Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Hii kamba ya Ndege za Israel zinazurura ovyo Iran inarudiwa kila siku humu, lete source, siku zote hizo Ndege zinatumia Anga ya Iraq, na sasa hivi Iraq pia kimenuka soon wataikosa na hio support.

Halafu we jamaa mweupe Sana, USA kashindwa miaka 20 Afghanistan, unahisi Israel anaweza siku 3 Iran? Israel wenzako wanachapika huko, Tel Aviv kuna mafuriko, kila kona kunawaka na Moto.

Iran kama ilivyo Afghanistan ni nchi ya milima, huwezi kamwe kuipiga na Air strikes, Zana zao na tech zao zote zipo chini ya milima. Kuna njia moja Tu ya kupigana nao ni vita vya Ardhini ama ufanye Mapinduzi, ambayo so far ni unlikely kwa support inayoendelea.
Tel Aviv inanuka kinyesi, mfumo wa maji taka unaobeba uchafu toka majumbani kupitia chambers umetandikwa, Tel Aviv inanuka kinyesi... hapo lazima ifuatane na kipindupindu, homa ya tumbo na kuhara..
 
Eeeh bwana eeeh, Israel inapelekewa moto huko sio poa.
Makombora yanapishana tu hewani kuelekea Israel.
Hawa Iran wanarusha makombora kutokea wapi.
Maana nasikia Israel anatawala anga la Iran anavyotaka, kama ni hivyo wanashindwaje kudhibiti haya makombora yanayoenda kuibomoa Israel?
 
Wazee kuna aina mpya ya kombora Iran anaendelea kurusha toka leo alfajiri, linapangua makombora ya iron dome halafu linakwenda kuipiga launcher ya iron dome..

Yaani badala ya kombora la iron dome ku neutralize makombora ya Iran, kombora la Iran linaanza na kombora la Iron dome kulilipua halafu inafuatwa launcher iliyolituma... asee kama vita inaelekea huku basi tutashuhudia mengi.. haya ni zaidi ya matusi..


View: https://twitter.com/i/status/2027857349361226104
 
Swali lengine, vita vikiwa vya muda mrefu Marekani na Israel wamejiandaa kuvipigana pale malengo ambapo hayatafikiwa ?

Nina uhakika Israel na Marekani wanatumia gharama kubwa kwa siku tu toka jana mpaka leo tena Marekani toka ana hamisha vifaa. Swali wapo tayari kuendelea kuchoma hizi pesa kwa muda gani ?
 
Aiseeh! Yaani ni aibu Sana.

Hapo watarusha makombora hovyohovyo bila mipango.
Ni kama mtu aje kwako akupige wewe Baba WA familia. Alafu watoto wako wakarushe mawe nyumbani kwako wakapasue vioo vya dirisha, au gari, wachome shamba lako.

Bado haiondoi ukweli kuwa Baba wa Familia amepigwa na familia yenu imepigwa.

Tatizo wengi hawajui nini maana ya vita.
Na kwenye vita kuna target ambazo zikipigwa itadaiwa umepigwa. Target ya Kwanza ni kiongozi mkuu na viongozi wa majeshi.
Simple.
Mkuu Iran harushi hovyo hovyo angekuwa ana shambulia hovyo basi hayo makombora yangekuwa yanaangukia nchi yeyote ile hata zile ambazo hazihusiki .
Mashambulizi yake hayafanyiki kwa bahati mbaya bali moja wapo ya mkakati wake kwanza mkakati wake ni kutaka kusimamisha shughuli za kiuchumi kwenye eneo lote la mashariki ya kati ili nchi hizo ziathirike ili ziishinikize Marekani iache kuishambulia nchi hiyo .
Mkakakati wa pili ni kuichosha mifumo yao ya ulinzi ili waishiwe makombora ya kutungulia na ndio maama unaona mpaka sasa Iran anatumia makombora yenye kasi ya kawaida na si yenye kasi kumbwa.
Alafu kingine mkuu ni kweli Iran kwa sasa yupo kwenye engo mbaya lakini kisema anashambulia hovyo unakosea kwa sababu mpaka sasa Iran imekiharibu kabisa kituo kikuu cha wana maji cha marekani kilichoko Baharen,hata kituo cha Kuwait kwa mujibu wa picha za satellite zilizo oneshwa asubuhi ni kimeharibiwa kwa kiasi kikubwa bado na cha Iraq kimeharibiwa huko Qtaar rada kubwa na ya hali ya juu ya kufaatilia makombora ya Marekani imeharibiwa kabisa kwa upande wa Israel kwakweli sijui maama kuna udhibiti mkali ya habari.
Kwangu mimi mkakati wa mapigano alio nao Irani naona wako sawa kabisa ila mm kinacho nikera kwa Iran ni uzembe ulio pitiliza juu ya usalama wa viongozi wake.
 
Iran kuiangusha bila ground invasion,coup au civil war itanipa picha mpya kabisa kuhusu mbinu za kimedani kama Israel na Marekani wataweza kufanya hivyo kinyume na hapo ni kutwanga maji kwenye kinu
Ndio maana wanataka wana nchi waingie barabarani waandamane ili kutokee uasi ili serikali ipinduliwe kutoka ndani.
 
Yaani kwa ufupi Iran anachapika kuliko zile siku 12
Endelea kuota.
US senate wanamlaumu Trump kwa vifo vya US navy nchini Bahrain na UAE.
Hasara zilizoletwa ni billions of dollars..
Strait of Hormuz imefungwa na kuna meli imelipuliwa ya mafuta.
Balozi za USA Baghdad na Karachi zimetiwa kibiriti.
Embu hesabu hizo hasara.
 
Mauaji ya 07/10/2023 Israel iliyaruhusu kwa makusudi ili wapate sababu ya kufanya haya wanayofanya leo.
Maana Hamas, Hezbollah, Assad na Houthis wote hawapo
Israel anatumia anga ya Syria kujaza mafuta ya kwenda ipiga Iran
 
Nisiwe mnafiki vifaa alivyo kusanya Marekani ukichanganya na jeshi la Israel na hiki kinacho endelea napata mashaka kama Marekani anaweza pigana na taifa lenye uwezo mkubwa wa kiviwanda na linalo karibiana naye kwa namna fulani pasipo Washington kuumia vibaya sana.

Imagine Iran huyu si mdogoshi hata kidogo ana uwezo wa kushambulia makambi ya Marekani na yupo kwenye vikwazo muda mrefu wala hana teknolojia kubwa maeneo mengi kijeshi kwa ukaribiano na Marekani vipi kuhusu taifa ambalo litakuwa na uwezo mkubwa wa kiviwanda na lipo huru na vikwazo kwa muda mrefu Marekani itapata hasara kiasi gani ?

Mpaka sasa utofauti wa mtu mbili dhidi ya mtu mmoja sio mkubwa kama nilivyo tegemea au tegemewa kwa jinsi vifaa vilivyokuwa vikikusanywa labda kama taswira ya vita itabadilika huko mbele tusubiri tuone
 
Back
Top Bottom