Itashangaza Dunia kama Waziri wa Afya na Naibu wake hawatafukuzwa kazi ya uwaziri

Itashangaza Dunia kama Waziri wa Afya na Naibu wake hawatafukuzwa kazi ya uwaziri

vp umejiweka lockdown tayar?
Mwenzako huyo anavyo ropoka na mkamshangilia na kumpongeza kama amasema maneno ya busara kumbe ni ulevi wa madaraka .https://www.instagram.com/p/CLazp5gDQ9A/?igshid=x4v65qng0brb
 
Wana Jf kwa jinsi tulivyo katika kipindi kigumu ambacho kimezua hofu kwa kila mtu ni wazi kuwa Waziri wa afya na naibu wake hawastahili kuwepo kwenye hii nafasi mpaka sasa.

Mwaka jana bila kupepesa macho Dk Faustine Ndugulile alieleza ukweli umma wa Watanzania kuwa kujifukisha hakuwezi kuua wadudu wa Covid 19, hii ni sababu hawa virus wakiingia kwa binadamu huingia moja kwa moja kwenye mfumo wa kupumua( mapafu) hivyo hata ukijifukiza ni ngumu kuwaua huko ndani ya mapafu.

Mwaka huu baada ya dalili kuwa hili janga limerudi Tanzania kwa namna nyingine,maana inadaiwa sasa hivi kirusi cha korona kimejibadili. Tumeshuhudia madaktari wawili ambao wanasimamia wizara ya afya wakisisitiza watu kujifukiza. Je hawa watu kwa nini hawakutoa ushauri wa kitaalamu unaozingatia taaluma yao kama Faustine Ndugulile?

Leo hii toka watoe demostrantion namna ya kujifukiza hali inaonekana kuwa mbaya. Maana vifo vya vigogo mpaka makabwela vinazidi kupamba moto. Na tatizo ni hilo la kukosa uwezo wa kupumua.

Karne ya ishirini na moja kuongozwa na wasomi ambao hawezi kusimamia taaluma yao na kumshauri rais namna ya kukabiliana na magonjwa kisayansi ni aibu kubwa. Mawaziri hawa wawili wasisubiri vifo vya watanzania iwe sababu ya wao kujiuzulu.
Leo hii unamkana mwenezi wako kwa maneno mliyo yaona ya busara na kuyapongeza?
 
Hongera kwa Mara nyingine tena chagu wa malunde kwa kuwa mkweli. Mimi ni mkosoaji wako mkuu katika mambo mengi lakini unaposimamia ukweli lazima nikupe heko zako.

Kweli Katibu Mkuu Prof Mchembe ndiyo chanzo cha tatizo. Yeye ndiye aliyepeleka sampuli za oil chafu na mapapai kule National Health Lab.

Ni ajabu wasomi wa hali ya juu wanasaliti usomi wao kumfurahisha Meko
Tatizo dikteta amekamata mifumo yote
 
Na atakayewatumbua na yeye atajitumbua ? Unajua kabisa kinachotokea sasa ni kufuata maelekezo
 
Hapana bado ila nachukua tahadhari ,huku nikiendelea na mishe zangu.
Nalog off

then wacheni cheap politics, mnajua kabisa lock down is impossible sasa kelele za nn? unataka serikali ifanye nn? hata magufuli akismama akasema watu wamekufa na corona then whats next?
 
Mwenzako huyo anavyo ropoka na mkamshangilia na kumpongeza kama amasema maneno ya busara kumbe ni ulevi wa madaraka .https://www.instagram.com/p/CLazp5gDQ9A/?igshid=x4v65qng0brb

swali nlilokuuliza umelielewa lakini?
 
Wakuu (ukiwemo chagu wa malunde) ninaomba nakala ya kiapo cha uwaziri na unaibu waziri tafadhali.

Hongera Mkuu Chagu kwa kulisema hili .......
 
Back
Top Bottom