Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Israel na Marekani zaishambulia Iran. Serikali ya Israel yatangaza hali ya hatari

Hio ni namna ya kuomba cease-fire, amezoea kuingia Iran na kuua, halafu anaomba cease-fire, ni kama amewazoea waajemi, this time lazima kimlambe na awajibike.

Iran iendelee na mashambulizi hadi kule baharini, wasogeze na majeshi karibu na Israel, maana jeshi la Iran ardhini wapo vizuri kuliko hata jeshi lao la anga.

Israel itandikwe na mshariki ya kati ichafuke, iwe fundisho.
Ha ha ha mkuu unafurahisha sana. Makao makuu ya jeshi yameisha huko Iran. Ndege za Israel zinatamba Tehran inakuwaje?
 
Haaa! Aiseeh
Mkuu wewe hujui mambo ya kijeshi na medani za kivita.

Na pengine huenda hujui kadiri kiongozi wa kijeshi anavyokuwa na cheo kwanini ulinzi wake unaongezwa.
Ungejua hivyo ungeelewa Kwa nini Israel na USA na wafuasi wao kwao huo ni ushindi mkubwa

Vita Siku zote ni mpige Mchungaji na kondoo watatawanyika wenyewe. Hiyo Kanuni inatumiwa na Majeshi yote yenye nguvu.

Sasa Hiyo Iran anachofanya ni kuhadaa walimwengu na pengine kujitetea maskini.

Unarusha rusha mabomu hovyo, hata uchome Ikulu, au mji mzima kama kuna watu wakubwa hujawaua hiyo vita haijaisha.

Wewe anapigwa mkuu wa majeshi na Ayatollah sasa nani aliyebaki kwenye nchi??
Majeshi yapi? Kama yameshindwa kulinda viongozi wao wataweza kujilinda wao wenyewe?

Iran sasa hivi ipo kwenye mfumo, inatagemea tuu utashi wa Trump
Kuua makamanda wakuu ndio kushinda vita??
2006 IDF iliua makamanda wakuu wote wa Hizbollah lakini bado Hizbollah imeshinda vita dhidi ya Israel.

-Ameshateuliwa kiongozi mpya Alireza Arafi. Iran ina mkakati mrefu wa succession sio nyepesi kama unavyodhani.
Ayatollah mpya katangazwa na msimamo wake ni ule ule.
Iran serikali yake inaongozwa KIITIKADI. Nadhani hili wengi hamlijui.
 
Inategemea na jamii na jamii, kuna jamii Kufa kwenye vita ni status.

just imagine kuna watu watoto wao, ndugu zao na jamaa zao wanakufa vitani ila wakiangalia viongozi wao wanakula Tu mema ya Nchi,

Ila unapoona kiongozi wako yupo mstari wa mbele na yupo tayari Kufa kwa ajili yako inakupa morale na wewe unajitolea kwa Moyo wote.

Mashia ni nut case, huyu khamenei alikua ni mpole na kazuia mambo mengi Sana, ila akiingia hardliner wa Jeshi hapo juu patachafuka mno hapo.

Sina tatizo na khamenei.
Hapa tunazungumzia Suala la Iran anatoboa au hatoboi.

Vita inakanuni zake.
Na Khamenei na wenzake wote wanazijua.

Iran wanajua fika hawana uwezo wa kumshinda Marekani. Hilo lipo wazi kimahesabu.

Ili Iran ashinda lazima apate washirika wakweli kabisa ili kumpa nguvu na ku share cost.

Ndege za Israel kama zinazurura hovyo juu ya anga la Iran unafikiri kuna nini hapo.

Yaani Israel wakisema wapige kipigo cha hasira kama wehu. Ni Siku tatu tuu kwa kutumia ndege kazi itakuwa imeisha.

Ila Hawawezi kufanya hivyo kwa sababu pia vita ni suala la kisaikolojia. Wanapiga kimkakati na pia kuwashirikisha na kuwashawishi raia wa IRAN wajiunge kuungausha utawala wa Ayatollah.
Lengo unajua ni nini?
 
Wengi uwezo wao wa kufikiri mdogo humu watakuelewa basi, Fox wanareport damage Tel Aviv ni kubwa kupita wakati wowote, sasa hivi huoni iron dome wala patritot, Iran kaanza na Radar na Base za waarabu Kwanza kuvunja mfumo wote, Even Meli vita za Marekani zishaondoka huo Ukanda nyengine zimeenda India na nyengine zimekimbia nyuma ya Israel
Hizo bases za US zilizopigwa zilikuwa zina radars na vyombo ambapo vilitumika kutoa early warning hadi Israel.
Walitengeneza Integrated Air and Missile Defense (IAMD), Iran ikirusha makombora, tayari Qatar inaona, Kuwait, Bahrain n.k... hivyo wanafanya radar data sharing ama wana link na radar za Israel, hivyo Israel wanapata taarifa kuna missiles zipo njiani.

Kwa jinsi hali ilivyo, Israel itaharibiwa vibaya, na Iran imeamua kufa na Israel, hata waarabu wengi hapo wana kinyongo kuhusu Gaza bado, hata Qatar watakaa kimya.

Ndio maana Iran kwa hasira anatandika hizo kambi na anapiga si mchezo, maana hizo nchi walifahamu wanatumika na US na walikaa kimya.

Tel Aviv inaharibiwa vibaya kabla hata masaa 48 hayajafika, ni majanga makubwa.
 
Mkuu location ya Ayatollah sio big deal?🤓🤓.
Hapo humzungumzii Ayatollah personal unazungumzia Ayatollah kama taasisi.
Sijui kama unaelewa.

Viongozi wa serikali na kijeshi wanafamilia ndio.

Hivi unajua kiongozi wa nchi analindwa kuliko vinu vya Nyuklia?
Mwanzo walikuwa wanasema hawezi kufikiwa sasa kadikiwa yeye na wakuu wengine sio deal.
 
Kiongozi wa nchi kauawa,mkuu wa majeshi kauawa,waziri wa ulinzi kauawa vipi tena hawa Iran hawakuhifunza kwenye ile 12 day war ambayo wanasayansi na makamanda waliuawa pia? Nakumbuka Trump alisema yeye ndio alozuia Israel wasimuue wengi wakaona ni propaganda sasa nafikiri wengi wamejua ile haikuwa propaganda.
Vita imeisha hio.
Na pia Israel ndo kamuua
 
Ni sawa mwanaume aliwe tundu aseme nimeliwa kidogo.
Aibu na jambo hilo halikutegemewa..Wataandaman ila jibu ni moja aibu...aliyeuliwa ukiangalia kauli zake zilikuwa za kibabe amekkufa kiboya boya sana...potea na mawazo hayo utakufa na presha.
Hao wajiite Dunia nzima..wahuni watapagonga hapo kama Syria..pataisha mtakuja kulia lia humu free Iran free Iran..Wazungu ni wahuni hawana hizo stori zenu za kelele nyingi.
Bro sasa unaongea hisia badala ya uhalisia.
Nakuacha na facts chache pia sitahitaji kujadiliana na wewe maana uko kihisia zaidi.
1.2006 Israel iliua makamanda wakuu wote wa hizbollah,ila Hizbollah ilifanikiwa kuwapiga Israel na kuwapokonya Bint jubeir.
2.1980 hadi 1988 Iran ilivamiwa na Iraq ikiwa na usaidizi wa Marekani viongozi wengi wa Iran waliuawa,Iran iliteua uongozi mpya ikapambana na kushinda vita.
3.2025 June Israel iliua asilimia 90 ya top millitary commanders na viongozi wakuu ila still Iran iliteua viongozi wapya na ikapambana na Israel na aliyeomba vita iishe ni Israel.

SIONGEI MAHABA KAMA WEWE KAA PEMBENI NIJADILI NA WANAOJIELEWA.
 
Mkuu unafuatilia kinachoendelea Tel Aviv, Tel Aviv inawaka moto...:FIRE::elmoFire:..

Kwa haya mashambulizi ikipita siku 10, Tel Aviv inakuwa Gaza..
Nafuatilia naona Iran anavyorusha missile hovyo pande zote. Anaharibu apartments,airports. Mwenzio analenga vitu muhimu vya kivita.
 
Netanyahu alishawahi sema yuko tayari kwa Israel kushambuliwa imradi tu Uongozi wa Iran ubadilishwe
 
Nafuatilia naona Iran anavyorusha missile hovyo pande zote. Anaharibu apartments,airports. Mwenzio analenga vitu muhimu vya kivita.
Kama analenga vitu muhimu vya kivita, kwanini asilenge huko Iran wanaporushia hayo makombora?
Israel kuna sheria kali sana sasa ya kudhibiti taarifa za kivita.. wananchi wanakamatwa na polisi..
 
Mwanzo walikuwa wanasema hawezi kufikiwa sasa kadikiwa yeye na wakuu wengine sio deal.

Aiseeh! Yaani ni aibu Sana.

Hapo watarusha makombora hovyohovyo bila mipango.
Ni kama mtu aje kwako akupige wewe Baba WA familia. Alafu watoto wako wakarushe mawe nyumbani kwako wakapasue vioo vya dirisha, au gari, wachome shamba lako.

Bado haiondoi ukweli kuwa Baba wa Familia amepigwa na familia yenu imepigwa.

Tatizo wengi hawajui nini maana ya vita.
Na kwenye vita kuna target ambazo zikipigwa itadaiwa umepigwa. Target ya Kwanza ni kiongozi mkuu na viongozi wa majeshi.
Simple.
 
Vita mbichi kiongozi wa juu anapigwa kirahisi. Hivi unafikiri sawasawa kweli?

Tafuta wanajeshi au watu wa usalama watakuambia hiyo inamaana gani.
Au kama huna watu wa aina hiyo omba msaada wa AI.




Unafikiri hiyo inamaanisha nini?
Vita sio tuu kurusha makombora vita ni akili na mbinu.
Trump anaposema wananchi watoke wapambane wachukue nchi Yao unajua inamaana gani hiyo kisaikolojia na kimedani?

Unafikiri kwa nini sio Iran inayowaambia wananchi wa Israel waichukue serikali yao?



Sio lazima watumia njia hiyo unayoijua. Mbona wametumia njia ya Anga na wamemuua Mkuu wa nchi kwa pigo Moja?

Embu eleza kama Mkuu wa nchi anapigwa kwa pigo Moja. Nani mwingine mwenye ulinzi au nguvu zaidi yake?


Iran pekeake hawezi Mkuu. Hilo hata wao wanajua
Bila Msaada wa Urusi na China Iran hii Ngoma ameshaelekea kibla.

Marekani na Israel wenyewe wanaanza vita wakiwa mbali, wanakupiga kabla hawajafika.

Kadiri wanavyosogea ndivyo wanavyokushinda. Usishangae Urusi anamzuia. Urusi anajua hizo mbinu.

Mimi ndio ningekuwa Ayatollah au Iran nikijua kabisa mechi napoteza ningeshafanya maamuzi mapema. Zile Ceasefire Yale ni Makosa ya Iran. Asingekubali.

Najua wengi hawaoni ni kwa namna ipo Iran imeshashindwa lakini kimedani na kivita Game Over.

Kumua Rais au mkuu wa majeshi sio Jambo la kuota au kubahatisha. Ni mchakato unaohitaji mambo mengi Sana.

Fikiria sasa hivi usikie Iran imetuma kombora limemuua Benjamin Netanyau unafikiri itakuwa ni Jambo rahisi?
Unajua wewe kwenye haya masuala ufahamu wako ni mdogo.

Kwa ujumla vita hupimwa kwa njia mbili kuu: Mosi, kwa malengo yake kutimia, na hapa huwa kwa mtizamo wa kisiasa au kijeshi. Mara nyingi kwa msingi huu vita hupimwa kwa; Je, malengo ya kisiasa yalifikiwa? Je, eneo au mamlaka waliyoyahitaji yalipatikana? Je, adui alisalimu amri?

Kwa mfano, katika WW2, washirika walihesabiwa washindi waliangusha utawala wa Hitler na Japan, hivyo kufanikisha lengo lao la kumwangusha. Katika kumwangusha huku walikufa sanaaa. Lakini lengo la vita lilitimia.

Wewe unachukulia kuuawa kwa kiongozi mkubwa wa nchi au wakubwa jeshini ni kama ushindi, nakushangaa! kwa sababu wewe unajiita mtu wa fasihi halafu historia hujui hali ya kuwa historia imethibitisha kuwa ukiua kiongozi ni tukio la kimkakati, siyo hitimisho la vita.

Kuuliwa kwa Ayatollah kwa mbinu za kijeshi inaitwa "decapitation". Lengo ni kuvuruga amri na udhibiti (command and control), kushusha morali ya wanajeshi, kusababisha mgawanyiko wa ndani na kuharakisha kusalimu amri.

Lakini inafanya kazi lini? Mbinu hii huwa ina mafanikio zaidi kama mfumo wa adui unategemea sana mtu mmoja (utawala wa mtu mmoja). Aidha, ikiwa hakuna mpango madhubuti wa kurithisha uongozi. Halikadhalika, jeshi la adui halina muundo thabiti.

Hii mbinu huwa inashindwa ikiwa kama; Mosi, kuna safu ya uongozi iliyoaandaliwa. Pili, Itikadi ni kali kuliko mtu binafsi. Tatu, Kifo cha kiongozi kinageuzwa propaganda ya kuhamasisha zaidi vita. Vita vya kisasa ni vya kimfumo, si mtu au watu pekee.

Inakubidi ufahamu vilevile tactical victory na strategic victory. Tactical victory ni ushindi wa kimbinu, ushindi wa eneo eneo dogo, muda mfupi. Tactical victory inaweza kuonekana kubwa, lakini isibadilishe mwelekeo wa vita. Strategic victory huu ni ushindi unaobadilisha mwelekeo mzima wa vita au kufanikisha malengo ya kisiasa ya vita.

Kilichofanyika kwa Iran ni tactical victory, ambayo pia ni decapitation strategy; yaani kukata kichwa cha uongozi ili kuvuruga mfumo wa adui. Kwa bahati mbaya mfumo wa Iran ni tofauti. Njia pekee inayofaa kwa kuung'oa ni kuingiza askari wa mapigano ya ardhini. Mbali na hapo hakuna chochote kitakachofanyika zaidi ya Marekani na Israel kufanya operesheni maalumu na kisha mchezo umeisha.
 
Unajua wewe kwenye haya masuala ufahamu wako ni mdogo.

Kwa ujumla vita hupimwa kwa njia mbili kuu: Mosi, kwa malengo yake kutimia, na hapa huwa kwa mtizamo wa kisiasa au kijeshi. Mara nyingi kwa msingi huu vita hupimwa kwa; Je, malengo ya kisiasa yalifikiwa? Je, eneo au mamlaka waliyoyahitaji yalipatikana? Je, adui alisalimu amri?

Kwa mfano, katika WW2, washirika walihesabiwa washindi waliangusha utawala wa Hitler na Japan, hivyo kufanikisha lengo lao la kumwangusha. Katika kumwangusha huku walikufa sanaaa. Lakini lengo la vita lilitimia.

Wewe unachukulia kuuawa kwa kiongozi mkubwa wa nchi au wakubwa jeshini ni kama ushindi, nakushangaa! kwa sababu wewe unajiita mtu wa fasihi halafu historia hujui hali ya kuwa historia imethibitisha kuwa ukiua kiongozi ni tukio la kimkakati, siyo hitimisho la vita.

Kuuliwa kwa Ayatollah kwa mbinu za kijeshi inaitwa "decapitation". Lengo ni kuvuruga amri na udhibiti (command and control), kushusha morali ya wanajeshi, kusababisha mgawanyiko wa ndani na kuharakisha kusalimu amri.

Lakini inafanya kazi lini? Mbinu hii huwa ina mafanikio zaidi kama mfumo wa adui unategemea sana mtu mmoja (utawala wa mtu mmoja). Aidha, ikiwa hakuna mpango madhubuti wa kurithisha uongozi. Halikadhalika, jeshi la adui halina muundo thabiti.

Hii mbinu huwa inashindwa ikiwa kama; Mosi, kuna safu ya uongozi iliyoaandaliwa. Pili, Itikadi ni kali kuliko mtu binafsi. Tatu, Kifo cha kiongozi kinageuzwa propaganda ya kuhamasisha zaidi vita. Vita vya kisasa ni vya kimfumo, si mtu au watu pekee.

Inakubidi ufahamu vilevile tactical victory na strategic victory. Tactical victory ni ushindi wa kimbinu, ushindi wa eneo eneo dogo, muda mfupi. Tactical victory inaweza kuonekana kubwa, lakini isibadilishe mwelekeo wa vita. Strategic victory huu ni ushindi unaobadilisha mwelekeo mzima wa vita au kufanikisha malengo ya kisiasa ya vita.

Kilichofanyika kwa Iran ni tactical victory, ambayo pia ni decapitation strategy; yaani kukata kichwa cha uongozi ili kuvuruga mfumo wa adui. Kwa bahati mbaya mfumo wa Iran ni tofauti. Njia pekee inayofaa kwa kuung'oa ni kuingiza askari wa mapigano ya ardhini. Mbali na hapo hakuna chochote kitakachofanyika zaidi ya Marekani na Irani kufanya operesheni maalumu na kisha mchezo umeisha.

Sasa unafikiri Trump anapowaambia wananchi wachukue nchi yao unafikiri anamaanisha nini?
 
Hizo bases za US zilizopigwa zilikuwa zina radars na vyombo ambapo vilitumika kutoa early warning hadi Israel.
Walitengeneza Integrated Air and Missile Defense (IAMD), Iran ikirusha makombora, tayari Qatar inaona, Kuwait, Bahrain n.k... hivyo wanafanya radar data sharing ama wana link na radar za Israel, hivyo Israel wanapata taarifa kuna missiles zipo njiani.

Kwa jinsi hali ilivyo, Israel itaharibiwa vibaya, na Iran imeamua kufa na Israel, hata waarabu wengi hapo wana kinyongo kuhusu Gaza bado, hata Qatar watakaa kimya.

Ndio maana Iran kwa hasira anatandika hizo kambi na anapiga si mchezo, maana hizo nchi walifahamu wanatumika na US na walikaa kimya.

Tel Aviv inaharibiwa vibaya kabla hata masaa 48 hayajafika, ni majanga makubwa.
mashehe ubwabwa kwa kujiamini mpo vizuri na hicho ndicho kinachowaponza
 
Inategemea na jamii na jamii, kuna jamii Kufa kwenye vita ni status.

just imagine kuna watu watoto wao, ndugu zao na jamaa zao wanakufa vitani ila wakiangalia viongozi wao wanakula Tu mema ya Nchi,

Ila unapoona kiongozi wako yupo mstari wa mbele na yupo tayari Kufa kwa ajili yako inakupa morale na wewe unajitolea kwa Moyo wote.

Mashia ni nut case, huyu khamenei alikua ni mpole na kazuia mambo mengi Sana, ila akiingia hardliner wa Jeshi hapo juu patachafuka mno hapo.
Jamaa mnajua kunifariji kweli nyie. Aiseeeee
 
We jamaa bhana, video ya kwanza kabisa hapo ni IRAN, tena ni Tehran mji wao mkubwa
Acha kudanganya watu Kuanzia Iraq, Iran, Pakistan Hadi India kuna maandamano makubwa kumlilia Ayatollah.

Hii Iran, unambie kuna kiumbe kilitoka nje hapa kupinga? Tena ndani ya Iran utembee na bendera ya Israel? Kadanganye chekechea huko.

 
Pasi na shaka ni sahihi Iran yuko vizuri.
Kuna mtu angetegemea kama Iran atashambulia kambi zote za USA mashariki ya kati!??
USA amepata hasara ya vifo vya askari wake kila nchi aliyoweka kambi middle east.
Na sasa anadai vita kwake imeisha na anaikataza Iran isiendelee na mashambulizi.
Atakaehoji uwezo wa Iran nitamuona hatumii akili vizuri.
Leta habari za uwakika hapa usite propaganda, sema wamekufa askari wangapi. Yaani mtu anakuja kukuzingira kwako na mameli ya kivita na anauwa kiongizi mkuu nchi na viongizi top wa ulinzi unashindwa kushambulia meli unaenda kupiga kambi ambazo makimbira enyewe wana ya intersect.
 
Mkuu unafuatilia kinachoendelea Tel Aviv, Tel Aviv inawaka moto...:FIRE::elmoFire:..

Kwa haya mashambulizi ikipita siku 10, Tel Aviv inakuwa Gaza..
iran anashambulia apartments tel aviv na hoteli za dubai.. yeye anachapwa strategic sites
 
Back
Top Bottom