. Nimeshangaa hili kwa maana umeshindwa kusema kuwa wanashambulia wanajeshi Tena high rankings na kuwaua. Nimeshangaa pia hujasema mashambulizi yanayofanywa kila siku kwenye kambi za jeshi. Au hayafanyiki?
Ukweli mchungu wala tusibishane sana Iran hawezi kuwa na huruma na Israel ikiwa lengo la Iran ni kuifuta Israel. Yaani uwe na lengo la kuangamiza nchi nzima then hapa useme kuwa Iran hajaamua kupiga hizo sehemu zingine? Inawezekanaje hii?
Wewe sasa unaleta uhalisia gani zaidi ya kutuuzia chai uhalisia husio na reference huo nao unauita uhalisia, maana vita umeigeuza kama marede,mara Fatuma kamrushia mpira,Habiba mara Fatuma kamrushia mpira Joyce reference hauna?
Sasa umeshambulia high rankings officer vipi wamefanikiwa kupunguza rate ya mashambulizi? Umeangamiza high rankings officers halafu unaomba suluhu ya kidiplomasia, sasa ina maana gani? Iran sio Hamas, kila position ina watu zaidi ya kumi wanaweza shikilia hiyo nafasi. Yaani unaangamiza high rankings officers halafu bado unapiga vyuo vikuu,nyumba za maproffesa mpaka nyumba za ibada, vipi sites za kijeshi zimeisha? Maana rate ya mashambulizi Iran inazidi kuwa kubwa kila siku.
Hizo nyingine ngonjera hao high ranking officers wenyewe wa NATO na mkuu wa Counterterrorism Kent hawajui wala hawaoni sababu ya kwa nini US/Myahudi wanampiga Iran,hizo sijui Iran anataka kumfuta Myahudi ni sababu tu za uongo kama ilivyo kwa Mass of Weapons Destruction na Iraq ya Sadam.
Hata nikikuuliza wewe malengo ya hii vita hauna kwani kila siku yanabadilika, Trump mwenyewe mpaka sasa haeleweki lengo lake ni nini,yaani ile press ya jana amekuwa kama chizi aliye kabiziwa rungu, hajui alitumiwe wapi na wakati gani.
Kuna Maseneta huko wanataka ku-invoke 25 ammendments,wanaona wanaongozwa na chizi.
View: https://m.youtube.com/watch?v=ZlQAP_VGCq8