Israel yajibu mashambulizi dhidi ya Iran. Yashambulia Iran, Syria na Iraq

Israel yajibu mashambulizi dhidi ya Iran. Yashambulia Iran, Syria na Iraq

Israel sijakuzoea hivi picha na video mpaka sasa zakutafuta kwa tochi.Peleka makombora Tehran tuone majivu.Vinginevyo naungana na wote wanaodai Iran ni maji ya shingo kwako.Mpaka itakapotangazwa vinginevyo.
Israel haina uwezo huo kwa sasa. Kwenye lile shambulio la Iran walitumia USD3.5bn ndani ya usiku mmoja. Vipi vita vikichukua mwezi?
 
Hahahaha moderators kama kawaida yao, siku hizi wana attack watu wanaoandika thread za kuishambulia Israel. Baada ya kuona thread niliyoandika inaiacha uchi Israel na wengi wanaonekana kuunga mkono na ku Like nilichoandika. Sasa wamekuja na uamuzi wa kuunganisha uzi wangu kwenye uzi mungine.

Jana niliandika mungine wakakimbia kuutupa katika jukwaa la Rwanda forum 😂😂😂
Hii hali ya uonevu na kuchagua thread za kuandika kuna siku itaisha tu. Maana hili shambulio la leo kuna thread kibao tu zimeandikwa na hazikuunganishwa maana zimeandikwa na wanao support Israel, ila ya kwangu ya kuponda kashambulio ka Israel ndo imetafutiwa sehem ya kupachikwa ili kuifichia huko na alieandika asijulinae 😂😂😂.

Hii ndio JF tulionayo sasa hivi.
Acha bangi, sasa mada yako inautofauti gn na hii mada ilipounganishwa.?
 
Israel karudisha heshima yetu... 🤣 🤣

Wavaa kobazi walianza kutamba sana...

Yaani Israel imenipunguzia muda wa kukaa online kufatilia lini watashambulia
Picha au video tafadhali
 
Iran ana mikwara mingi lakini hana ubavu wa kuendesha vita kubwa, nzito na muda mrefu kwa sababu hizi.
1. Ana matatizo makubwa mnoo ya kisiasa ndani ya taifa lake.
2. Hana uungwaji mkono kutoka taifa lolote kubwa lenye nguvu ya kijeshi.
3. Waarabu wanaomzunguka mpaka sasa wameshindwa kumuunga mkono.
4. Israel ina uungwaji mkono mkubwa kutoka mataifa makubwa ya kivita na wanaomzunguka.
Mkuu hujui lolote na unapotosha. Iran kapigana na Iraq ya Saddam Hussein iliyokuwa inaungwa mkono na Marekani na nchi zote za magharibi pamoja na majirani kama Saudia, Kuwait UAE na wengineo kwa miaka minane kuanzia 1980 hadi 1988 na technically alishinda ile vita. Nikujibu yafuatayo:
1. Iran hawana matatizo makubwa mno ya kisiasa ndani ya nchi yao. Kama yapo yataje.
2. Iran anaungwa mkono na Urusi na China. Tena Iran ni msambazaji mkubwa wa silaha anazotumia Urusi kule Ukraine zikiwemo Shaheed 136 drones ambazo zinasumbua sana Ukraine.
3. Hakuna hata mwaka mmoja Waarabu waliwahi kuiunga mkono Iran. Ukiachilia mbali masuala ya kiitikadi Waarabu na Waajemi walikuwa maadui wa jadi. Hata kwenye vita vya Iran na Iraq Waarabu wote walimuunga mkono Saddam Hussein. Kwahiyo hoja yako haina mashiko
4. Hayo mataifa makubwa yanayomuunga mkono Israel hayako tayari kwa vita nyingine kubwa. Vita ya Ukraine imewafilisi na mpaka sasa wanashindwa hata kutuma silaha na Zelensky kutwa anapiga kelele apewe fedha na silaha lakini hapati. Juzi shambulizi la Iran limeigharimu Israel USD 3.5BN ndani ya usiku mmoja tu. Vipi kama vita ikipiganwa mwezi mzima?
Usiandike tu kwa mihemko ya kiimani. Check your facts before writing.
 
Inawezekana ni mpango kabambe wa siku nyingi..... Iran anatakiwa kuwa makini katika hili
Tangia Israel ishambuliwe Netanyau amekuwa akishiriki vikao na Baraza lake la ulinzi huku mataifa ya magaribi yakifuatilia moja kwa moja through E-Conference na kama unazielewa siasa za kimataifa na ugomvi unaoendelea kati ya East na West, jiulize kwanini Israel kamshambulia Syria pia? Maanaake anataka kumhusisha Urusi kwenye mgogoro huu ambaye ana mutual military assistance na Syria. Mambo ni mengi mazuri na mabaya yanakuja mkuu. 3WW ipo njiani
 
Mkuu hujui lolote na unapotosha. Iran kapigana na Iraq ya Saddam Hussein iliyokuwa inaungwa mkono na Marekani na nchi zote za magharibi pamoja na majirani kama Saudia, Kuwait UAE na wengineo kwa miaka minane kuanzia 1980 hadi 1988 na technically alishinda ile vita. Nikujibu yafuatayo:
1. Iran hawana matatizo makubwa mno ya kisiasa ndani ya nchi yao. Kama yapo yataje.
2. Iran anaungwa mkono na Urusi na China. Tena Iran ni msambazaji mkubwa wa silaha anazotumia Urusi kule Ukraine zikiwemo Shaheed 136 drones ambazo zinasumbua sana Ukraine.
3. Hakuna hata mwaka mmoja Waarabu waliwahi kuiunga mkono Iran. Ukiachilia mbali masuala ya kiitikadi Waarabu na Waajemi walikuwa maadui wa jadi. Hata kwenye vita vya Iran na Iraq Waarabu wote walimuunga mkono Saddam Hussein. Kwahiyo hoja yako haina mashiko
4. Hayo mataifa makubwa yanayomuunga mkono Israel hayako tayari kwa vita nyingine kubwa. Vita ya Ukraine imewafilisi na mpaka sasa wanashindwa hata kutuma silaha na Zelensky kutwa anapiga kelele apewe fedha na silaha lakini hapati. Juzi shambulizi la Iran limeigharimu Israel USD 3.5BN ndani ya usiku mmoja tu. Vipi kama vita ikipiganwa mwezi mzima?
Usiandike tu kwa mihemko ya kiimani. Check your facts before writing.
U.s amekaa afganstan miaka 20 sembuse hio ya ukraine na israel ambayo hana wanajeshi wanaopigana direct acha uongo
 
Score board inasoma ISR 2:IRN 0
kwanini;
1. Israel ndo alienzisha ugomvi kwa kuua maafisa 7 wa Iran WHILE Iran hajaua mtu yeyote iwe kwa bahati mbaya au kwa makusudi zaidi ya kumchubua mtoto wa miaka 9 tu.
2. Iran katika kumjibu Israel alituma drones 300+ bila kuwa na target yoyote ile ya msingi yaani alirusha randomly itayompata na impate(huu ni ujinga wa hali ya juu kwa jeshi kama Iran),walichofanya ni kuonesha wa silaha nyingi kwenye ghala na wanaeza hata kuzichezea au walimisi kurusha kwa masafa? au show off ?au hawana shabaha? Au hawakuwa na uchungu na makanda wao walokufa? Au ndo kutuma meseji(🤣🤣) WHILE Israel katuma drones katika majimbo 7 muhimu yanahusu nyuklia,na angalau 3 katika jimbo Isfahan ambazo zilitunguliwa vizuri,hapa Israel anatuonesha kuwa hana silaha za kuchezea na anajua point za kutarget💪💪
3. Iran alirusha drones zake kutokea nyumbani kwake WHILE Israel kaenda kuzidondoshea kwenye Anga hilo hilo la Iran,maana yake anga lake ni penetrable au makanda walisinzia kudili na rada🤔🤔
4. Iran alitumia wiki 2 kujibu mashambulizi ya vifo vya makamanda wake While Israel katumia less than a week tu(hiyo inaitwa,I WAS BORN READY)
5 Iran ilivyopiga drones zake ikajitangaza kuwa kafanya umwamba sana na akijibiwa ataongeza kubwa zaidi ya hilo WHILE Israel baada ya shambulio lake kasema shambulio lake ni dhaifu sana🤔🤔,hapa watu waanaamini Israel kaonesha udhaifu sana,la hasha,Israel Inatambua ukubwa wa Iran kwahiyo lazima atumie akili kubwa kumjaza mtu upepo ajichanganye,maana alisema bwana Nyau kuwa watalipa kisasi kwa faida yao.
Conclusion;
Vita ikitokea Iran atapoteza kwa sababu ana silaha za uhakika na watu wa kutosha ila hana Akili (strategies),kumbuka Ndani ya miaka 75 Israel amepigana na kushinda sababu ya akili(hana watu wala silaha nyingi) na support kutoka magharibi
 
Kama unafikiri huu ndio mwisho wa response ya Israel kwa Islamic Republic huielewi Israel
Serikali ya kislam ya Iran imejaa ma agent wa Israel tegemea matukio mengi hivi karibuni
 
20240419_112729.jpg
 
Back
Top Bottom