Israel yalaani Sweden kuruhusu uchomaji wa biblia ya kiyahudi ya Toraw

Hivi nini kitatokea iwapo nitachoma katiba ya nchi?
Utaitwa kituo Cha polisi kilichokaribu utatrend sana kwenye magazeti yote ya Ndani mpaka nje mpaka kimataifa nadhani watakuchukua mpaka video kabisa taarifa zako zitasomwa kwenye platforms zote za social media utakua gumzo utazungumzwa na kila mtu wapo watakaokucheka wapo watakao tafuta mbinu na namna ya kukutetea, kumbuka ukienda polisi hautorudi kwa kosa ulilofanya utachukuliwa maelezo utawekwa lupango moja kwa moja segedance utakaa huko mpaka kesi yako itakaposomwa utaenda kusomewa kesi ukiwa na utitiri wa wanahabari wengi wanaokuzonga, utaambiwa na kuulizwa na Jaji au Hakimu je! unakubari shitaka lililopo mbele yako au unakana shitaka?! Ukikubari kesi haitochukua mda utachezea mvua ya kutosha ili iwe funzo kwa wengine na utapewa haki yako ya kukata rufaa na ukikana basi utaanza utaratibu wa kukusanya ushahidi kukuthibitishia kua umefanya wewe na sio mwingine, kupitia wewe wengine watajifunza kwanini ni kosa mtu kuichoma KATIBA YA NCHI YAKE
 
Hahahaaa!Na wakati huohuo anasema katika(Yohana 5:45-47)

45Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi. 46Kwa maana kama mngalimwamini Musa, mngeniamini mimi; kwa sababu yeye aliandika habari zangu. 47Lakini msipoyaamini maandiko yake, mtayaamini wapi maneno yangu?.

Sasa wewe unayetenganisha mafundisho ya Musa na Yesu,ni kwamba unapotea.
 
Na wakati huohuo anasema katika(Yohana 5:45-47)

45Msidhani kwamba mimi nitawashitaki kwa Baba; yuko anayewashitaki, ndiye Musa, mnayemtumaini ninyi.
Yesu ni mtetezi na sio mshitaki.
1 John 2 : 1 " My little children, these things write I unto you, that ye sin not. And if any man sin, we have an advocate with the Father, Jesus Christ the righteous "

Shetani ndiye Mshitaki
Ufunuo 12 : 9 - 10 " Yule joka akatupwa, yule mkubwa, nyoka wa zamani, aitwaye Ibilisi na Shetani, audanganyaye ulimwengu wote; akatupwa hata nchi, na malaika zake wakatupwa pamoja naye.
Nikasikia sauti kuu mbinguni, ikisema, Sasa kumekuwa wokovu, na nguvu, na ufalme wa Mungu wetu, na mamlaka ya Kristo wake; kwa maana ametupwa chini mshitaki wa ndugu zetu, yeye awashitakiye mbele za Mungu wetu, mchana na usiku. "

Musa Aliitwa mshitaki kutokana na kubeba Sheria na Amri za MUNGU
Cha kushangaza zaidi hakuweza kuitimiza hiyo sheria . MUNGU Alimwambia auambie mwamba utoe maji , yeye akaupiga mara 3 . Mbaya zaidi aliwaambia wana Israel yeye ndiye atakayewapa maji na sio MUNGU. Na hii ndiyo sababu MUNGU alimuua
 
Roho mtakatifu ni nani?
 
Wiki mbili zilizopita alichoma pia qruani je ulisikitishwa na kitendo hicho?
 
Ngoja tuone kama Wayahudi wataandamana hadi kufa wakilaani Torah yao kupigwa kiberiti
Si wamesema jamaa ka abort his mission? Inawezekana Mungu wa waisrael kabonyeza kitufe kitu alichoshindwa kufanya Mungu wa waislam😂😂
 
Yesu hakufa?.


Na vipi kuhusu mafundisho haya ya Yesu katika Mathayo 5:17-19 ?

17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza. 18Kwa maana, amin,nawaambia, Mpaka mbingu na nchi zitakapoondoka, yodi moja wala nukta moja ya torati haitaondoka, hata yote yatimie. 19Basi mtu ye yote atakayevunja amri moja katika hizi zilizo ndogo, na kuwafundisha watu hivyo, ataitwa mdogo kabisa katika ufalme wa mbinguni; bali mtu atakayezitenda na kuzifundisha, huyo ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
 
Yesu hakufa?
Alikufa na Akafufuka , Na anasubiriwa kurudi mara ya pili kama Masihi
Na vipi kuhusu mafundisho haya ya Yesu katika Mathayo 5:17-19 ?

17 Msidhani ya kuwa nalikuja kuitangua torati au manabii; la, sikuja kutangua, bali kutimiliza.
Kutimiliza = Kukamilisha
Na kitu ambacho hakijakamilika basi kina kasoro.

Yesu hakuja kusema Mzini , Bali aliongezea kuwa ukiwa na mawazo ya ngono wewe tayari ni mzinifu. ( Hiyo ndo maana ya kuikamilisha na sio kuitengua)

Kwa hiyo Musa alikuwa anakasoro , Na Yesu alizirekebisha :
Musa alisema : Wazinifu wa pigwe mawe Mambo Ya Walawi 20 : 10-12 , Torati 22 : 22-24

Yesu akasema : Wazinifu wasiuliwe ,MUNGU ndiye anahukumu
na sio mwanadamu mwenzako
Yohana 8 : 1-11

NB : SOMA KITU KILICHO KAMILIKA , NA SIO CHENYE KASORO
 
Sijui umeandika nini labda hukunielewa nilichomaanisha. Mimi siamini dini. Naamini uwepo wa Mungu bila kupitia dini. Secular-theist me.
THIS IS YOU: DEIST
Deism is a philosophical position that asserts the existence of a higher power or creator but rejects organized religious doctrines and dogmas. Deists typically rely on reason, observation of the natural world, and personal experiences to form their beliefs about God. They tend to view God as a distant, non-intervening entity who set the universe in motion but does not actively participate in human affairs or religious rituals.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…