Issa Shivji: Ufutaji wa Uchifu Kisheria, ulitusaidia sana kujenga umoja wa kitaifa

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Posts
25,724
Reaction score
55,906

Kwani uchifu ni utamaduni wetu? Makabila mengi hawakuwa na wachifu. Waliwekwa na wakoloni kwa maslahi yao (km Wazanaki). Uchifu ulipigwa marufuku na sheria mnamo 1962. Machifu waliyokuwepo (km Adam Sapi, Fundikira, Kunambi nk) waliingizwa Serikalini katika nyadhifa mbalimbali.

Ufutaji wa uchifu ulitusaidia sana kujenga umoja wa kitaifa. Nchi zingine Za Afrika (kmNigeria, Ghana nk) wamepata shida kujenga umoja wa kitaifa. Sababu mojawapo ni machifu kulinda himaya zao kwa kukuuza ukabila badala ya utaifa. Tunachotakiwa kusisitiza ni utamaduni wa kitaifa.

Issa G. Shivji ni mwanasheria nchini Tanzania na mwandishi wa Vitabu, pia ni mmoja wa wataalamu bingwa katika Afrika wa sheria na masuala ya maendeleo.

Pia amewahi kufundisha na kufanya kazi katika vyuo vikuu mbalimbali duniani kote.


 
Hili mimi sikubaliani nalo ni siasa tu,hebu angalia hizi nchi jirani yetu,Zambia,Namibia,Botswana,SA etc etc bado zina viongozi wao wa asili na zipo na umoja na kimaendeleo wapo mbali mno kuliganisha na sisi,tuacheni maneno maneno tujenge nchi kwa misingi ya kisheria,fumua na ondoa KATIBA hii na tutengeneze KATIBA ya wananchi SIO politicians.
 
CCM wanautumia kuvuna wafuasi!
 
Unaongelea nchi zenye makabila mawili au matatu tu.
 
Uchifu ule na uchifu huu ni tofauti, uchifu ule haukuhusisha vyama vya siasa, uchifu huu unahusisha vyama vya siasa na ndiyo maana kwenye sherehe za Moshi zinazofanyika leo waalikwa ni wanaccm katika nguo zao! Mathlani wangetokea wanachadema wakiwa na nguo zao pasingetosha!
 
Kuta za chuo kikuu zimemlemaza Prof Shijvi: IGP mahita
 
Labda anazungumzia "Kaizer Chiefs Football club"😂😂 Eti Chief Mkwawa et al waliwekwa na wakoloni!!!..
What a joke !
 
Baada ya uchifu kuondolewa kisheria miaka ya 60 ,hawa machifu wa sasa wametokea wapi?wanaweza kuwa fake tu
 
Sisi ma chief lazima tuheshimiwe, unataka V8 apande pole pole peke yake?
 
Direct the information to Chief Hangaya.
 
Machifu wa asili waliondolewa lakini sasa kuna machifu wa kupigiwa kura, tunawaita wabunge, RCs, DCs na wengineo. Bora hata machifu wa jadi.
 
Ninachokiona ni kwamba CCM watawatumia machifu kuhakikisha wanaingizanseranzao kupitia machifu wakati wa uchaguzi ili waendelee kutawala.

Imagine kama Rais ndio wamemfanya mkuu wa wao maana yake wako tayari kupokea maelekezo kutoka kwake hii imekaa kimtego sana.
 
Wadau wote Tunajua Machifu waliwekwa kando ili kujenga Umoja wa Kitaifa na kuepuka Ukabila tena Enzi ya HAYATI BABA wa TAIFA
Toka imeingia AWAMU ya 5 naona Kasi ya MACHIFU kuibuka imekuwa kubwa kuliko AWAMU zote.
Tumeshuhudia Machifu wa Usukumani,leo Tumeshuhudia Wa KILIMANJANO
Nadhani Tutarajie Machifu wengi KUJITOKEZA.
 
Ndio shida ya kuwapa uongozi watu wasiojua historia ya nchi. usikute baada ya watu kuanza kuongea ndio na yeye kashtuka kama kaingizwa chaka
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…