Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Aiseeh! Yaani ni aibu Sana.

Hapo watarusha makombora hovyohovyo bila mipango.
Ni kama mtu aje kwako akupige wewe Baba WA familia. Alafu watoto wako wakarushe mawe nyumbani kwako wakapasue vioo vya dirisha, au gari, wachome shamba lako.

Bado haiondoi ukweli kuwa Baba wa Familia amepigwa na familia yenu imepigwa.

Tatizo wengi hawajui nini maana ya vita.
Na kwenye vita kuna target ambazo zikipigwa itadaiwa umepigwa. Target ya Kwanza ni kiongozi mkuu na viongozi wa majeshi.
Simple.
Mkuu vita haijaisha..

Iran kuuawa kwa Khamenei kumepelekea regime change?
Kuna maana gani ya US na Israel kila siku kuwaweka raia wao matatizoni halafu regime change haitokei, mbona wanatwanga maji kwenye kinu?

Hapo unasema wameshinda vita? malengo ya yalikuwa ni yapi?

12 days war, Netanyahu alipata hasara kubwa sana, kwa shinikizo, uchungu na aibu akalazimishwa asimame vita, hata hii vita anapambana hivi sasa yupo kihisia zaidi, kitu ambacho kitampelekea kujuta.

Isral na US ni kama walipanga walau kumaliza hasira zao ni kummaliza Khamenei, ndio maana Trump kaandika gazeti refu huko mitandaoni.

Iran hasara iliyo sababisha 12 days war ni kubwa kuliko watu wafikiriavyo.

Ajabu toka hayo yote yameanza hawajafanikiwa hata moja, labda kuua viongozi.
 
Screenshot_2026-03-01-14-11-24-48_40deb401b9ffe8e1df2f1cc5ba480b12.jpg


Paralyze uchumi mzima middle east, funga njia zote, hakuna anayeingia hakuna anayetoka!
Oyah weeeeh!!!
Muajemi hacheki na yeyote!
 
Iran inapigwa kihatatua zilipangika.

Vita ya siku 12, ilikuwa ni kwa ajili ya kuharibu uwezo wake wa Nyuklia na wamakombora.

Vita ya sasa hivi ni kumaliza uwezo wake wa makombora na Kijeshi na kitaasisi.


Iran ikishamalizwa malizwa uwezo wake kuishambulia Israel, Silaha zitaanza kugawiwa kwa wananchi wa kawaida kuipindua Serikali huku Israel akiwa anaishambulia Iran kama Syria.
Kwamba Iran uwezo wao wa makombora uliharibiwa vita ya siku 12? Hebu kuwa serious basi, vice versa is true Israel Hana tena Ammunition za kuzuia makombora ya Iran sasa hivi huoni tena makombora ya Iran yakiwa intercepted kwa nguvu. Ndio maana sasa hivi Tel Aviv kila sehemu kunapigika.
 
Kama anpigwa strategi sites, si wapige huko kwenye missiles launchers zake?
Tel Aviv inapigwa vibaya...
KWani Israel Gaza alikuwa anapiga strategic sites..
Kuua wanafunzi waliokuwa shuleni ni strategic site?
Shida kubwa ya pro -Israel na US ni kwamba Iran ikishambulia maneno yanakuwa anapiga sehemu zisizo za kimkakati ,wakati pale Gaza alikuwa anafanya hivyo hivyo ukiwaambia hivyo utasikia magaidi walikuwa wamejificha😀

NB:Vita sio ya kuweka ushabiki wa Simba na Yanga.
 
Acha kudanganya watu Kuanzia Iraq, Iran, Pakistan Hadi India kuna maandamano makubwa kumlilia Ayatollah.

Hii Iran, unambie kuna kiumbe kilitoka nje hapa kupinga? Tena ndani ya Iran utembee na bendera ya Israel? Kadanganye chekechea huko.

View attachment 3550548
Nimekuambia video ya kwanza ni IRAN. Umeona bendera ya Israel kwenye video ya kwanza?
 
Binafsi kifo cha Ayatollah hakija ni shitua kabisa mzee tayari alikuwa maiti inayotembea muda wowote ange fariki hata kwa presha hata yeye bila shaka alikata tamaa ya kuendelea kuishi tena hapa Israel na Marekani ni kama wamepiga bomu mochwari.

Israel na Marekani walipaswa kumuua successor wake na successor wa IRGC wadeal na kuiangamiza kabisa Iran tofauti na hapo sidhani kama kuna kitu kita badilika kwa ukubwa ndani ya Iran.
 
Leta habari za uwakika hapa usite propaganda, sema wamekufa askari wangapi. Yaani mtu anakuja kukuzingira kwako na mameli ya kivita na anauwa kiongizi mkuu nchi na viongizi top wa ulinzi unashindwa kushambulia meli unaenda kupiga kambi ambazo makimbira enyewe wana ya intersect.
-Bahrain walitangaza wanajeshi 13 wamefariki.
-UAE wameripoti wanajeshi wanne.
-Kuwait waliripoti wanajeshi wanne.
Hizo ni taarifa rasmi.

Zisizo rasmi zinasema mamia wameuawa katika kambi za Qatar,Jordan.
 
Sina tatizo na khamenei.
Hapa tunazungumzia Suala la Iran anatoboa au hatoboi.

Vita inakanuni zake.
Na Khamenei na wenzake wote wanazijua.

Iran wanajua fika hawana uwezo wa kumshinda Marekani. Hilo lipo wazi kimahesabu.

Ili Iran ashinda lazima apate washirika wakweli kabisa ili kumpa nguvu na ku share cost.

Ndege za Israel kama zinazurura hovyo juu ya anga la Iran unafikiri kuna nini hapo.

Yaani Israel wakisema wapige kipigo cha hasira kama wehu. Ni Siku tatu tuu kwa kutumia ndege kazi itakuwa imeisha.

Ila Hawawezi kufanya hivyo kwa sababu pia vita ni suala la kisaikolojia. Wanapiga kimkakati na pia kuwashirikisha na kuwashawishi raia wa IRAN wajiunge kuungausha utawala wa Ayatollah.
Lengo unajua ni nini?
Hii kamba ya Ndege za Israel zinazurura ovyo Iran inarudiwa kila siku humu, lete source, siku zote hizo Ndege zinatumia Anga ya Iraq, na sasa hivi Iraq pia kimenuka soon wataikosa na hio support.

Halafu we jamaa mweupe Sana, USA kashindwa miaka 20 Afghanistan, unahisi Israel anaweza siku 3 Iran? Israel wenzako wanachapika huko, Tel Aviv kuna mafuriko, kila kona kunawaka na Moto.

Iran kama ilivyo Afghanistan ni nchi ya milima, huwezi kamwe kuipiga na Air strikes, Zana zao na tech zao zote zipo chini ya milima. Kuna njia moja Tu ya kupigana nao ni vita vya Ardhini ama ufanye Mapinduzi, ambayo so far ni unlikely kwa support inayoendelea.
 
Shida kubwa ya pro -Israel na US ni kwamba Iran ikishambulia maneno yanakuwa anapiga sehemu zisizo za kimkakati ,wakati pale Gaza alikuwa anafanya hivyo hivyo ukiwaambia hivyo utasikia magaidi walikuwa wamejificha😀

NB:Vita sio ya kuweka ushabiki wa Simba na Yanga.
Well said mkuu..
Iran imesababisha ionekane kawaida Tel Aviv kushambuliwa..
 
Iran kuiangusha bila ground invasion,coup au civil war itanipa picha mpya kabisa kuhusu mbinu za kimedani kama Israel na Marekani wataweza kufanya hivyo kinyume na hapo ni kutwanga maji kwenye kinu
 
Kama Israeli na marekani waliamini tatizo la Iran ni kamineeh basi wameshinda. Kama tatizo halikuwa hilo. Basi wana kazi kubwa sana mbeleni
Wamemchagua kiongozi wa mpito Ayatollah Alireza Arafi.
Ana misimamo mikali kuliko Khamenei. Huwenda huyu jamaa kama akiendelea kushika uongozi Iran ikamiliki nuke weapons soon.
 
Back
Top Bottom