Kwa kweli watanzania uwezo wetu wa kuchanganua huwa ni wa kipekee sana.
Tatizo la kwanza ni kuwa biased hata kwa vitu vya kawaida.
Siasa za mashariki ya kati nazielewa kwa sehemu kubwa, na nilishaandika nyuzi humu.
Hivyo usije fikiria una deal na mtu asieelewa nini kinaendelea.
12 Days war aliyeomba cease-fire ni Israel kupitia kwa US.
Iran inaweza kupigwa kweli na ikavumilia, lakini Israel haina uvumilivu huo, mitaa inapigwa na watu wanakufa, hili linapelekea ku pressure serikali isimame vita.
Tujipe muda. Nadhani inabidi utathmini uwezo wako wa kuchanganua mambo si mimi.
Trump si ndiye kaanzisha vita na Israel, si wana hasira sana na wanataka regime change, iweje aanze tena kuonyesha nia ya kuwasikiliza Iran?
Kama Iran imekuwa weak kwanini wasiishambulie kwa nguvu zaidi na kuangusha uongozi wa Iran?
Kwa sababu US na Israel wameona hawaendi kufanikiwa zaidi ya hasara, kuepuka aibu anaanza kuwaandaa watu kisaikolojia kwamba Iran imepigwa hadi inakubali mazungumzo.
Na niliandika humu kama kutabiri Trump atafanya hivyo.