Israel yajibu mashambulizi dhidi ya Iran. Yashambulia Iran, Syria na Iraq

Mnatia aibu, Israel kawapa nini mmutukuze hivo? Mtu mweusi kwa Israel ni uchafu...watu wa ajabu Sana ninyi na Imani zenu za kinaskini.
Kwani wewe Iran kakupa nini hadi mkihisi Israel anatukuzwa mnachafukwa kiasi hicho? Mbona mimi sijaona popote kama huyo uliyemjibu anaitukuza Israel?
 
Hayo ni maneno ya serikali ya Iran kujifariji na kuwatuliza raia wake, taarifa zisizoegamia upande wowote zinasema miji saba ya Iran imepokea kichapo cha makombora ya chap chap na miundo mbinu kuteketea.
 
Hakuna cha vita mbaya wala nini, Iran anakwenda kuchakazwa na dunia itaiomba Israel itulize mzuka.
Mkuu hebu nidadavulie kidogo nyuma ya maneno yako kuna maelezo gani ya kufanya dunia iamini hivyo......ukizingatia Iran na wenyewe wamepiga hatua kubwa kiuchumi na kiteknolojia
 
Kuna kila dalili WWW3 inakwenda kuanza rasmi........na mwisho wa Israel unakaribia........kumbuka Amerika ameshasema yeye anakaa kando......
Israel peke yake hana ubavu huo, Amerika ni waongo, wapo nyuma ya mashambulizi haya wakishirikiana na NATO yote pamoja na vibaraka wao wa mashariki ya kati.
 
Tukiangalia mgogoro unavyokuwa na waliopo kwenye mgogoro huo nyuma yao kuna kina nani.......lakini pia eneo la mashariki ya kati liko eneo zuri kimkakati katika uchumi wa dunia ukizingatia bidhaa adimu unatoka hapo........
 
Israel pke yake hana ubavu huo, amerika ni waongo, wapo nyuma nyuma ya mashambulizi haya wakishirikiana na NATO yote pamoja na vibaraka wao wa mashariki ya kati.
Najua USA sio mtu wa kumuamini linapokuja suala la Israel.....
 
Hawa watu wasituaribie dunia wakatuingiza kwenye ww3.
Hizi nchi zetu za chini tutakula msoto ambao haujawahi tokea.
 
Tukiangalia mgogoro unavyokuwa na waliopo kwenye mgogoro huo nyuma yao kuna kina nani.......lakini pia eneo la mashariki ya kati liko eneo zuri kimkakati katika uchumi wa dunia ukizingatia bidhaa adimu unatoka hapo........
Mkuu, baada ya ngano kuadimika sisi huku siku hizi tulisha sahau kama ngano ni hadimu au laah, siku hizi matumizi ya unga wa ngano yameshakuwa replaced na unga wa mihogo. Kuanzia chapati, mikate, maandazi tunatumia unga wa mihogo tu.
Hivyo kama issue ni uadimu wa bidhaa zitokazo pale, basi jua tayari dunia ina altenative na huenda hata hiyo vita inachochewa ila hiyo altenative product iingizwe sokoni.
 
Hawa watu wasituaribie dunia wakatuingiza kwenye ww3.
Hizi nchi zetu za chini tutakula msoto ambao haujawahi tokea.
Hayo ni Mawazo ya kila mwenye akili timamu.....ndugu yangu.....hili jambo sio la kuombea
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…