yaani hata wakipigana hawatusaidii chochote, zaidi sana wataongeza ugumu wa ,maisha baada ya mafuta kupanda. Iran amekuwa gentleman sana kwenye suala hili, baada ya kupiga, ilikuwa ni kama watoto wawili walikuwa wamechokozana akajirudishia akampigia marekani kumwambia nimejirudishia na sina nia ya kuendelea na ugomvi, marekani hakupokea simu, kaenda Qatar ambaye akipiga simu tu marekani anapokea kwa sababu kuna base yake pale, akamwambia naomba mwambie marekani mimi nimeshajirudishia sitaki ugomvi uendelee, of course quatar inaonekana alifikisha meseji, Iran hakuishia hapo, akatuma watu India, ambayo ni rafiki wa Israel akawaambia waishauri israel isijirudishie kwa sababu yeye amejirudishia na hataki waendelee kupigana.
ukweli ni kwamba, nchi zote mbili ni imara sana. iran amechimbia chini ya mahandaki silaha zake nyingi ambazo myahudi anaweza asizilipue hadi aende ground invasion jambo ambalo ni baadaye sana. pia iran alishajipanga kwa mahandaki mengi kupigana na marekani hivyo israel akienda miundombinu ile waliandaa kupigana na marekani itatumika kupigana na israel, na israel itapata shida kumpiga, kwa sababu silaha anazo nyingi. hata vitu vya nuclear vipo ardhini.
iran anaogopa sana kulipuliwa kwa visima vyake vya mafuta, mitambo yake ya kufua umeme na radar zake ambavyo vitambarimu sana, kwa sababu Iran sio taifa tajiri, ni middle income, bado anajikokota hata kama ana mafuta mengi na gas lakini bado sio nchi ya ulimwengu wa kwanza. hivyo hataki kurudishwa nyuma. ila kama wakiingia vita akaamua kujitoa mhanga, ataisumbua sana israel, na hayupo tayari kujitoa mhanga kwa sababu ana uhakika with time israel atampiga tu.
Marekani ana mabom makubwa sana hata ya bunker za kupiga kitu kikiwa chini ya ardhi, na ameweka base nyingi kuizunguka iran, hataiacha salama. labda vita visianze, vikianza tu havitaisha hadi iran iwe Gaza, ndio hofu ya iran. ikianza tu uso kwa uso havita isha hadi iran iwe gaza kwasababu UK, Ufaransa, Ujerumani, NATO yote, Israel, Marekani wataungana na kupigana bila uchumi wao kuteketea ila uchumi wa irani utakuwa unateketea and with time atashindwa hata kuhudumia wanajeshi wake mishahara. ndicho anachoogopa.
kama ni vita ya siku moja au miezi sita, iran anaweza kustahimili, ila vita vya muda mrefu, uchumi wake hauruhusu.