Israel yajibu mashambulizi dhidi ya Iran. Yashambulia Iran, Syria na Iraq

Israel yajibu mashambulizi dhidi ya Iran. Yashambulia Iran, Syria na Iraq

Israel sijakuzoea hivi picha na video mpaka sasa zakutafuta kwa tochi.Peleka makombora Tehran tuone majivu.Vinginevyo naungana na wote wanaodai Iran ni maji ya shingo kwako.Mpaka itakapotangazwa vinginevyo.
 
Israel wameanza kupiga Kwanza rada zilizopo Iraq na Syria huku ndege zingine zikipiga site 7 za Iran pia kulikuwa na cyber attack nchini Iran ili iwe rahisi kupiga..inaonekana mawasilianao ya kuchunguza hatari hayakufanya kazi

Israel news channel wanasema target zao zimefanikiwa Kwa 99% na Iran wanasema hakuna kilchofanyika ndani ya nchi Yao.
 
Sikiliza vyombo vya ndani ya Iran kwanza, BBC na Aljazeera watakuja baadaye.
Halafu imekuaje leo "bibisii" kimekuwa chombo cha habari cha uhakika?🤣
Lile shambulio la Iran lilikuwa kama makokbora ya abiria au mapokezi ya ndege mpya. Dunia nzima ilikuwa inashuhudia tangu yanafyatuliwa.
Ila hili la Israel watu wanasikia vilio tu, vinatokea nchi fulani huku wakilalamika kupigwa. Israel mwenyewe hasemi kitu ndiyo kwanza anaendelea na mambo yake.
 
Sikiliza vyombo vya ndani ya Iran kwanza, BBC na Aljazeera watakuja baadaye.
Halafu imekuaje leo "bibisii" kimekuwa chombo cha habari cha uhakika?🤣
wanakataaa kwa maslahi yao.. Vipo biased
 
Kuna kila dalili WWW3 inakwenda kuanza rasmi........na mwisho wa Israel unakaribia........kumbuka Amerika ameshasema yeye anakaa kando......
Nduguuu yangu Hadi unashindwa kutambua mbinu za marekani? Kumbuka Israel hawezi kufanya Jambo bila USA na allies wake ..
Marekani kaongea vile ili Russia na china wasiunge mkono Iran Ila hata haya mapigo Kwa Iran ymeendeshwa na America wenyewe
 
Nchi kama Tanzania huwa hazijifunzi, so kusalimika ni ngumu, ila kama ingekuwa ni nchi inayojielewa na watu wenye vichwa ambao vichwani zina chaji, basi migogoro ya hivi ingekuwa ni fursa ya kuiimarisha nchi na kuipeleka kwenye kundi la nchi zilizoendelea.
Ila kwa sasa ni lazima ziathirike kuliko nchi zinazopigana.
Nchi za kiafrika zimeshaona msaada ya bajeti za serikali zao ni haki yao
 
Iran ana mikwara mingi lakini hana ubavu wa kuendesha vita kubwa, nzito na muda mrefu kwa sababu hizi.
1. Ana matatizo makubwa mnoo ya kisiasa ndani ya taifa lake.
2. Hana uungwaji mkono kutoka taifa lolote kubwa lenye nguvu ya kijeshi.
3. Waarabu wanaomzunguka mpaka sasa wameshindwa kumuunga mkono.
4. Israel ina uungwaji mkono mkubwa kutoka mataifa makubwa ya kivita na wanaomzunguka.
Mbona naona kama Russia ni mdau mkubwa wa Iran..... unadhani anaweza kumuacha peke yake akichanwa chanwa na MAKOMBORA ya Israel ukizingatia Russia ni miongoni mwa mataifa yenye nguvu kubwa za kijeshi
 
Shirika la habari la Mehr news agency lenye usuhuba na serikali ya Iran limesema mji wa Isfaham uko salama kabisa na watu wanaendelea na shughuli zao kama kawaida.
Wakionesha msongamano wa magari mapema asubuhi yanayoelekea kazini,shirika hilo limesema sauti za miripuko iliyosikika mapema kabla ya hapo ilikuwa ya droni zilizodondoshwa na mifumo ya ulinzi ya nchi hiyo.
 
Nduguuu yangu Hadi unashindwa kutambua mbinu za marekani? Kumbuka Israel hawezi kufanya Jambo bila USA na allies wake ..
Marekani kaongea vile ili Russia na china wasiunge mkono Iran Ila hata haya mapigo Kwa Iran ymeendeshwa na America wenyewe
Nilikuwa natambua na kujua unafiki wa US hasa linapokuja suala la Israel....... nilijaribu Tu kuliweka hapa ili kukaribisha mawazo mbaadala na kuboresha majadiliano
 
Back
Top Bottom