Israel yajibu mashambulizi dhidi ya Iran. Yashambulia Iran, Syria na Iraq

Israel yajibu mashambulizi dhidi ya Iran. Yashambulia Iran, Syria na Iraq

Serikali ya Iran imesema haijaona mashambulizi yoyote badala yake imezima majaribio ya drone za Israel tatu kwa kuzidungua kabla hajazijaleta madhara nchini mwake

=====

1713519554779.png

Vyombo vya habari vya Serikali nchini Iran vimesema kuwa mfumo wa ulinzi wa anga wa nchi hiyo uliangusha ndege tatu zisizo na rubani (droni) katika Mji wa Isfaha usiku wa kuamkia leo Ijumaa Aprili 19, 2024.

Taarifa hiyo imetolewa saa chache baada ya vyombo vya habari vya Marekani, vikiwanukuu maofisa wakuu wa Marekani, kuripoti kuwa makombora ya Israel yamepiga eneo la Iran.

Tovuti ya Aljazeera imesema kuwa televisheni ya Taifa ya Iran iliripoti kutokea kwa milipuko katika Mji wa Isfahan, ambapo mfumo wa ulinzi wa anga ukiyazuia, huku safari za ndege katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na Tehran na Isfahan zikisitishwa.

Ajazeera imeripoti kuwa anga la maeneo hayo lilifunguliwa kwa takriban saa nne na nusu baada ya tukio hilo na hakukuwa na ripoti za majeruhi.

Awali tovuti ya ABC ilimnukuu Ofisa Mkuu wa Marekani, kwamba Israel ilirusha makombora katika eneo moja nchini Iran. Habari za CBS pia ziliripoti kwamba shambulio hilo limeikumba Iran.

Israel iliahidi kujibu mashambulizi baada ya Iran Jumamosi iliyopita kurusha droni za makombora nchini humo.

Msemaji wa Shirika la Anga za juu la Iran, Hossein Dalirian alisema ndege kadhaa zisizo na rubani zimetunguliwa kwa mafanikio.

"Hakuna ripoti za shambulio la kombora kwa sasa," Dalirian alisema kwenye mtandao wa kijamii wa X.

Isfahan ni jiji muhimu kimkakati pia upo karibu na mji wa karibu Natanz ambalo ni eneo la lenye nyuklia ya Iran.

Mwananchi
 
Wote tunajua Ayotollahs ni mabingwa wa kukanusha hata kama wamepigwa🤔
......
Sasa unabisha nini na kukubali nini!?
Shambulio la Israel limefeli,nia yao ilikua kulipua Nuclear facility hapo Isfahan ila wakafeli makombora yakalipuka maeneo jirani na hapo na drone tatu zimedunguliwa za Israel.
 
Ayatollaah lazima Israel imvue dela, kilemba na kumkata ndevu chafu zile, mtaona
 
Iran yupo na sehemu nyingi za kubonyeza.
Akibonyeza hapa 👇 👇 👇 (Strait of Hormuz) Israel atasemaje? Karibia mafuta yote duniani yanapitia hapa

1713518969097.png
 
Eeh Mwenyezi Mungu njoo utunusuru waja wako
Maana wanadamu wamemaliza kuilima nchi sasa wameanza kulimana🙏
 
Hawezi kukubali kwa sababu zifuatazo:
1. Kuipa Israel anga ya Saudia ili ikapige Iran kutatafsiriwa sawa na Saudia kuiunga mkono Israel na vitendo vyake kule Gaza.
2. Iran italipiza kwa kurusha makombora ndani ya Saudia


Hapana, Saudia kapata madhara makubwa sana sbb ya Iran na Houthis, so Saudia ni adui mkubwa sana na Iran kama ulikuwa hujui, so vita vikianza anaweza mpe anga lake akapigwa Iran haraka sana, kwani Iran ndio adui namba moja wa Saudia
 
Hata mimi imeniwia vigumu kunielewa na kuikubali Ile kauli ya USA Hali ya kuwa kasogeza meli za kivita karibu na uwanja wa mapambano
USA hawez huacha israel apotee hata siku mojaaa, ataingia tu sijui kuna siri gani ya urafiki wa izi nchii, putin huu urafiki nae hauelewi
 
Iran yupo na sehemu nyingi za kubonyeza.
Akibonyeza hapa [emoji116] [emoji116] [emoji116] (Strait of Hormuz) Israel atasemaje? Karibia mafuta yote duniani yanapitia hapa

View attachment 2968137
Dunia ina wenyewe!

Na wenyewe ndio wanapamilili hapo Hoimuz.

Akijaribu ndio atachochea moto wa kukiona
 
Back
Top Bottom