Robert Heriel Mtibeli
Platinum Member
- Mar 24, 2018
- 40,153
- 93,069
Nimegundua kweli wewe ni mtu wa fasihi, huna ufahamu wa mambo ya kiusalama na geopolitics.
Kwa mfumo wa uongozi wa Irani jinsi ulivyo hii vita itategemea na aina yaAyatollah watakayempata. Vita bado ni mbichi.
Vita mbichi kiongozi wa juu anapigwa kirahisi. Hivi unafikiri sawasawa kweli?
Tafuta wanajeshi au watu wa usalama watakuambia hiyo inamaana gani.
Au kama huna watu wa aina hiyo omba msaada wa AI.
Trump na Netanyahu wametoa tamko kwa raia wa Iran wajitokeze wapambane na serikali yao lakini ni kama Iran wameziba masikio.
Unafikiri hiyo inamaanisha nini?
Vita sio tuu kurusha makombora vita ni akili na mbinu.
Trump anaposema wananchi watoke wapambane wachukue nchi Yao unajua inamaana gani hiyo kisaikolojia na kimedani?
Unafikiri kwa nini sio Iran inayowaambia wananchi wa Israel waichukue serikali yao?
Njia pekee ya kuuangusha utawala wa Iran ni kuingiza wanajeshi ardhini. Mbali na hapo hakuna matokeo yoyote watakayoyapata labda kumuua Khomein.
Sio lazima watumia njia hiyo unayoijua. Mbona wametumia njia ya Anga na wamemuua Mkuu wa nchi kwa pigo Moja?
Embu eleza kama Mkuu wa nchi anapigwa kwa pigo Moja. Nani mwingine mwenye ulinzi au nguvu zaidi yake?
Kwa usiku wa jana Israel na Marekani hawakufanya shambulizi hata moja. Kuanzia saa 2 usiku hadi saa 8 Iran imefanya mashambulizi makubwa sana non stop bila ya kuwa na uongozi. Hofu yangu inakuja ni aina gani ya kiongozi watakayempata: Wakimpata laini ambaye viatu havimtoshi utakuwa ni ushindi wa Marekani na Israel. Ikiwa wakimpata mgumu hakutokuwa na mabadiliko yoyote-Again, njia sahihi ni kuingiza wanajeshi ardhini.
Iran pekeake hawezi Mkuu. Hilo hata wao wanajua
Bila Msaada wa Urusi na China Iran hii Ngoma ameshaelekea kibla.
Marekani na Israel wenyewe wanaanza vita wakiwa mbali, wanakupiga kabla hawajafika.
Kadiri wanavyosogea ndivyo wanavyokushinda. Usishangae Urusi anamzuia. Urusi anajua hizo mbinu.
Mimi ndio ningekuwa Ayatollah au Iran nikijua kabisa mechi napoteza ningeshafanya maamuzi mapema. Zile Ceasefire Yale ni Makosa ya Iran. Asingekubali.
Najua wengi hawaoni ni kwa namna ipo Iran imeshashindwa lakini kimedani na kivita Game Over.
Kumua Rais au mkuu wa majeshi sio Jambo la kuota au kubahatisha. Ni mchakato unaohitaji mambo mengi Sana.
Fikiria sasa hivi usikie Iran imetuma kombora limemuua Benjamin Netanyau unafikiri itakuwa ni Jambo rahisi?