Israel yaishambulia Iran, milipuko yasikika katika mji mkuu wa Tehran

Ni nini kimeiuzi Israel hadi kuishambulia Iran???
Kosa la Iran liko wapi??
Iran aliapa kuifuta Israel kwenye ramani ya dunia, alianza kwa kusapoti makundi ya kigaidi matatu ambayo ni Hamas, Al Fatah na Hezbollah kuipiga Israel na wakati huo akitengeneza bomu la nuclear kuipiga Israel, usalama wa Israel uko kwa kuidhibiti Iran aliyeapa kuiharibu Israel, hilo ndio analofanya Israel kwa sasa.
 
Mbona kama Israel amekuwa mbabe wa Middle East kirahisi hivi! Anapiga popote akijisikia...ni mchokozi sana!
 
Hii ngoma ilikuwa ya kustukiza kumbuka Iran bado ilikuwa kwenye mudi ya mazungumzo Israel katumia chansi hio ku attack
Hadi Trump alishasema hilo, ww unakuja kusema n ya kushtukiza 😂 Wabongo bhana au unadhani Trump/USA ni sawa na viongozi wako wa Bongo maneno mengi ila hakuna vitendo?
 
Iran hawezi kulipiza ,kila site ya Israel ambazo ni core kuna base ya USA na US kasema zikiguswa tu basi anaingia mazima ...Hapo hawezi kufanya chochote kile.
 
Niliwahi sema hii kitu itatokea ila kuna mwanajamii alinipinga sana kuhusu hili
List ya Israel imeisha kwa sasa maana alibakia Iran pekee
 
Hapo jua kwamba kuna mashindano ya kielimu na fikra,hivi haviwezi kufa,,vitaendelea kubaki nakutengeneza teknolojia mbalimbali,jiulize tangu waanze kuua wanasayansi wa Irani ni lini??,, Ni kwamba wanaendelea kuzaliwa na kubuni pia mipango endelevu,,.
 
Ww unaishi Tz ndo mana unaona n jambo la kushtukiza labla kwakuwa hufatilii, Ila wahusika walikuwa wana taarifa hadi Trump alishaliongelea hili, sasa ww unasemaje n ya kushtukiza?
Iran ilizuia ndege zake kuruka ? Kama aikufanya chochote wewe jua kuwa mifumo yao ya ulinzi iliwekwa low level na manual .....usifanye mchezo na mifumo ya ulinzi inapokuwa katika automatic high level attack inapiga hadi decoys zinazo ruka angani ...ndiyo maana mrusi urusha decoys nyingi ukrain.
 
Hapo Iran alizubaa vibaya lakini amin mkuu marekani kahusika kwa asilimia kubwa pia wanapo shambulia wahakikishe wana piga na site za makombora ya masafa marefu la sivyo kitawaka
US ina maslahi makubwa na middle East na hawapo tayari kutoka hayo maeneo leo ama kesho, uchumi wa dunai upo pale, hii ndio ilipelekea Trump akawa hana budi zaidi ya kuomba amani na Houthis.

Kwa kilichotokea US kusaidia hili kutokea na kukana kinafiki, proxis wa Iran wapewa silaha na missiles hatari kushambulia bases za kijeshi za US hapo middle East huku Iran na yenyewe ikikana kutohusika..
 
Mbona tangu kitambo yeye n mbabe wa middle east, Au lini uliwahi kumuona amekaa kinyonge?
Yaani anapiga popote akijisikia, japo najua anapata nguvu ya USA pia. Ila kuzungukwa na muarabu kwake ni changamoto sana, atakuwa anapigana nao hadi kiama....Waarabu na Persians watawasumbua sana.
 
Hivi Waisrael wana nini? Kila siku wako vitani! Raia wao wana wakati mgumu sana, kila wakati ni milio na tahadhari.
Kazi yao ni kubomoa,kuharibu, Kujenga na kupanda. Wameumbiwa hayo LAZIMA yaonekane kimwili lakin ukisoma bible ni hivo TU mpera mpera
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…